IDF yaonya Wairani kuondoka katika maeneo karibu na miundombinu ya kijeshi

IDF yaonya Wairani kuondoka katika maeneo karibu na miundombinu ya kijeshi

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Vikosi vya Ulinzi vya Israel vimetoa onyo la dharura kwa Wairani, na kuwaambia wakaazi kuondoka katika eneo lililo karibu na vituo vya kijeshi.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, akaunti ya IDF ya lugha ya Kifarsi inasema: "Watu wote ... waliopo ndani au karibu na viwanda vya utengenezaji silaha za kijeshi na taasisi zao zinazowasaidia wanapaswa kuondoka mara moja katika maeneo haya na wasirudi hadi watakapopewa taarifa zaidi.

"Uwepo wako karibu na miundombinu hii unaweka maisha yako hatarini."
Picha zaonyesha matokeo ya mashambulizi ya Iran nchini Israel
Ni saa sita asubuhi nchini Israel na sasa tunaona baadhi ya picha za matokeo ya mashambulio ya Iran.

Maeneo ya makazi yameshambuliwa kaskazini na kati mwa Israel baada ya Iran kurusha makombora ya balestiki kuelekea Israel usiku kucha ili kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye maeneo lengwa ya Iran.

Huduma za dharura za kitaifa za Israel zimeripoti kuwa takriban watu 10 wameuawa, huku zaidi ya watu 100 wakijeruhiwa.
 
Always Israel ana stick kwenye plan yake; hataki kuua raia, kafanya hivo Gaza, Yemen, kafanya hivo pia Lebanoni, na anafanya hivo Iran as well; tena anatumia lugha inayoeleweka na wenyeji; what a humanity. Sina hakika kama nimewahi kusikia jeshi lingine linafanya hivi popote duniani.
Yaaani muuaji akitoa taarifa kuwa atakuja kuua hivyo watoto waondoke ndio anahitaji kusifiwa?
 
Always Israel ana stick kwenye plan yake; hataki kuua raia, kafanya hivo Gaza, Yemen, kafanya hivo pia Lebanoni, na anafanya hivo Iran as well; tena anatumia lugha inayoeleweka na wenyeji; what a humanity. Sina hakika kama nimewahi kusikia jeshi lingine linafanya hivi popote duniani.
Ndio maana.mnawasoma kwenye Biblia km mfano wa binadamu bora
 
Back
Top Bottom