Idris Abdul Wakil ni nani hasa?

VOICE OF MTWARA

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
2,779
1,369
Nafahamu aliwahi kuwa rais huko Zanzibar lakini sina taarifa nyingi za kumuhusu

1. Historia yake ya kuzaliwa, makuzi na elimu yake
2. Historia yake kwenye siasa
3. Kwanini alitawala kwa miaka mitano tu tangu 1985 hadi 1990
4. Kwanini hakua maarufu ilihali ameishi hadi miaka ya 2000 alipofariki
 
Ni binaadamu kama wengine ila yeye alizaliwa 1925 huko Zanzibar, akawa rais wa Zanzibar mwaka 1985, ambapo alitanguliwa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi na kumaliza kipindi chake cha uongozi kwa muhula mmoja mwaka 1990 na kumpisha kiti cha urais Dkt Salmin Amour, ambapo mwaka 2000 Idris Abdul Wakil alifariki.

ᴱᵛⁱᵗᵉᶻ ˡᵉˢ ʳᵃˢˢᵉᵐᵇˡᵉᵐᵉⁿᵗˢ ⁱⁿᵘᵗⁱˡᵉˢ ᵉⁿ ᵒᵈʳᵉ ᵖᵒᵘʳ ᵃʳʳᵉᵗᵉʳ ˡᵃ ᵖʳᵒᵖᵃᵍᵃᵗⁱᵒⁿ ᵈᵉ ᶜᵒᵛⁱᵈ ¹⁹
 
Tunajua sera ya ccm ni rais wao kuongoza kwa miaka 10, ilikuwaje yeye akatawala miaka 5?
Huyo Bwana, kabla ya hapo alikuwa Spika wa Baraza la wawakilishi. Alitokea huko Unguja. Ile mwaka, 1985,ilionyesha Mwalimu alilazimisha jamaa awe mgombea wa U Rais, na Wapemba wengi wakimtaka Maalim Seif Sharif Hamad. Cha kufurahisha, pamoja na kuwa alikuwa mgombea pekee, alipata kura za ndiyo 58% na za hapana 41% . Kule Pemba, akipata za hapana zaidi ya 60%. Alipoapishwa, akamteua Maalim kuwa Waziri Kiongozi wake. Lakini, bado chokochoko kutoka kwa Wapemba hazikuisha. Pamoja na kuwa baadaye Maalim alitumbuliwa, uchaguzi uliofuata, hakutaka shida tena, akaamua asigombee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wa zanzibar ni watu wastaarabu sana

Mzee angepata za hapana nyingi si asingekuwa Rais, maana ilikuwa lazima upate ndio zaidi ya 50%
Na je kwa nini Nyerere alikua hataki Maalim seif awe Rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom