siongelei kuhalalisha ila naongelea swala la mtoto kumfikiria mama yake na kumsamehe, kuna watu najua wamezaa na miaka 13, yaani mama ni mtoto kiakili, kimwili, kifikira. Ninaongelea special case mkuu. Ukisoma hiyo post yangu taratibu.
Kumsamehe ni kumwachilia mtu, ni kuachilia zile fikira alizokuletea zenye uchungu, chuki, na maumivu. Kuachilia mawazo ya kisasi kama nitamkomoa, sitaongea naye, sitacheka akiongea all the negative thoughts. Kusamehe sio kitu cha siku moja ni process, unaanza taratibu taratibu na unadhamiria kuwa nimemsamehe na baada ya muda utajikuta huko huru. Kusamehe haimanishi kuwa ndio tumekuwa marafiki ina maanisha kuwa nikikufikiria siumii tena, sifikirii kisasi ila nafikiria mazuri juu yako.Unaposema kumsamehe unakuwa unamaanisha nini?
Pongezi za dhati kwe nu wamam wote ambao mmetimiza majukumu yenu stahiki kwa viumbe mlivyovileta duniani kwa kutaka na kupanga wakatio havipo
Mbarikiwe nyote.
Do you think i'm a fool?
Na baba je?
Hakuna jambo lolote ambalo litahalalisha mama kumtelekeza mwanae!
Kumsamehe ni kumwachilia mtu, ni kuachilia zile fikira alizokuletea zenye uchungu, chuki, na maumivu. Kuachilia mawazo ya kisasi kama nitamkomoa, sitaongea naye, sitacheka akiongea all the negative thoughts. Kusamehe sio kitu cha siku moja ni process, unaanza taratibu taratibu na unadhamiria kuwa nimemsamehe na baada ya muda utajikuta huko huru. Kusamehe haimanishi kuwa ndio tumekuwa marafiki ina maanisha kuwa nikikufikiria siumii tena, sifikirii kisasi ila nafikiria mazuri juu yako.
Note: Hakuna mtu anayeweza kukupenda kama wewe unavyojipenda, jipende, kutokusamehe ni kujitesa mwenyewe.
Kuna mambo ambayo yanamfanya mama akatae na hata achukie watoto wake wengine mpk wanaua lakini wote hawa ni wagonjwa wa akili na kuna reason behind! Usiwahukumu ni kuwasaidia!
You are not a fool and never will u be. Kama nimekukwaza niwie radhi rafiki. I didnt mean to offend you. Sikujua kama comment yangu yaweza kukuudhi. Nisamehe tu bure rafk.
loh! Nina sifa zoooote za mama ulizotaja isipokuwa kwenye vigezo vya pongezi. Mimi mwanangu sikupanga kumleta wakati hayupo ila alipokuja nilishukuru na kumuandalia makao duniani na ninampenda sana.
Pole sana mkuu ,ila mzazi ni mzazi....piga moyo konde na hisia za upendo.
Mama yangu nampenda sana ,amenipigania daima mpaka leo hii naweza kusimama kama mwanaume wa kweli.
Huyu Mama huyu alinipigania kwenye shida na raha ,aisee sina cha kulipa zaidi ya kusema nashukuru kwa yote mama yangu.
Nakupenda sana.
Huwa naogopa sana kuhukumu. Ebu jaribu kuaangalia huyu mama kwa nini alifanya hivyo; mambo ya kukurupuka tu kulaumu na kuhukumu nahisi kama siyo sahihi. Mleta thread ametaja sifa za huyo mama anayemsema, tumfuate