I wish nisingekutana nae | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I wish nisingekutana nae

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Raia Fulani, Feb 6, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  ni binti mzuri sana kwa kumtazama. mweusi wa kuvutia, umbo jembamba lililogawanyika, si mrefu si mfupi. uzuri wake ungekolea pale ambapo angepata hali bora zaidi ya kimaisha. nasikitika kusema nimeachana nae pamoja na yeye kunipenda upeo japo ni muda mfupi tu katika mahusiano yetu. niliumia kuona ninamwacha ingawa sikutaka kuwa nae. aliumia mara dufu yangu na maumivu yake niliyaona na kuyahisi. sikupenda hali yake. sikuipenda familia yake. sikuyapenda maisha yake ya awali. sikupenda anapoishi. sikulipenda kabila lake. nilimpenda yeye tu! ningetamani kuwa nae lakini ndoa ni mfumo. unahusisha koo mbili na zaidi na kuzifanya familia. yaweza kuwa ni ya kutunga ama ni kweli, lakini mapenzi ni nini? usitake kujua undani zaidi ila yatafakari haya kwa sasa.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  Wewe hata yeye "hukumpenda" vilivyo, period.

  Watu wameacha ufalme wa uingereza kwa ajili ya "mapenzi" wewe unataka kuleta geresha za visingizio?
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  kuna mazingira ya kumpenda mtu na ya kumchukia mtu. ufalme una sababu zake na ziko wazi, hili si suala la kifalme, ni maisha halisi.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Ukilipenda Boga, penda na Majani yake!

  In any way, yeye yuko attached na kwao, ndugu zake, kabila lake, na kila kitokacho kwao, so sio rahisi akakubali ukampenda yeye tu, na kuidharau lineage yake...huh!

  Hayo ni mapenzi ya KUWAKA TAMAA ZAIDI, KULIKO mapenzi ya moyoni!

  Usimpotezee muda mtoto wa wengine babaake!
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  sure, thanks. wahusika walishaliona hilo na kulitengua mapema
   
 6. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  ...usingekutana nae ungejifunzaje hayo? ...learn from it!
   
 7. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  pole sana! thats life...
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2010
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Story yako imenigusa sana Kingi kwani na mimi kuna binti mmoja tuliingia kwenye mapenzi kupitia simu na email sasa tumeonana nimegundua kuwa simpendi kama ambavyo nilikuwa nahisi mwanzo, napata tabu sana manake yeye anaonyesha kunipenda sana wakati mimi kama vile najisukuma kumpenda kitu ambacho naona kitatuletea matatizo baadae. Am in dilemma
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  pole pia mkuu. Haya mambo yapo na wanawake wapo desperate kumpata mwanaume wa kufanya nae maisha. Ukichelewa kuuvunja huo uhusiano itakuwa tabu sana kwako. But utumie diplomasia sana kutengana. Kila mtu anapenda kuwa na uhusiano anaoutaka.
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Feb 6, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Daa umenigusa...inafanana na stori yangu!
   
 11. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani poor her!
   
 12. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Iliwahi kunikuta hiyo ya kupendwa na demu kuliko nilivyompenda yeye (mara nyingi hiyo unakuja ku-realize that later on). Yeah huwa ni bonge la dilemma, hasa jinsi ya kuterminate hiyo relationship as amicably as possible.

  Unakuta demu anaanza ku-dream aloud about your future together as a family. Hiyo ndiyo itakuchanganya kabisa.
  Think hard about what YOU want, and take action sooner rather than later.

  To Kingi: Usijutie hiyo experience, learn from it to go forward.
   
 13. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,581
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  ..........Wewe bana hukupenda acha longo longo, mapenzi hayana masikini wala tajiri.Kuna watu wana mapesa yao ni matajiri haswa na wameoa mwanamke ambaye kwao ni fukara lakini anamuinua na kumbadilisha kabisa.
  .........Wewe Sipo hebu achana na mambo ya kutafuta mwanamke online, tafuta mwanamke live umuone na kupenda tabia zake then muelewane.Haya mambo ya kutafuta mtu online ni wizi mtupu, at the end of the day ndio yanakuja hayo uliyoyasema hapo juu kwamba hujisikii kumpenda.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Feb 6, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,524
  Trophy Points: 280
  Una busara sana Mrembo. Kweli mambo ya online ni kuzugana na kuyeyushana tu. Huwezi ukamjua mtu online. Ni vizuri kukutana na mtu ana kwa ana na ni vizuri wewe na mtu huyo msiwe mnakaa mbali kiasi cha kufunga safari mkitaka kukutana.

  Kukutana ni mahali popote pale lakini kukutania online kunazidisha uwezekano wa mambo mengi hasa kudanganyana. Ana kwa ana inatoa fursa ya kumsoma mtu vizuri na kumjua zaidi. Binafsi kamwe sitilii umuhimu hata kidogo kukutania na mtu online.

  Otherwise mtu usipotaka kuvunja au kuvunjwa moyo ni bora kutokuingia katika uhusiano na mtu yeyote. Katika maisha yangu mafupi hapa duniani nimekuja kugundua binadamu ni viumbe walio si wakweli kwa asili na wasiotosheka. Kama upo kwenye uhusiano na mtu basi ukae ukijua kuwa ipo siku na wewe utavunjwa ama kuvunja moyo wa mtu. Kibaya zaidi mambo ya kuibia hufanywa kisirisiri na mtu unaweza hata usijue kuwa mwenzako anakula uroda nje na ukadhani mko kwenye mapenzi ya kweli kumbe wapi, mwenzako anakuchora tu. Ila unapokuwa uko mwenyewe (single) hakutakuwa na mtu atakayekuibia na kula au kuliwa uroda nje ya uhusiano wenu. Mimi nilishagaamua kufuata njia hii zamani.
   
 15. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Umemwacha bila kumwachia mimba?
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  una maneno mazuri ila ujue kuna umasikini na staili ya umasikini. Mwingine wa uzembe na mwingine huna jinsi. Umezungumzia variable moja-umasikini. Mi si tajiri najaribu kujipa option maishani. Umasikini si kigezo cha kutompenda mtu, so dont judge on that ground
   
 17. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 526
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Lets be serious. Huyu sio wa kupewa pole. Wewe ni mchafuzi tu, kumpotezea binti wa watu muda. Love is not selfish, love does not ask why... kabila, hali ya maisha...samahani lakini kaka inaonyesha jinsi ulivyo na narrow-mindedness.

  Nilidhani hii ni forum for Great Thinkers!
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,217
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  mwisho wa siku upweke utakutafuna. Jibu ni kuwa na mwenza ila omba asikuletee maradhi. Kumdhibiti mwenza ni sawa na kujaza maji kwenye gunia
   
 19. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #19
  Feb 7, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,524
  Trophy Points: 280
  Hapana. Sikusema usitoke na mtu au usiwe na marafiki kabisa. Watu wa kumega hawaishi. Wapo tu siku zote. Upweke utakuja kama huna mtu yeyote kabisa katika maisha yako. Lakini kama ulibahatika kuwa na watoto, kama una ndugu mlio karibu, kama una jamaa na marafiki sidhani kama upweke utakutafuna.

  Ninachokataa mimi ni kujikita katika ile wazungu waitayo "monogamous relationship" au "exclusive dating". Kwangu mimi hiyo kitu haipo. Ni kudanganyana tu.
  [​IMG]
   
 20. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Umemwacha binti wa watu kwa sababu hukulipenda kabila lake, hukuipenda familia yake, nk. Kwa maneno haya napata picha kwamba wewe ni mtu mbinafsi kupindukia, tena mwenye majivuno ya hali ya juu yaliyochanganyikana na madharau. Na kwa jinsi hiyo hata huyo binti hukumpenda kama unavyotaka tuamini bali ulijipenda mwenyewe, ukaitafuta nafsi yako na kutaka kuishibisha kisivyo halali. Nikwambie ukweli: mapenzi ya kweli hayaangalii nasaba ya mtu, kabila, utajiri, nk. Mapenzi yanavipiga chini vizingiti vyote hivyo. Ukiona hivyo vitu vimekuwa vipingamizi kwako ujue ulikuwa hujapenda, ulikuwa unacheza movie za Hollyhood ukaziita ni upendo. Pole ndugu. Kwa mtind huo itakuwa vigumu kupata mke wa kuoa kwa sababu ya sababu nilizozitaja hapo juu. Unahitaji kujinasua na utumwa wa kifikra, na prejudices.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...