I will kill him 4 my kids | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I will kill him 4 my kids

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sabry001, Jul 4, 2011.

 1. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Nina rafiki yangu alitengana na mumewe kwa miaka 6 sasa na mwaka jana wamepeana talaka rasmi.Huyu dada ni m2 strong sn kwani alipotelekezwa alijikaza akajisomesha huku anatunza watoto wake na sasa yuko chuo kikuu mwaka wa pili. Kuna ki2 kinamtesa dada huyu yani akipata mwanaume mtalaka wake huwa anaingilia mahusiano hayo ingawa alishaoa mke mwingne. Miaka 2 baada ya mwanaume kumwacha alipata mpenz jamaa alipockia akamvizia yule kaka akampiga sn so dada akamwagwa, mwaka mmoja bdae tena akapata mwingne nae akatishiwa akamwagwa tena, akaona bora apate talaka ndio atakuwa huru, mwaka jana walitalikiana ila mambo ndio yamekuwa mabaya zaidi, yule kaka alimwapia akiwa na m2 mwingne atamuua kwan ye bdo ni mkewe kwan walifunga ndoa kanisani na ndoa ya kanisani haifi. Akamwambia atamtesa hadi amrudie ila kwa vile dada ni strong akamwambia afanye atakavyo bs kaka yule ameanza kuchawia watoto aliokuwa amezaa na yule dada (watoto wanakaa na mama) anawapiga watoto wake majini, wanamsumbua sn huyo dada. Sasa amechoka hana raha tena kwani shule hasomi kwa raha kwani watoto wanaugua ugua (kipepo, wakipelekwa kwa walokole wakiombewa wanapona) akipata mwanaume wanatishiwa wanamuacha, amekuwa mpweke na anakaribia kuchanganyikiwa. Amepanga ki2 kibaya sn na amenishirikisha nikaogopa ndio mana nikaleta hapa jamvini kwani anataka kumrudia mtalaka wake kwa siri then cku moja amtaftie wahuni wamfanyizie. Nimeogopa na kuona madhara ya hlo jambo ila ndio alichoamua. Alisema maneno haya "NILIMPA MOYO WANGU, MAISHA NA WATOTO, SASA ANATUTESA, ANATAKA TUFE, BORA ANITESE MIMI KULIKO WATOTO WANGU, WAMEMKOSEA NINI? I'LL KILL HIM 4 MY KIDS" ushauri wenu plz NITAMSHAURI NINI AACHE WAZO LAKE? Nisaidieni plz
   
 2. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Cha kumshauri sina hili jambo ni zito. Mtu atarogaje wanawe wa kuzaa? Ila wadada muwe makini mnapoolewa koo nyingine wanga. Kama kweli huyo mwanaume anafanya hayo anayofanya basi ajue alikuwa anaishi na shetani miaka yote. Uchawi upo mshirikisheni Mungu kabla ya kuolewa.

  Kama ni mkistu awapeleke watoto kwenye maombi. Kama mwananume ana wazazi amshitaki kwa wazazi wake. Au walikutana mjini wazazi hawajuhi? AU wazazi nao wanga?
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mapenzi ya mama hayo....kusema ukweli hiyo hali waliyofikia ni hatari sana.

  Kitu ambacho ningeweza kumshauri huyo dada ni kama kuna uwezekano wa yeye kuhama afanye hivyo.Ahame mkoa hata nchi ingewezekana ingekua safi zaidi akaanze maisha mapya huko bila bugudha za huyo mwanaume....bila kumtaarifu ofcoz!!

  Maana kukaa kwake karibu kunampa huyo mwanaume fursa ya kujua nini kinachoendelea na mwanamama pia namna ya kumharibia pale anapotaka.Huyo dada akifanya hivyo anavyofikiria atakua hawatendei haki wanawe though kwa sasa hivi anaamini kwamba atakua anawasaidia sivyo....kufanya hivyo kunaweza kumuondolea amani hivyo kushindwa kuwalea watoto wake vizuri na kuishi maisha yake kwa furaha...au akaishia kugubdulika na kupatikana na hatia watoto wabaki bila mama wala baba wa kuwaangalia.

  Natumaini atapata namna sahihi zaidi ya kuondokana na hilo janaume....i really do!! Mpe pole sana!!
   
 4. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hapa nimesamarize tu dada. Wakwe wanajua na wanamsapoti kijana wao kwa kuoa mke wa pili na walimwambia huyu dada aende akasafishwe nyota alipokataa chuki ikazidi zaidi. Maombi yamemsaidia sn
   
 5. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole zake huyo dada! Hilo analotaka kufanya si njema kabisa kwa maisha yake! Ni bora autafute msaada kwa Mungu, hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Akitulie kwa Mungu, Mungu atamsaidia kumdhibiti huyo mwanaume, na kamwe hatamfanya kitu chochote!
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wote hawafai hawa ni makatili hawafai .
  Yeye kajuaje kama anawaloga hao wanawe?
  Na huyo mama ni mganga.

  Sasa atafia jela na kuwaacha hao watoto wagonjwa wawasumbue watu.
  Ajitahidi kumuomba mungu na kumuachia mungu.
  Imeandikwa nitakupa jaribu na nitakupa njia ya kutokea.
  Hilo jaribu ni saizi yake amuombe mungu atafanya njia na atashangaa!
   
 7. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  anatakiwa kushika dini ili aweze pambana na nguvu hizo za giza na ushetani wote wa huyo mtalaka wake.
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,753
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio ninaposhangaa kwa tabia fulani za kibabe ambazo hazina msingi wowote,..mwanamke umeachana nae tena muda mrefu_umepata mwanamke mwingine na kuoa lakn unataka mwenzio asiolewe wala kuwa na mpnz,...huu ni upuuzi , unyanyasaji,ukatili,ubinafsi,ubabe,na ujeuri uliopindukia wa kuthamini furaha na heshima yako bila kujali furaha na heshima ya watu wengine.

  Kuhusu hilo suala la kuroga watoto...hapo sitii neno kwani siamini sana kama mtu kweli anaweza kuloga watoto tena watoto wake wasio na hatia hata chembe,....ila inawezekana tu kwa mtu mkorofi na jeuri wa aina ya huyu jamaa.

  Muda mwingine sisi wanaume pengine hatuwatendei sana haki hawa wapenzi wetu......tunawaumiza sana na inatia hasira na uchungu sana kama angekua dada ako sidhani kama akifanyiwa hivyo kama utaridhika,......makosa mengine pengine yanastahili adhabu ya kifo,....nimenuna na kukereheka sana na tabia hii
   
 9. c

  charndams JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 437
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  ni jambo la kuhuzunisha sana. haya mambo huwa yanatokea sana kutokana na wivu wa wanaume. ila cha kunishangaza ni jinsi gani mwanamume anaweza kuwatendea wanae unyama...i think its a bit awkward. hapana fanya tena intensive research uone kama kuna ukweli wa uchawi dhidi ya watoto.
   
 10. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  1. Mungu yupo and Uchawi Upo, ni rahisi zaidi ku solve hili with God's Kingdom than Devil. With God haita guarantee pia quick solutions.......Hata
  watakatifu wanapata majaribu makali na ya kutisha wakati fulani.......

  2. Kuna logic fulani.......sometimes its logic kupoteza one person over 3, Meaning As a driver, your car break has failed and you cant help
  iit.......you find 5 men at work on your driving side and 1 person on the other side.....what u do......kill five rescue One or One over five?,
  Theres a time for every thing soma Ecclesiastes nadhani 6.............

  3. Kuna kitu chochote hajasema? any hidden facts?,

  4. Dunia sasa ni more than building, roads, and a like, Binadamu are worse than animals, Niliwahi kuambiwa you better meet a lion...once you
  succeeded your escape is once for all....but not these modern human being........................

  5. For ufalme wa Mungu, sali sana, samehe and treat it like Watoto ni wa Mungu, hata Baba yao ni wa Mungu pia.....Usihukumu.........Ki Dunia
  Dunia....Fight and protect whats yours and what you believe is right.........

  Keep updating us...
   
 11. Sabry001

  Sabry001 JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,064
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  sio matani hapo kuloga mazeeWATOTO WAKIOMBEWA PEPO WANALIPUKA WANASEMA NA ALIEWATUMA NA REASON.
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Jamaa ana wivu wa kijinga tu,kama ulishamwacha wa nini kumbughudhi?Naamin akikaa nae mbali, kama mkoa mwingine itakuwa ahueni kwake.Kama anaroga wanae ni kigagula mzoefu sana.
   
 13. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani..hali hiyo hapo juu inawapata pia wale ambao imani/dini zao zinaruhusu kuoana na kupeana talaka? Au wale walio na ndoa za wake wengi kufuatana na dini au mila zao?

  Ninauliza haya ili kujua hasa tatizo liko wapi.
   
 14. A

  Aine JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ee Mungu tusasidie. Mwambie huyo dada kwanza afunge na kuomba na asome YEREMIA 33.3, 32.26-27, aidha atafute mchungaji amueleze ili amsaidie kwa maombi. Ila kama anakaa karibu na huyo mwanaume ajaribu kuhama na akae sehemu ambayo hataijua huku akimuomba Mungu amsaidie. Huyo mwanaume ana mapepo si bure, pole yake sana
   
 15. T

  Tall JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  mkuu hakikisha jambo baya na ovu halitokei kati yao,na Mungu atakuongoza na kukusaidia.
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye Nyekundu ndo wasi wasi wa hii story ulipo! Unaweza kweli thibitisha huo uchawi na majini?
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,416
  Trophy Points: 280
  ghoulish
   
 18. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,280
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Na ilikuwaje mwanaume mkorofi hivyo amruhusu huyo dada aondoke na watoto? Mimi nijuavyo sheria ya Tz mama hana mamlaka na watoto kwa hiyo ninge expect huyo jamaa ang'ang'anie watoto kama njia ya kumrudisha wife. Imekuwaje kamruhusu aondoke na watoto? I am trying to think what kind of a man he is. Kwa experience yangu wanaume makatili kama yeye chakwanza anachofanya ni kukunyang'anya watoto; sasa hapa naona different story!
   
 19. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Mie namshauri atimize nia yake. Ubaya hulipwa kwa ubaya
   
 20. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  He wewe umtakii mema huyu dada si atafia jera kama si kunyongwa!
   
Loading...