Idara ya Usalama wa Taifa ipewe Mamlaka zaidi ili kuinusuru Nchi

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) ni miongoni mwa Taasisi nyeti kabisa nchini kutokana na umuhimu wa majukumu yake.

Umuhimu wake unakuja kutokana na sabababu kwamba; nchi yeyote ile ni lazma iwe na maadui wa ndani na nje na ili nchi hiyo ipate kustawi, basi ni lazma maadui hao wadhibitiwe.

Baadhi ya maadui wanao hujumu nchi (wawe wa ndani au nje) wanaweza kufanya shughuli zao kwa siri sana lakini kwa ufanisi mkubwa na mazingira na mitandao wanayotumia kufanya uhalifu inaweza kuwa yenye utata na usiri mkubwa kiasi kwamba Jeshi la polisi kulingana na muundo wake haliwezi kugundua njama hizo bila kupata msaada wa vyombo vingine.

Kadhalika viongozi wa nchi huhitajika kufanya maamuzi wakiwa na taarifa za kutosha hivyo ni lazma wawe na njia inayoweza kuwapa taarifa juu ya mambo kadhaa ili wafanye maamuzi "With informed mind".


Pamoja na kuwepo kwa Taasisi hii inayoogopwa na wengi, kumekuwa na matukio mengi ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi kama vile Ujangili wa Tembo, Usafirishaji wa wanyama Hai nje ya Nchi,Ulipuaji wa mabomu ya kuua, Kuongezeka kwa ufisadi,Ufichaji wa fedha nje ya nchi,Uingizaji wa fedha chafu kwenye mzunguko,Rushwa kwenye mambo nyeti ya kitaifa na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja yanahatarisha usalama wa nchi yetu.

Kwa mujibu wa sheria iliyounda taasisi hii (TISS) ,yaani ; "TANZANIA INTELLIGENCE AND SECURITY SERVICE ACT 1996", Unakuta taasisi hii haipaswi kulaumiwa kwa kile kinachotokea nchini. Hii ni kwa sababu; kwa mujibu wa sheria hii,Taasisi hii imepewa majukumu ya kukusanya taarifa, kuzichambua, na kisha kushauri.

Wanaoshauriwa wanakuwa ni viongozi wa siasa wanaotokana na vyama vya siasa (Rais na Mawaziri) ambao licha ya kuwa viongozi wa kitaifa ; pia wanakuwa wamebeba ajenda zao za kisiasa,ajenda za vyama vyao na dhamira zao binafsi (ambazo zaweza kuwa za afya kwa taifa au hatari kwa Taifa). Kwa hiyo basi; Chombo hiki kinapokuwa kimemaliza majukumu tajwa hapo juu kwa kuishia na "kushauri"Kinakuwa kimemaliza majukumu yake kisheria (Bila kujali kama ushauri wake utafuatwa au laa) na hakipaswi kulaumiwa kwa kuwa sheria hairuhusu kufanya zaidi ya hapo.


Katika mazingira kama haya (ya kuipa TISS) Mamlaka kidogo namna hii, kimsingi kuna mambo mengi yanaweza kuhatarisha usalama wa nchi na huku kukiwa hakuna maelekezo ya kutosha ya kisheria kwamba nani afanye nini.Kwa mfano; Milipuko ya mabomu kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha; Upo uwezekano kwamba TISS Walijua, pengine wakashauri, na ushauri wao ukapuuzwa.(kama ambavyo naamini walikuwa wanajua kuhusu suala la kusafirishwa kwa Twiga hai lakini bado Twiga walisafirishwa). Kimsingi kama suala la Arusha lilikuwa ni tukio la kisiasa kama baadhi ya watu wanavyo sema,na ikiwa watekelezaji ni CCM; TISS, Kushauri ingekuwa ni sawa na kumshawishi boss wao asitekeleze kile anachodhani anatakiwa kutekeleza. Kwa hakika katika mazingira haya, inawezekana kabisa kwamba chombo hiki kinatekeleza majukumu yake lakini pamoja na hivyo matukio ya kuhatarisha usalama yanatokea kutokana na udhaifu wa kisheria.

Kwa kuendelea na sheria hii (1996) bado vyama vya siasa,Viongozi wa kisiasa, na baadhi ya watu wanaweza kuwa na nguvu kuliko TISS; Yaani TISS, inaweza kukusanya taarifa,kuzichambua na kuwashauri ila wakakataa ushauri na kutenda kinyume na kuvuruga usalama wa nchi.Katika mazingira haya upo uwezekano siku moja nchi ikaelekea tusiko kutegemea kwa kuwa si lazma kila mwanasiasa awe na nia ya dhati ya kuipeleka nchi mbele kwa kuwa viongozi wa kisiasa hupatikana kwa bahati nasibu kutoka katika jamii (jamii yenye watu wema na wabaya).

Katika mazingira haya mfanyabiashara mmoja wa madawa ya kulevywa anaweza kugombea ubunge, baada ya kupata ubunge akapewa uwaziri mkuu (by chance), baada ya kupewa uwaziri mkuu akawa anatumia nafasi yake serikalini na kinga za kiungozi kufanya mambo yenye manufaa kwake lakini hatari kwa taifa,TISS wakamshauri lakini akakataa.

Kimsingi taasisi hii ya Usalama wa Taifa sasa inatakiwa kupewa mamlaka zaidi na kuruhusiwa kuzuia matukio yoyote yanayoonekana kuwa ni tishio kwa usalama wanchi bila kujali mfanyaji ni nani(Wawe na nguvu ya juu kabisa katika masuala yanayoweza kuhatarisha usalama).Inatakiwa tuwe na dira,misingi na maadili ya taifa ambayo ni lazma yafatwe na kila mtu (kuanzia Rais na wengine wote) na mamlaka ya kuhakikisha kwamba misingi hiyo inafuatwa wapewe TISS. Hii itawasaidia kuwa na mmlaka kamili ya kutekeleza majukumu yao kama lilivyo jina la Taasisi yenyewe. Baada ya kukipa mamlaka hayo chombo hiki, mambo kama vile kuficha fedha nje, umafia kwenye siasa na mambo mengine kama mitandao ya madawa ya kulevya yanaweza kudhoofishwa sana hata kama yanafanywa na vigogo wazito.

Swali la kizushi:
Kama msajili wa vyama vya siasa anasema ikibainika kuwa waliolipua bomu Arusha ni CHADEMA atakifuta CHAMA, Lakini kama ikibainika ni CCM; Kwa kuwa ni chama tawala atakishauri. Je! ushauri wa Tendwa unaweza kuwa na nguvu kuliko wa TISS, na hivyo kuwa ni lazma ukubalike? Ikiwa sio, Je ikibainika ni CCM, halafu akawa shauri na wakakataa, TISS wakawashauri wakakataa, ni nani wakuwadhibiti? Je! Hali itakayofuata baada ya hapo itakuwa ya afya kwa nchi yetu kweli?
 
Hivi ni nani alileta hoja bungeni ya kuwa na sheria iliyounda USalama wa taifa (TISS) mwaka 1996 ?
 
Hivi ni nani alileta hoja bungeni ya kuwa na sheria iliyounda USalama wa taifa (TISS) mwaka 1996 ?
Nadhani ilikuwa ni hoja ya serikali kuirasimisha taasisi ambayo hapo kabla ilikuwa ikifanya kazi bila kuwa na muongozo wowote wa kisheria.Kufuatia sheria hiyo kupitiswa, sasa ndio ikatambulika kama taasisi rasmi na halali kisheria.
 
Nadhani ilikuwa ni hoja ya serikali kuirasimisha taasisi ambayo hapo kabla ilikuwa ikifanya kazi bila kuwa na muongozo wowote wa kisheria.Kufuatia sheria hiyo kupitiswa, sasa ndio ikatambulika kama taasisi rasmi na halali kisheria.
Baada ya kuirasmisha...kipindi cha Mkapa...ikawa rais sasa kuwa'track' wote waliokuwa kwenye kitengo hiki nyeti...ambapo hapo kabla hakikuwa rasmi.

Ndipo sa uhalifu wa EPA, richmond na mwingine kama huo ukaweza kutekekelezwa kwa urahisi...(Just thinking loud! may be I should think quietly as thinking loudly may cause serious errors )
 
Wazo zuri.
Wapewe na mamlaka ya ku-terminate viongozi wakuu wa nchi ambao kwa utendaji wao kwa sasa au badae wanahatarisha usalama wa taifa kwa sasa ama kwa vizazi vijavyo.
 
mada tete hii mkuu ngoja tukasome sheria.Naomba kuuliza,je TISS wanaolinda viongozi wakugundue una silaha eneo la tukio wataenda kufanya mashauriano wapi?PRESS YA MABERE MARANDO mnaikumbuka?Mwanahalisi lilipochomoka na watuhumiwa wa unyama dhidi ya Dottore ULI hawakuwa watu wa hii maneno inaitwa TISS?Na wewe mtoa mada,SHERIA HUWA VERY BROADER na kwa taasisi hii itakuwa broader kupindukia pia,kanuni zao huwezi kuzipata na operations zao bado si wazi kwa raia popote duniani.Tuendelee kuishi kwa imani+ mashaka +tahadhari+usugu kidogo.napita
 
mada tete hii mkuu ngoja tukasome sheria.Naomba kuuliza,je TISS wanaolinda viongozi wakugundue una silaha eneo la tukio wataenda kufanya mashauriano wapi?PRESS YA MABERE MARANDO mnaikumbuka?Mwanahalisi lilipochomoka na watuhumiwa wa unyama dhidi ya Dottore ULI hawakuwa watu wa hii maneno inaitwa TISS?Na wewe mtoa mada,SHERIA HUWA VERY BROADER na kwa taasisi hii itakuwa broader kupindukia pia,kanuni zao huwezi kuzipata na operations zao bado si wazi kwa raia popote duniani.Tuendelee kuishi kwa imani+ mashaka +tahadhari+usugu kidogo.napita
Mkuu kwa kiasi fulani pia inaonekana hata sasa hivi kuna baadhi ya majukumu ambayo chombo hiki kinatekeleza bila sheria kuwapa majukumu hayo (yaani wanatekeleza kwa uzoefu tu na kusoma mazingira na mahitaji )sasa hii ni hatari sana hasa kama siku ikitokea kwa bahati mbaya tukapata viongozi wa juu wa kisiasa ambao watakuwa wendawazimu.Yaani sasa hihi ni sawa na tunaishi tu kwa kuomba mungu kwamba ajalie wahusika wawe na nia njema.Ndio maana nasema ni muhimu kuwaongezea mamlaka kisheria katika maeneo yote yanadhaniwa ni muhimu
 
Hii ni topic nzuri, bila shaka yataendelea kutolewa maoni na mapendekezo mazuri, ili wenye macho na masikio waone na kusikia!
Swali ambalo Kila siku najiuliza bila kupata majibu... Hivi hiki chombo kikiboreshwa zaidi na kupewa nguvu( ki sheria na fedha), kisha kikatekeleza majukumu yake ipasavyo na kama yatakavyoainishwa, Je kwa style hii ya uongozi Wetu kuanzia Ngazi ya Taifa hadi mitaa, kuna atakayebaki madarakani??!
 
Mimi sio mweledi sana katika amda kama hizi (naziita mada za wakubwa) ninachoomba kwa wale mnaoelewa lolote la kuchukuliwa hatua, hii ndio sehemu yake ili raiya tuwe tumetimiza wajibu wetu na itabaki kazi ya tuliopwachagua kutuwakilisha katika utawala wa nchi hii kuyafanyia kazi haya.
 
Ni wazo zuri sana japo kuna side effects ambazo ni vyema kutazamwa.

Moja ni kuwa taasisi moja kuwa na nguvu sana kisheria ni tatizo, suppose ikiwa penetrated by local or foreign enemy (kama kinachotokea sasa kwa viongozi wa kisiasa) we may be in more serious trouble.

As we know intelligence community works by compartmentalization which means the limiting of access to information to persons or other entities who need to know it in order to perform certain tasks.

The basis for compartmentalization is if fewer people know the details of a mission or task, the risk or likelihood that such information could be compromised or fall into the hands of the opposition is decreased. Hence, varying levels of clearance within organizations exist.

Kwa lugha rahisi senior officers knows more than lower ranks hence if the organization is penetrated may cause higher damage to nation as whole.

Nakubaliana na mtoa mada, kuwa TISS wanahitaji kupewa meno but also kutoweka mayai yote kwenye kapu moja, yaani kuwe na taasisi zaidi moja with specific tasks i.e., uchumi, foreign security services, interior and those protecting natural resources and cyber communication

I believe this will reduce risks of intrusting our whole nation into hands of few people who may have individual interest as well
 
mimi naona ili kuimarisha tiss ni bora ikaunganishwa na millitary interigence na pccb vikawa vitengo vinavyosimamiwa na head mmoja
hapana.mimi naona si sahihi kuunganishwa na jeshi kwa sababu kama wakiunganishwa na jeshi tutakuwa tumelipa jeshi mamlaka ya kuingilia shuguli za kiraia, na kisiasa.
 
Inawezekana una hoja ya msingi sana katika mada yako hii lakini what begs the question is "Are these TISS guys really professional enough; do they really know what they are supposed to be doing katika idara hiyo nyeti au they are simply adding up the numbers and earning big salaries for nothing at the expense of the taxpayers?!

Nyara za serikali zinaibiwa, wako wapi!? mtafaruku wa gesi Mtwara; Kutekwa na kuteswa Ulimboka na Kibanda, milipuko ya mabomu; rushwa na ufisadi of astronomical proportions; extra judicial killings; wako wapi hawa!? have they been compromised or embedded!! if so what will be the effect or impact of what you are proposing; KUONGEZEWA MAMLAKA?! tudadavulie tafadhali?!
 
Ni wazo zuri sana japo kuna side effects ambazo ni vyema kutazamwa.

Moja ni kuwa taasisi moja kuwa na nguvu sana kisheria ni tatizo, suppose ikiwa penetrated by local or foreign enemy (kama kinachotokea sasa kwa viongozi wa kisiasa) we may be in more serious trouble.

As we know intelligence community works by compartmentalization which means the limiting of access to information to persons or other entities who need to know it in order to perform certain tasks.

The basis for compartmentalization is if fewer people know the details of a mission or task, the risk or likelihood that such information could be compromised or fall into the hands of the opposition is decreased. Hence, varying levels of clearance within organizations exist.

Kwa lugha rahisi senior officers knows more than lower ranks hence if the organization is penetrated may cause higher damage to nation as whole.

Nakubaliana na mtoa mada, kuwa TISS wanahitaji kupewa meno but also kutoweka mayai yote kwenye kapu moja, yaani kuwe na taasisi zaidi moja with specific tasks i.e., uchumi, foreign security services, interior and those protecting natural resources and cyber communication

I believe this will reduce risks of intrusting our whole nation into hands of few people who may have individual interest as well

Hapo kwenye mstari, issue ya "penetration" sio jambo geni katika espionage. Linatokea duniani kote. Soma vitabu kuhusu majasusi wa CIA kama Edward Lee Oswald, Albert Hansen wa FBI, na wengine walivyotumiwa na warusi kutokana na uroho wao wa pesa na wanawake. So la msingi sio kuogopa kuwa penetrated, bali kuwa na mbinu nzuri za counter espionage ili kuweza ku deal na foreign espionage ambayo hujumuisha hao penetrators [those who enlist the services of state agents -penetration- in a foreign environment]. So ni la kiutendaji zaidi na ni universal [lipo nchi zote duniani]... Kwa taarifa zaidi, soma hapa FBI — Aldrich Hazen Ames. soma pia hapa FBI — Robert Philip Hanssen Espionage Case.
 
The first advice from strategist master Sun Tzu in his art of war is to avoid war at any cost, also we know that kinga ni bora kuliko tiba hivyo I wouldn't define "laying down strategies to avoid penetration' as "being afraid of penetration"

We may differ in our opinion on this (which is good thing for any development) if necessary "agree to disagree" on this but I sincerely believe it is not right to rely on counter espionage which sadly may be a department which answers to the same director than formulating a secure system by distributing power to different agencies

Also kuhusu issue kama ya Lee Osward we are not sure if he real worked for foreign agency or he was just executing his directors orders, to me I think it is easy to bear the burden of being penetration by Russians (as of Oswald' case than of executing my commander in chief (cover))
 
Ndugu wana Intelijensia.
Naomba mpitie threads zifuatazo na kisha tuanze mjadala:
1.AJALI
2.WANAJESHI WAUAWA

Ukisoma taratibu kabisa na kwa kutafakari hizo thread mbili tu utapata kionjo fulani juu ya hisia za Wananchi, japo kwa sample ndogo, jinsi wanavyowachukulia viongozi wao na Jeshi letu adhimu JWTZ.
Kuna threads nyingine nyingi tu zenye ukakasi zaidi zinazoonyesha picha au taswira au mwangwi wa mtazamo wa wananchi kwa taasisi hizi, ukiachilia mbali jeshi la POLISI ambalo comment za raia zinatisha kabisa!

Nyie wenzetu wa Usalama wa Taifa mnaona mambo bado ni salama tu?
Sisi wengine tunatishika kidogo tukisoma hizo chuki za wananchi juu ya Majeshi na Viongozi wao wakuu!

Nini Kifanyike?
UWT mna weledi mkubwa kwenye kila nyanja zinazohusu Usalama na harmony ndani ya Taifa. Naamini hata kama kwenye majeshi yetu kutaonekana kuwa na kasoro fulani nyie mnaweza kuingilia kati kwa nguvu yoyote ile, licha ya kwamba mna watu wenu tayari huko!

Ndani ya miezi miwili iliyopita kumekuwa na lawama na malalamiko mengi sana juu ya JWTZ huko Mtwara kuwa linatesa raia, japokuwa habari hizo zinakanushwa na waandamizi wa Jeshi. Ni kweli gesi ya Mtwara inatakiwa ifike Dar, lakini UwT tumieni fani yenu kuharmonize hali ili mchakato huu mzima usiache madonda na makovu kwa raia na Taifa zima.

Kwa upande wa Thread inayomhusu Waziri Mkuu, naamini kuna mnaloweza kufanya, maana suluhu ya raia wanaokosea machoni pa Polisi wetu si KUPIGWA TU! Najua kauli ya Waziri Mkuu ni nzito sana kwa mfumo wa dola, lakini kama kauli yake inasababisha watu ndani ya Taifa kuichukia serikali yao kwa kiasi hicho, basi ni lazima kauli hiyo iwape UwT homework ya kufanya ili kurestore situation.

Najua kuwa mpo wengi humu mnasoma, lakini sisi raia tunategemea sana kuona mabadiliko kwenye mfumo kutokana na feedback hiyo ya raia dhidi ya Majeshi ya JWTZ, POLISI NA WAZIRI MKUU!

Ahsanteni.
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi hii, jukumu la chombo ulichotaja hapo juu linaishia kwenye kutafiti, kuchambua na kushauri viongozi wakuu wa nchi.Sasaa! mmmh!
 
Nia yako ni nzuri lakini sidhani kama Idara ya USalama wa Taifa itaweza kuondoa chuki za wananchi dhidi ya vyombo vya dola. Kwanza Idara yenyewe ni miongoni mwa vyombo ambavyo viongozi wengi wa kisiasa hawavipendi hata kama hawajui kazi zake. Kwa kauli za dr slaa dhidi ya usalama wa taifa, unafikiri kuwa yeye atajenga trust thidi ya chombo hiki. Mie naona tatizo si vyombo vya dola, tatizo lipo kwa wanasiasa wanaopandikiza chuki dhidi ya vyombo hivi
 
Kwa upande wa Thread inayomhusu Waziri Mkuu, naamini kuna mnaloweza kufanya, maana suluhu ya raia wanaokosea machoni pa Polisi wetu si KUPIGWA TU! Najua kauli ya Waziri Mkuu ni nzito sana kwa mfumo wa dola, lakini kama kauli yake inasababisha watu ndani ya Taifa kuichukia serikali yao kwa kiasi hicho, basi ni lazima kauli hiyo iwape UwT homework ya kufanya ili kurestore situation.


Piolisi hawatakiwi kupiga wakati wowote katika kazi yao.

Kitu kama hiki hakuna kabisa na wala si sehemu ya suluhu.
"suluhu ya raia wanaokosea machoni pa Polisi wetu si KUPIGWA TU!:"
Kupiga haimo kabisa katika utaratibu wa Kipolisi katika mazoea ya taratibu za Polisi , ndiyo kupiga ni utaratibu.
Polisi wenyewe binafsi ndiyo wamechukua sheria mkononi na kuamua kupiga watu.
Kupiga ni kwenda kinyume kabisa kisheria.
Jaji ndiye mwenye ruksa ya kutoa adhabu ya mtu kupigwa viboko ikibidi.
Na wato adhabu hiyo ya kupiga si Polisi.
Hata pale Jaji akitoa hukumu ya kunyongwa wanyongaji si Polisi
 
Mie naamini kuwa Idara ya Usalama wa Taifa inafanya kazi kubwa kuharmonize mambo katika nchi hii. Maana tunavyosikia na kuona nchi zingine ni tofauti sana na hapa tanzania. Ili watu wachukie vyombo vya dola, sharti pawepo mtu wa kutengeneza na kusambaza chuki hiyo.

Hapa Tanzania tuna wanasiasa wengi wanaoeneza chuki na kujenga uhasama wa vyombo vya dola dhidi ya wananchi. Kwa mataifa mengine, wanasiasa wachochezi mara nyingi huishia jela. Ila kwa hapa Tanzania, idara ya usalama wa Taifa inajitahidi kutoa ushauri ambao hauegamii upande wowote na ndo maana unaona kuwa akina mbowe wanahojiwa kwa ustaarabu mkubwa bila ya kuwekwa rumande.

Big up sana TISS. Ila nawaomba wanasiasa msiwalazimishe TISS wafanye yale ambayo yatawaumiza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom