I miss you mom

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920

Nakukumbuka sana mama yangu.

Simzunguzii yule mama ambae alichindwa kujua jukumu lake abaada ya kuzaa na kulea kwa miaka michache kisha akamtelekeza mwanae

Namzungumzia yule mama ambae nasikia watu wakimsema kuwa hawezi kulala mwanae akiwa hajalala
Namzungumzia yule mama ambae watu wanasema mwanae akiwa anaumwa anakosa kabisa amani
Namzungumzia yule mama ambae watu wanasema mwanae akishindwa kwenda shuleni kwasababu ya hali ngumu anakosa amani
Namzungumzia yule mama ambae watu wanamsema mwanae akilia usiku nae anakesha

Mama huyu ambae sifa zake hapo juu nimeweka baadhi ndie ninaemkumbuka na nahisi namkosa sana na namhitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote ule.

Mama nimekukumbuka sana na nasikitika sijapata kukuona kabisa kwenye maisha yangu,niliyemuona ni yule ambae hata sifa hata moja hapo hana,niliishia kubebwa kwenye tumbo lake tu na kisha kuletwa duniani ambako nilikuwa mgeni na yeye ambae alikuwa mwenyeji hakunisaidia kuijua dunia hii.

Uchungu pekee alioupata yeye ni ule wa kunizaa tu lakini zaidi ya hapo hakuna.

Naendelea kukutafuta wewe iliestahili kuwa mama yangu ili nami nione sifa kukuita mama,uko wapi?
Natamani nikuone nami nikupe mapenzi ya dhati ambayo natamani kuyatoa kwako.

Nitaendelea kukutafuta milele

Pongezi za dhati kwe nu wamam wote ambao mmetimiza majukumu yenu stahiki kwa viumbe mlivyovileta duniani kwa kutaka na kupanga wakatio havipo

Mbarikiwe nyote.
 
pia usisahau mababa wote
ukakosa baraka za baba maana wao ndio wanabariki

mababa wote stand up!!!!!!!!

Hakika usemayo. Naishi katika baraka za baba angu. Alinitamkia baraka na mpka sasa kile alichokitamka kimetimia ktk maisha yangu. Baraka ya baba ni kubwa mno. R.I.P baba yangu.
 

Ukifanikiwa kumpata mama yako msamehe tu. Nina rafiki yangu yy mama yao aliwaacha wakiwa wadogo baada ya baba yao kufariki na kwenda kuolewa na mwanamume mwingne. Kwa bahati nzuri huyu rafk yangu alichukuliwa na baba ake mdogo akalelewa na kusomeshwa. Na kwa kipindi chote hakuwahi kukutana na mama ake kabisa. Amekuja kukutana na mama ake akiwa tayari ana degree yake. Huwez amini yule mama ndo anamuona wa maana mtoto wake sa hz kwa kuwa ana mshiko. Kaza moyo kijana Mungu atakusaidia. Ila mama asiyelea mwanae huwa nashindwa kumwelewa kabisa.
 
Ila mama asiyelea mwanae huwa nashindwa kumwelewa kabisa.
Vya kuzingatia cha kwanza umri wa huyo mama kama alikuwa mtoto mdogo labda hakuwa amekomaa kuelewa, pili mazingira ya nyumbani baada ya yeye kupata mimba wengine wanapitia trauma za ajabu. Sisapoti wanaokimbia watoto, ila ninajua mama mwenye akili timamu hawezi kukimbia mtoto. Ni vizuri kupata taarifa kutoka pande zote mbili kabla hujaconclude.
 

Hakuna jambo lolote ambalo litahalalisha mama kumtelekeza mwanae!
 

Do you think i'm a fool?
 
Hakuna jambo lolote ambalo litahalalisha mama kumtelekeza mwanae!

siongelei kuhalalisha ila naongelea swala la mtoto kumfikiria mama yake na kumsamehe, kuna watu najua wamezaa na miaka 13, yaani mama ni mtoto kiakili, kimwili, kifikira. Ninaongelea special case mkuu. Ukisoma hiyo post yangu taratibu.
 

Na baba je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…