mwenzagu umetua lini kutoka sayari mpya kwa maana anachosema idd simba ni ukweli mtupu tena "from the horse's mouth". hujawai kuwa mwakilishi wa wananchi katika nchi hii wala mtoto pekee uliye na mshahara kutoka ukoo maskini. jamani penye ukweli na uhalisia tuseme na tukubali ili tutafute ufumbuzi.
hata huo mfuko wa jimbo wanaharakati waliupinga nao pia si wa mda mrefu kiasi kwamba haujabadilisha tabia iliyozoeleka ya mda mrefu ya wananchi kuwaomba wawakilishi wao misaada ya maendelo yao kama jamii au wao binafsi.
amini nakwambia hiyo posho itapitishwa hasira zenu mtazimalizia kwenye kura 2015 mtakaowachagua nao watazila na kamchezo kataendelea millele na milele sema amina.
Wewe ndiye unaishi kwenye dunia ya UTOPIA ndiyo maana hata hoja zako ziko pogo. Kama mimi ni
mtoto pekee kutoka familia masikini ninayepokea mshahara, mbona sijaomba niongezewe posho ili nipate
pesa nyingi ya kuigawia familia yangu?. Shirikisha akili zako wakati unapoandika.
Aidha I can bet my neck mimi tangu nianze kupiga kura hakuna hata mbunge mmoja aliyewahi kunigawia
pesa pamoja na kwamba mimi ni mpiga kura mzuri.
YES we will keep changing them hadi hii mind set kwamba kazi ya mbunge ni kuwagawia wananachi pesa
itakapobadilika. There is a light at the end of the channel. Waulize wapiga kura wa jimbo la Mwanza mjini.
Boman 1990 aligawa pesa wananchi wakampiga chini wakachagua mwalimu wa school Mabiti. 2010 Masha
amemwaga pesa wananchi wamepiga chini wamechagua a fresh graduate from SAUT Wenje.
Bottomline, hizo posho wanazotaka wabunge wa CCM waongezewe ili wapate ziada ya kuwagawia wananchi
ni HONGO, period. Tunajua Simba anajikomba kwasababu sakata lake la UDA liko bungeni hivyo anatafuta
huruma ya wabunge kwa mgongo huo. That is a child brain.