manchoso
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 1,605
- 2,058
shetani huweza kuzalianaHivi shetani wanazaliana kama sisi??
Mungu anasema katika vitabu "tumejaalia maadui katika kila Mtume,nao ni mashetani katika watu na mashetani katika majini "
kwa uelewa wangu wa maandiko na imani yupo shetani mkuu na wapo shetani wadogo
Na Mungu ameumba kila kitu katika pair dume na jike
na wale wanaomfuata shetani katika majini na wanadamu nao huitwa shetani,
Wakati mwingine pia shetani yaweza kuwa sifa zaidi kuliko umbile,
katika macho yako yaweza ukamuona fulani ni binadamu lakini mbele ya Mungu yeye akawa shetani kutokana na matendo yake
na ukiacha yule shetani mkuu alielaaniwa na hatasamehewa na Mungu, hawa wadogo huweza kutubu wakiona haki na kuwa watu wazuri mbele ya Mungu japokuwa kama alivyoeleza mshana jr yule shetani mkuu mara zote atataka kuwavuta kwake wamkufuru Mungu