Idadi ya walipa kodi yapungua

Acheni kutupanga hivi nchi hii kuna mtu alipi kodi, hivi miamala kwenye sim , malipo kwenye luku , maushuru mbalimbali ikiwemo maegesho ya magari sio kodi

Kwa nini mnataka fanya watz wajinga sana ,pumbavu
unaweza ukajiona una akili kumbe wewe ndo mpumbavu jielimishe au omba uelimishwe. Takwimu za walipa kodi hazijumuishi mambo ya kodi ya subunit unayonunua
 
Sisiem wamejaa wataalamu hamnazo.
 
Halafu unaambiwa TRA inavunja record kwa mapato kila mwezi toka mwaka uanze.

Dr Mpango ni mkweli mno mpaka wameamua kumpumzisha.
kwa upande wao wanakua kweli wamevunja rekod yaaan kua juu ya lengo kwasababu wao hupanga maybe tukusanye milion 100 so wakikusanya mil 111 wanakua wamevunja record. Sasa msingi wa hoja yetu tujikite kwenye malengo wanayojiwekea kwa kuzingatia tax to GDP ratio
 
Reforms hadi kwenye Ulipaji Kodi??
 

Naona umeonesha Nchi yenye walipa kodi wengi ni South Africa; ikifuatiwa na Kenya na Mozambique
Nafikiri moja ya sababu nikuwa na kodi rafiki inayolipika kirahisi; South Africa VAT kwao ni 15% Ikifuatiwa na Kenya na Mozambique ambao VAT ni 16%
Marekani ni kati ya Nchi inayo ongoza kuwa na walipa kodi wazuri Duniani ila ukiangalia VAT kwao ni 11%
Sijasema tupunguze kodi, nimetoa tu sababu...
 
Kwa mtazamo wangu hapa wanazungumziwa walipakodi katika nyanja zote maana kuna kodi zinazolipwa tra na ambazo hazilipwi tra. inawezekana kabisa tra wakawa wanavuka malengo ila baadhi ya sekta zingine walipa kodi wakawa hawapo. mfano kuna mtu anaweza kuwa na kampuni akawa analipa kodi au tozo au liseni ya kampuni baadaye kampuni akafunga na kuwa na bishara binafsi badala ya kampuni hivo tra wakawa wanapokea kodi yao kama kawa ila kwenye liseni ya kampuni katoka. huu ni moja ya mfano.
 
Biashara ya umachinga imerahisishwa sana,kuna walipa kodi wakubwa wamejificha kwenye machinga hususani Kariakoo

Maofisa usafurishaji Bodaboda , bajaj hawalipi PAYE, wenye mifugo, wavuvi, wakulima hawalipi PAYE
 

South Africa ajira zote katika Uchumi na biashara zipo rasmi hakuna kazi ndogo kudai kuwa wewe ni kinyozi au unaendesha daladala (taxi), kibarua, mvuvi, mlinzi, daktari, sangoma (mganga wa kienyeji), kibarua n.k hulipi PAYE

Tanzania watu wengi hawapo katika mfumo ndiyo maana hawalipi kodi. Dawa ni kuwa kama haupo ktk PAYE basi watu wote zaidi ya umri wa miaka 18 walipe kodi ya kichwa ili kuwepo usawa wale wa PAYE wasibebeshwe zigo pekee yao.
 
Mkuu hizo ulizotaja ni kodi za huduma. Na sio kodi binafsi.
Maana yangu kwa mfano ni kuwa usiponunua vocha basi upo salama au usipokuwa na gari basi pia upo salama.
Kodi inayoongelewa hapa ni kodi binafsi… twaweza iita kodi ya “kichwa” kwa maana nyingine.
 
VYANZO VINGINE TRA WAONGEZE WIGO WA PAYE

Makato ya PAYE South Africa yameelezwa

View: https://m.youtube.com/watch?v=RtI4Y5y9yYMWakubwa vigogo nao ni ma hustler wamesahauliwa kwa kuwa wanafanya kazi mfano BOT, TRA, HALMASHAURI n.k wana miradi ya mabanda ya kuku, nguruwe, bodaboda, bajaj n.k lakini hawalipi kodi za mapato yao yote kwa ujumla
 
Mfanya biashara wa karikakoo
1) Kodi ya mapato
2) Kodi ya pango
3) Kodi ya leseni ya biashara
4) Kodi ya service Levy
5) Fire
6) Usafi
7) Parking Kwa wenye magali
8) Kodi ya fremu
9) Kodi ya store
10) Kodi ya ulinzi


Lazima wapungue Kwa kufunga biashara au kutafuta njia mmbadala
 

Moja ya eneo ambalo lilikuwa wazi ni utoaji wa huduma za afya. Tulikuwa tunakata mti tuliokalia. Vituo vya afya vingi vimefungwa na wafanyakazi kuachishwa kazi. Hakuna aliyeingiza mguu wake kunusuru hili ila tunakuwa tayari kwenye kusoma matokeo yake.

Kama mwekezaji mfano: Aga Khan kafunga vituo 7 vyenye wastani wa kuajiri wafanyakazi 18 kwa kila kituo na bado anaendelea kufunga vingine. Hali ikoje kwa wengine na kwenye sekta nyingine?

Mbili, utitiri wa kodi usio na kuzingatia mfanyabiasha anapata nini bali unakadiria kwenye mtaji wake na kodi za kujurudia ambazo ilitakiwa kuwa hufuma kwa aliyelipa kodi ni mgandamuzo mkubwa. Wafanyabiashara wengi wanaona ni bora kuongea vizuri na mwakirishi wa TRA kuliko kulipa kodi yenyewe. Tume iliundwa ya kutathimini kodi hizi lakini kimya mpaka leo. Ingekuwa tume ya kugawanya majimbo, majibu ndani ya wiki mbili. Sijui vipaumbele vyetu viko wapi?

3: Kuambiwa ukweli hatutaki, tunapenda mapambio matamu.
 
Mbona tuliambiwa Magu aliua uchumi na mama anaufufua?
 
Je huku kwetu kukoje, Rais Makamu wa Rais Waziri mkuu Majaji Mawarizi Wabunge Wakuu wa Mikoa Wilaya n.k wanalipa kosi

Waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer alilipa kodi ya £54,718 mwaka jana

Waziri Mkuu Sir Keir Starmer alilipa ushuru wa pauni 54,718 mnamo 2023/24, kulingana na hati iliyotolewa na serikali.

Muhtasari unaonyesha alilipa ushuru wa pauni 152,225 za mapato katika mwaka wa kifedha unaoishia tarehe 5 Aprili 2024, kipindi ambacho chama cha Labour kilikuwa na upinzani.

Sir Keir alipata sehemu kubwa ya mapato yake kutokana na jukumu lake kama mbunge na kiasi kidogo kutoka kwa mirahaba ya vitabu na riba ya £5,174 ya pesa katika akaunti ya akiba.

Kansela Rachel Reeves na Naibu Waziri Mkuu Angela Rayner pia wamechapisha muhtasari wa masuala yao ya ushuru kwa mwaka huo huo.

Reeves alipata jumla ya £91,758 na alilipa £24,215 katika kodi ya mapato.

Chansela alipokea £12,372 kutokana na mapato ya kujiajiri, ambayo yalihusiana na mirahaba ya kitabu na ada za vitabu vya sauti.

Rayner alipata jumla ya £85,205 na kulipa £21,514 katika kodi ya mapato.

Mapato yote ya Rayner na manufaa yanayotozwa ushuru yalitokana na jukumu lake kama mbunge.

Bili ya ushuru ya Sir Keir ya 2023/24 ilikuwa chini kuliko mwaka wa fedha uliopita, alipolipa £52,688 katika kodi ya faida ya mtaji baada ya mauzo ya Desemba 2022 ya shamba ambalo sehemu yake linamilikiwa na mali ya babake.

Mswada wake wa ushuru mnamo 2022/23 ulikuwa chini mara tano kuliko wa Waziri Mkuu wa zamani Rishi Sunak kwa mwaka huo huo.

Muhtasari wa hivi punde zaidi wa Sir Keir wa mapato yake yanayotozwa ushuru nchini Uingereza, faida za mtaji na kodi aliyolipwa katika mwaka uliopita wa kodi kama ilivyoripotiwa kwa HM Revenue & Customs, ulitayarishwa na wahasibu wake wa kukodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…