Idadi mawaziri kivuli Mbowe kaonyesha kuridhishana nafasi badala ya kupunguza idadi ya wizara

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
Mbowetalk(3)(3)(2).jpg
Barazajipya-Mei10-2014.jpg

Umoja wa Katiba ya Wananchi Bungeni (Ukawa) umetangaza Baraza la Mawaziri vivuli kutoka vyama vya Chadema NCCR-Mageuzi na CUF.

Baraza hilo lenye mawaziri 25 kutoka Chadema , 11 wabunge wa CUF na wanne kutoka NCCR Mageuzi, lililowaweka pembeni wabunge wa TLP na UDP,lilitangazwa jana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni , Freeman Mbowe katika mkutano na wanahabari.

Akitangaza Wizara hizo, mawaziri na manaibu wao, Mbowe alisema

  1. Ofisi ya Rais(Utawala Bora), itaongozwa na Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema).
  2. Ofisi ya Rais(Menejimenti na Utumishi wa Umma), Waziri ni Vicent Nyerere (Chadema).
  3. Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Waziri ni Esther Matiko (Chadema),
  4. Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Waziri ni Mchungaji Israel Natse (Chadema) na Naibu wake ni Assa Othman Hamad (CUF).
  5. Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Waziri ni Pauline Gekul (Chadema),
  6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Rajab Mohammed Mbarouk (CUF),
  7. Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Waziri wake ni David Silinde.
  8. Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika, Waziri wake ni Meshack Opulukwa (Chadema) wizara hizo hazina manaibu.
  9. Wizara ya Nishati na Madini, itaongozwa na John Mnyika na Naibu wake, Raya Khamis Ibrahim wote kutoka Chadema,
  10. Wizara ya Fedha na Uchumi, itaongozwa na James Mbatia (NCCR Mageuzi) na naibu wake ni Christina Lissu (Chadema).
  11. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, waziri kivuli ni Ezekiah Wenje (Chadema) na naibu ni Haroub Mohammed (CUF).
  12. Wizara ya Katiba, Sheria na Muungano, itasimamiwa na Tundu Lissu (Chadema) na Rashidi Abdallah (CUF) atakuwa naibu.
  13. Wizara ya Ujenzi, Waziri wake ni Felix Mkosamali (NCCR Mageuzi),
  14. Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Magdalena Sakaya (CUF)
  15. Wizara ya Uchukuzi, itaongozwa na Moses Machali (NCCR Mageuzi) wizara hizo hazina manaibu.
  16. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wake ni Godbless Lema (Chadema) na naibu wake ni Khatibu Saidi Haji (CUF).
  17. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, waziri wake ni Halima Mdee (Chadema) na pia haina naibu.
  18. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Waziri ni Rose Kamili (Chadema), akisaidiwa na Mkiwa Adam Kiwanga (CUF).
  19. Wizara ya Maliasili na Utalii, waziri wake ni Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kadhalika hana naibu.
  20. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, itaongozwa na Joseph Selasini (Chadema), naibu wake ni Rukia Ahmed Kassim (CUF).
  21. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa itakuwa chini ya Masoud Abdallah Salim (CUF) ambaye hana msaidizi.
  22. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, waziri wake ni Susan Lyimo na naibu wake Joshua Nassari wote kutoka Chadema.
  23. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, itaongozwa na Dk. Gervas Mbassa na naibu Conchesta Rwamlaza wote wa Chadema.
  24. Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, David Kafulila (NCCR-Mageuzi).
  25. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia itaongozwa na Habib Mnyaa (CUF) na naibu wake Lucy Owenya (Chadema).
  26. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, waziri wake ni Barwany Salum Khalifan (CUF) akisaidiwa na Sabreena Sungura (Chadema).
  27. Wizara ya Kazi na Ajira, waziri wake ni Cecilia Paresso (Chadema). Haina naibu.
  28. Wizara wa Habari, Vijana na Michezo, waziri wake ni Joseph Mbilinyi (Chadema).

Awali akizungumza kabla ya kutangaza baraza jipya, Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe alisema baraza hilo litatoa taswira ya Ukawa ingawa tafsiri ya umoja huo ilionekana kwenye Bunge Maalumu la Katiba zaidi.

“Ushirika wetu, ulikuwa kwenye Bunge Maalum la Katiba lakini sasa tunauleta ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.,” alisema.

Alisema uteuzi wa mawaziri hao ulifanywa kwa makini na kila mbunge ana zosifa na uwezo wa kuwa waziri hivyo haukuwa na upendeleo.

Kwa mujibu wa Mbowe, awali Baraza hilo lilikuwa dogo kwa vile lilikuwa la chama kimoja na hivyo kwa sasa wamebadilisha Baraza na kwamba wajibu wa mawaziri hao ni kuwakabili wale wa CCM.

Mbowe alisema mawaziri kamili wa CCM wapo 28, wa upinzani wapo 28 huku manaibu mawaziri wa CCM wakiwa 22 na wale wa upinzani wapo 12.

IPPMedia publications
 
Baraza jipya la mawaziri kivuli Mbowe ameonyesha kurudi kule kule wanakofanya serikali ya CCM kujazana kwenye nafasi kwa kudhishana badala ya kuachiana nafasi kulikotazamiwa kwa ajili ya kujenga mshikamano. Idadi ya mawaziri waliokuwa chadema inaonekana kutopungua isipokuwa Zitto Kabwe ambaye kesi yake inaendelea mahakamani. Labda hawakuwa tayari kuachiana nafsi kwa ajili ya wapya, hapa ni udhaifu wa waziwazi.

Nilitazamia Mbowe apangue kwa kupunguza idadi ya mawaziri kutoka Chadema ili kuwapa nafasi wapya anaowaingiza kutoka Ukawa.

Sijaona dhana ya kubana matumizi ambayo upinzani unataka kuonyesha dhidi ya baraza la mawaziri lililopo, vinginevyo naona kama kilichofanyika ni usanii wa maigizo.

Katika hili Mbowe kateleza.
 
Hili baraza ni hewa, hakuna ishu hapo, jana prof kahigi ameshindwa kusoma hotuba ya wizara yake kama waziri mpya kivuli....kituko cha mwaka
 
Nauliza hivi hawa mawaziri vivuli huwa wanalipwa chochote?

Walipwe wasilipwe lakini dhana kamili huwa kioo chao kwa kile wanachoona si vema kinachofanywa na serikali iliyopo madarakani, cha ajabu wampanga safu vile vile nini sasa dhana ya kubana matumizi? Tulitegemea wangefanya kili wanachokazania kwenye rasimu ya katiba, lakini sivyo.
 
Back
Top Bottom