Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Yeah hii inalipa ndio tena sana tuu lakini uwe unajitahidi kubalance sukari kwa maana raia wengine hawapendi sukari nyingiiii!!
 
Kwahiyo tofauti na ubuyu au ukwaju, kuna ice cream gani nyngine mtu anaweza kutengeneza? Na je, unga wa ngano unahusika kotekote?
 
Mie naomba nifahamishwe jinsi ya kutengeneza za maziwa natengeneza za ubuyu na ukwaju ila wateja wanataka za maziwa.

Yanatumika ya unga au?
Vipimo maji sukari maziwa je?
Natanguliza shukran
 
Nsemwas Junior,

Kwa haraka haraka mtu anaweza kukuona kama mjinga au mtu aliyeshindwa maisha lakini una akili sana na inshaalah mungu atakufanyia wepesi. Napenda kukushauri kwenye swala la MARKETING ambapo ukicheza vizuri unaweza kuishi maisha ya kutembelea gari hata kwa hiyo biashara yako ya Ice cream.

Kwenye marketing kuna P's na mojawapo ni Place yaani sehemu ambayo bidhaa inaweza kuuzwa au sehemu ya kufanyia biashara husika. Hapa kwenye place kuna maajabu makubwa sana tena ni miongoni mwa maajabu makubwa sana katika dunia ya biashara, ukiwa mbunifu katika biashara yako hiyo ya ice cream na ukaitumia Place kwa makini nakuhakikishia utakua unakaa na remote mkononi unatizama TV nyumbani halafu hela ya kutosha inaingia kiulaiiiiiiini.

Swala la ugumu au ulaini linatokana na Ratio au wastani wa maji na hicho unachochanganyia kwenye ice cream zako, nakupa ushauri wa sisi magenius kama ifuatavyo; kama unatumia ukwaju nunua kilo moja halafu igawe mara nne yaani uwe na robo nne kila moja uiweke kivyake, halafu baada ya hapo robo moja changanya na maji robo lita, ya pili changanya na maji nusu lita, ya tatu changanya na maji nusu na robo ya lita halafu robo ya mwisho ya ukwaju changanya na lita nzima moja ya maji na ukimaliza kufanya haya gandisha zote kwakuzitenganisha kwa alama ambayo itatofautisha kiwango cha maji ulichoweka.

Baada ya kuganda chukua ice cream moja kila upande ili upime menyewe ugumu na ulaini, nafikiri kwakufanya hivi utapata ice cream laini na ngumu katika hizo ulizozigandisha. Pia katika vipimo hivyo vya maji bila kuongeza wala kupunguza unaweza kuongezea moja katika aina za biskuti zinazouzwa madukani au matunda fulani ambayo hayawezi kuiathiri radha husika unayoitaka kwa kiasi kulingana na bei ambayo unauza hizo ice cream zako.

NB: Kila biashara inaweza kukupatia kipato kizuri katika maisha lakini inategemea unaifanya vipi na katika mazingira yapi.
 
Portable ice cream maker

54eb2e6a6b5d3_-_ice-cream-makers-hamilton-beach-15-quart-0610-s3.jpg


mkuu tuongee biashara ni PM

mkuu tuongee biashara ni PM
hivi hiyo yako au na unaiuza au?

N

Ni vyema kufungia vifuko vya karanga. Mfuko upo kwenye rola haina usumbufu katika kujaza. Unafunga kwa mashine zinauzwa 50,000 zinatumia umeme. Hizi ni za kuchomea tu
Ok

Hello friends,

Nitajibu comment zenu ila kwanza nianze na junsi ya kutengeneza ice cream za ubuyu.

Mahitaji
1. Ubuyu(tsh 2000 kisado)
2. Maji
3. Rangi(tsh100)
4. Ladha(tsh1000)
5. Sukari (tsh1300 nusu)
6. Vifungashio (tsh 500)

Kwa kipimo cha sado moja ya ubuyu utapata icecream nyingi zaidi ndio maana sukari itakua nusu. Sasa hapa ili upate bidhaa nzuri unafanya hivi chukua maji weka kwenye sufuria yenye ukubwa wa kutosha weka ubuyu wako kisha bandika jikoni (ubuyu ukibandikwa jikoni icecream yako itakua haibakizi kile kijiwe cha mwishoni ambacho hakina ladha ila inakua laini kabisa, japo unaweza kuloweka tu bila kuchemsha)

Funika sufuria yako utakua unafunua kukoroga ili ubuyu na mbegu viachane. Ikifikia hatua ubuyu unachemka tayari mbegu na ubuyu wa nje vitakua vimeachana epua subiri vipoe. Sasa chuja mbegu na uji uji wa ubuyu weka uji wako kwenye chombo kingine sasa ongeza maji taratibu huku ukikoroga ili kupata uzito wa uji ubaotaka usiweke maji mengi sana ikawa maji kabisa. Baada ya hapo malizia kuweka sukari, rangi na ladha unayotaka mie hutumia passion. Funga bidhaa yako gandisha, kazi imeisha unasubiri mkwanja tu.

Kwa mnaosema icecrean ni 100 tu, you are very wrong. Hata maandazi kuna jingine huwezi uza zaidi ya 100 lakini andazi hilo hilo duka la pili linauzwa 500. What matters ni ubunifu katika kazi yako; mimi huuza 200 na nikiitwa sehemu napeleka kwa 300.

Pia icecream sio spesho kwa watoto tu. Ukitengeneza vizuri hata watu wazima watanunua tu mbona (ukwaju wa Bakhresa unaliwa na kila rika?) Ile ni icecream tu kama hizi za kawaida sema kaboresha package na ubunifu. Mie siwauzii watoto tu, napata oda hadi za maeneo yenye mikutano japo I'm m still growing. Hivyo, kama unahisi upo kwenye nafasi ya kufanya hii kitu usiichukulie poa its a deal.

Kuhusu fridge, labda niseme hivi: ukiamua kweli kweli na ukiona unaweza kufanya hii kitu basi tafuta hata ki freezer used ufanyie kazi ama kama home kuna fridge basi ifanye iwe ni kama asset sio kuweka nyanya tu. Tuamke vijana wenzangu tusisubiri ajira tufanye yaliyopo kwenye uwezo wetu wakati tunasubiri hayo mambo mengine.
 
Mimi natumia ubuyu wa unga, naupika kama uji nauacha unapoa kabisa, kisha nakadiria maji ya size, naweka sukar na kisha naweka ladha. Baada ya hapo naweka rangi ninayoipenda. Maji yakizidi zinakua ngumu.
 
Ukijibiwa nitafaidika nami!
Hata mimi pia nahitaji hizo mashine ndogo, hizo kubwa nmeziulizia Zanzibar bei yake ni mil3.5 zipo za mil3, na za mil2.9 nazo ni mpya used sijazipata hata hizo ndogo cjazpata ila nahitaji sana hizo ndogo za bei nafuu. Nipo Znz ila muda c mrefu nitarudi DSM.
 
vidudi,

Wakuu mimi nimesaidia tu kuwapa idea kuwa zipo ndogo mpaka portable kwa bei isiyozidi laki, sasa ni kazi kwako kutembelea supermarket kubwa sidhani kama utazikosa na hata kama hawana ukipress order watakuletea, kwa wastani zipo hadi za US dollar 50.
 
Wakuu mimi nimesaidia tu kuwapa idea kuwa zipo ndogo mpaka portable kwa bei isiyozidi laki, sasa ni kazi kwako kutembelea supermarket kubwa sidhani kama utazikosa na hata kama hawana ukipress order watakuletea, kwa wastani zipo hadi za US dollar 50
Naomba kufahamishwa maeneo husika zinako patikana hizo portable.
 
Au naomba link yao
Amazon.com zipo lakini hata alibaba hazikosi,wewe google min icecream maker kisha angalia image zake na link zipo,halafu humu mbona kuna watu wanafanya hizo kazi unaweza kuwapa order unahitaji ya ukubwa upi na ya bei ipi na wakakuletea.
 
Amazon .com zipo lakini hata alibaba hazikosi,wewe google min icecream maker kisha angalia image zake na link zipo,halafu humu mbona kuna watu wanafanya hizo kazi unaweza kuwapa order unahitaji ya ukubwa upi na ya bei ipi na wakakuletea
Ahsante sana mkuu, ila nilishawahi weka tangazo kuwa mwenye nazo hizo mashine ila sikupata support
 
Back
Top Bottom