I got to say it; watawala wana matatizo kichwani!?

nguvumali (old or new?), kwani kazi ya pingu ni nini hadi mtu aulizie mahakamani? Kweli tunahitaji mahakama kuuliza kazi ya pingu ni nini?
unajua namna ambavyo Kova anataka jamii iamini ni kua Muro ni sehemu ya kundi la wahalifu ambae anatumia Pingu katika matendo yakutishia watu, na ndio maana siku ya pili akaibuka na wadau fulani hivi akiwahusisha na matukio kadhaa ya kitapeli hapa mjini, na akahitimisha kwa kusema kua wale jamaa ukiwapa dhamana wanaweza kuitapeli hata dhamana yenyewe.....
ninachotaka kusema ni kua kama atathubutu kumpeleka Muro mahakamani anaweza akafile swala la kukutwa na Pingu kama dhana yakutishia raia ili apate kitu kidogo , sasa silazima kumuhoji lakini kama moja ya vithibitisho vya Jerry kuhusika na aina hiyo ya Uhalifu hakuna namna ila ni kumuhoji kwanini anamiliki hiyo PINGU, na hapo ndipo hoja yangu imelalia.
 
bingo!!!!!!!!!!! I like you Kimweri.. ndio maana nimesema kwenye ule ukurasa mwingine hakuna jaji wala mahakama inayoweza kumfunga Muro kwa "kosa" la kukutwa na pingu ambazo zilikuwa ndani ya gari (wapi???)! Vinginevyo, itafungua mlango wa watu kufungwa wakikutwa na kamba, mnyororo n.k!

..... unajua ukikutwa na gudulia la plastic kwenye gari unaweza kushtakiwa kwa kutembea na kifaa cha kuwezesha usambazaji wa pombe haramu ya gongo!!!! lol
 
Hili ni suala dogo sana kushughulikiwa kisheria kwani utaratibu uko wazi ila kutokana na upeo mdogo na ushabiki hasa wa taasisi kama jeshi la polisi yote haya yanatokea na kuudhiii...

Ninaamini chanzo cha umasikini wetu ni ukosefu wa watu makini katika nafasi za uongozi hasa upeo wa kuchambua na kuona mbele wala sio mbali..

Tutaliia rasilimali tulizonazo lakini ukosefu wa rasilimali watu katika kutumikia umma ni KIKWAZOOO KIKUBWAA..Hatuhitaji madini, mafuta wala ardhi yenye rutuba, TWAHITAJI RASILIMALI WATU.
 
hili swala naamini likifikishwa mahakamani kuna mengi yaliofichika yatakua wazi, upo upande utaumbuka na utatafuta pakufichia sura zao. nasema haya kwa maana kuna mtafaruku katika kila hatua, hali ambayo inamuacha mtanzania wakawaida asiwe na maoni binafsi yaliyo huru....bado natamani kumuona Jerry Muro akiulizwa swali la matumizi ya pingu yake mahakamani .... maana Kova ameshindwa kumuhoji hilo swali kama Jerry mwenyewe alivyonukuliwa.
sasa baaada ya sakata hili na UMMA kueleweshwa juu ya matumizi ya PINGU bila shaka duka linalouza pingu lijiandae kupokea maombi mengi ya kuhitaji bidhaa hiyo.

hata mimi nilijiuliza sana kwa nini Muro anamiliki pingu, labda anafungia ng'ombe utajuaje? lakini kuna jamaa amesema mwanzoni kuwa kuwa kuna watu wanazitumia kwenye mapenzi! LOL! inawezekana Kova analijua hili na ndiyo maana hajamuuliza Muro. aha ahaaaa!

that bring to another question
Muro amejifunzia wapi, kwa hao hao polisi au kwenye movies? maana isije matumizi ya pingu kwenye mapenzi ni kitu cha kwaida kwa polisi kwa sababu wanazimiliki! na ikipitishwa search unaweza kukuta wengi wanamiliki hizi pingu for the same purpose!!

Hilo duka wamemuuzia pingu Muro tu au? haiwezekani wakaleta stock ya pingu moja jamani ebu fungueni macho !!!!!

makubwa!!
 
Mkjj, unasahau kwamba serikali yetu inapinga shughuli za ukahaba??... hatuchelewi kukuta kwamba sababu kubwa zinazowapelekea 'watawala' wetu kupinga manunuzi ya pingu hizo ni matumizi yake yasiyotarajiwa kwenye mambo ya ukahaba. Wamegundua hivi karibuni ununuzi wa pingu umeshamiri na uchunguzi wao umewajuza kuwa pingu hizi zinatumika kwenye S & M (ngono machachari), jambo ambalo ni kinyume na sheria zetu.

Nauliza wanajanvi, toka lini jinsi ya kufanya ngono kukasimamiwa na sheria na sheria hiyo ni ipi?
 
HUYU KOVA KASEMA PINGU NI ILLEGAL,swali la msingi MTU AKIKUTWA NA GONGO(which is deemed illegal) huwa anaulizwa risiti ya kununulia gongo hiyo?au huwa anakamatwa kwa kumiliki,kunywa gongo?

Duh! kweli JF kiboko Risiti ya kununulia gongo!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hili ni suala dogo sana kushughulikiwa kisheria kwani utaratibu uko wazi ila kutokana na upeo mdogo na ushabiki hasa wa taasisi kama jeshi la polisi yote haya yanatokea na kuudhiii...

Ninaamini chanzo cha umasikini wetu ni ukosefu wa watu makini katika nafasi za uongozi hasa upeo wa kuchambua na kuona mbele wala sio mbali..

Tutaliia rasilimali tulizonazo lakini ukosefu wa rasilimali watu katika kutumikia umma ni KIKWAZOOO KIKUBWAA..Hatuhitaji madini, mafuta wala ardhi yenye rutuba, TWAHITAJI RASILIMALI WATU.

Rasilimali watu sio bidhaa adimu nchini mwetu; kwani wengi wao wako DIASPORA kwasababu hawathaminiwi na watawala wetu!! Watawala wetu wanathamini zaidi PATRONAGE[ uanamtandao] kuliko MERIT [PROFESSIONALISM] ya watu na ndio maana kuna artificial lack of RASILIMALI WATU nchini!!
 
Hivi hawa viongozi wetu wanashindwa nini kabla ya kuongea kuhakikisha kuwa wemepima wanachoongea? Ngumu kweli kwa sasa kujua kuwa mtu amekosea kwa makusudi au hajui aongeacho

wanatapatapa kama wafa maji, na chakusikitisha bado hawataki jujifunza kutokana na madudu ya muheshimiwa kamanda K....KUKURUPUKA!!!

kweli as MMK says wanaweza kuwa wagonjwa upstairs!!! maana haiwezekani baada ya kamosa yote waloonesha kwenye hili sakata bado wanashindwa wa-atack from which angle!!!

something is just too wrong somewhere!!!!!!!
 
Nilalapo usingizi wa mangamungamu napata majinamizi juu yako weee!
Niamkaponi ni uchungu kwangu mama wa kambo weeee!

kweli tunahitaji kuedit mashairi ya wimbo huu, we have had enough ahhhhhhhhhh!!
 
Sisemi kwa maana ya kuwatukana lakini kutokana na uzoefu wangu katika mambo ya afya ya akili (mental health) naweza kusema pasipo shaka kabisa kuwa kuna watu wanahitaji kupimwa na kupatiwa matibabu ya haraka kwani wana matatizo katika uwezo wao wa kutumia chembechembe za ubongo kufikiri na kujenga hoja.
.
Mzee Mwanakijiji, hili mbona liko wazi tuu, tena sio tuu watawala wetu, bali miongoni mwetu sisi wana JF, kuna watu wanahitaji kupimwa na kupatiwa matibabu ya haraka kwani wana matatizo katika uwezo wao wa kutumia chembechembe za ubongo kufikiri na kujenga hoja.

Kwa watawala wetu, tuna haki ya kuwajadili public na private, kwa sababu, tunawalipa mishahara yao kwa kodi zetu, hivyo ni haki yetu kuhoji kila kitu kuhusu wao.

Ndio maana tunasisitiza, wale wenye uwezo, usiotia shaka, waje na hoja zao, wawaeleze Watanzania, watawaelewa na kuvote on board, vinginevyo tutaendelea kutawaliwa ha hawa hawa na maroroso yao.
 
HUYU KOVA KASEMA PINGU NI ILLEGAL,swali la msingi MTU AKIKUTWA NA GONGO(which is deemed illegal) huwa anaulizwa risiti ya kununulia gongo hiyo?au huwa anakamatwa kwa kumiliki,kunywa gongo?
Nother greater thinker!! - - - mental health again man, should we wonder who "rules" this country?
 
Wote hao wajeshi tuuuu! Hawapimi sentensi zao kabla hawajasema. Anaongea na umma kama vile anaongea na wanajeshi (Yes Sir)?
 
Hilo duka wamemuuzia pingu Muro tu au? haiwezekani wakaleta stock ya pingu moja jamani ebu fungueni macho !!!!!

!!
macho nimefunguka Waberoya, naninaamini sakata la muro litaibua mengi mazuri aidha kisheria ama kijamii, maaana nimeanza kujua matumizi mwanana wa pingu katika mahaba, hii imenipa hamasa ya mimi kuitafuta ili nikidhi haja....
nataraji jambo moja rate ya wanunuaji wa bidhaa hiyo itaongezeka.
 
kinachonishangaza Nyambala ni kuwa wanakasirishwa sana na kukutwa pingu ndani ya gari kuliko bunduki!! NIlikuwa najiuliza mara ya mwisho kusikia majambazi yamevamia mitaa na pingu au wamepora benki kwa kutumia pingu ilikuwa lini?

Mkjj,

Hiyo bold hapa bongo siku hizi wanaita ni changamoto.

Juzi liliokotwa BOMU mitaa ya Mikocheni (122mm) lakini Kamanda Kova wala Msemaji wa jeshi sikuwasikia wakiongelea hilo...!
 
unajua namna ambavyo Kova anataka jamii iamini ni kua Muro ni sehemu ya kundi la wahalifu ambae anatumia Pingu katika matendo yakutishia watu, na ndio maana siku ya pili akaibuka na wadau fulani hivi akiwahusisha na matukio kadhaa ya kitapeli hapa mjini, na akahitimisha kwa kusema kua wale jamaa ukiwapa dhamana wanaweza kuitapeli hata dhamana yenyewe.....
ninachotaka kusema ni kua kama atathubutu kumpeleka Muro mahakamani anaweza akafile swala la kukutwa na Pingu kama dhana yakutishia raia ili apate kitu kidogo , sasa silazima kumuhoji lakini kama moja ya vithibitisho vya Jerry kuhusika na aina hiyo ya Uhalifu hakuna namna ila ni kumuhoji kwanini anamiliki hiyo PINGU, na hapo ndipo hoja yangu imelalia.

Nguvumali.. hivi Muro akisema Pingu hiyo alikuwa anataka kuitumia incase gari lake linaharibika ili aiunganishe na mnyororo kuweza kuvuta gari hilo utamkatalia?
 
hilo ndio jibu murua nililikuwa nataka kuliweka ile pingu Muro anamajibu mengi zaidi ya maswali kwa nini anayo .
ingekuwa ni mimi ningejibu kama ifuatavyo
1. nilinunua ili nijua pingu ikoje na inafanyaje kazi.
2. kutokana na wizi wa magari kukisiri hapa mjini hasa katika kanda hii unayo iongoza mara nyingi nikiwa bar fulani naamua kulifunga kwa pingu
3.
 
This is only the tip of the iceberg I am afraid.

Sheria zetu za ajabu nyingine hazijabadilishwa tangu zikokotolewe na muingereza kutoka India 1948.

Mkuu heshima mbele hapo usiwalaumu Waingereza kwani ni sis wenyewe na bunge letu lilipitisha huo mswaada kwa mafisadi kujilinda incase tukiona enough is enough
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom