I got to say it; watawala wana matatizo kichwani!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I got to say it; watawala wana matatizo kichwani!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 5, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Sisemi kwa maana ya kuwatukana lakini kutokana na uzoefu wangu katika mambo ya afya ya akili (mental health) naweza kusema pasipo shaka kabisa kuwa kuna watu wanahitaji kupimwa na kupatiwa matibabu ya haraka kwani wana matatizo katika uwezo wao wa kutumia chembechembe za ubongo kufikiri na kujenga hoja.

  Soma sehemu hii ya habari iliyoko kwenye gazeti la mwananchi kuhusu mambo ya Muro:

  wengi wamekuwa wakihoji mtu kukutwa na pingu ati ni raia; na sasa duka linasema wanashangaa inakuwaje raia kuuziwa pingu! Sikutaka kusema lakini sina budi kusema.

  HIVI NI KIPI KIGUMU ENYI watawala WETU?! Kumuuzia raia bunduki na risasi za moto au kumuuzia pingu? Kama mmepitisha sheria inayokubali raia kununua bunduki na risasi kwenye duka la serikali inakuwaje jambo la kushangaza kununua pingu KWENYE duka hilo hilo?

  Yaani mnachofanya ni sawasawa mnashangaa imekuwaje mtu kanunua baskeli wakati yeye ni raia ilhali duka lenu linauza magari!? Kama raia anaweza kununua gari kusafiria na akakuta mnauza, piki piki na baskeli, akiamua kununua gari na baskeli ni kipi kinaweza kudhuru zaidi barabarani!?
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  This is only the tip of the iceberg I am afraid.

  Sheria zetu za ajabu nyingine hazijabadilishwa tangu zikokotolewe na muingereza kutoka India 1948.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mkjj, unasahau kwamba serikali yetu inapinga shughuli za ukahaba??... hatuchelewi kukuta kwamba sababu kubwa zinazowapelekea 'watawala' wetu kupinga manunuzi ya pingu hizo ni matumizi yake yasiyotarajiwa kwenye mambo ya ukahaba. Wamegundua hivi karibuni ununuzi wa pingu umeshamiri na uchunguzi wao umewajuza kuwa pingu hizi zinatumika kwenye S & M (ngono machachari), jambo ambalo ni kinyume na sheria zetu.
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Jamani mimi sijapata jibu. Hii kesi inasikilizwa kwenye vyombo vya habari? Hakimu ni nani? Mawakili Je?
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 38,087
  Likes Received: 9,747
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kama mtu unajiexpress kama "Californication" na mkeo nao pia ni ukahaba?

  Au bongo tuna Cultural police kama Saudi Arabia na Iran?
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sasa na hilo duka kwa nini linauza bidhaa ambazo raia hawaruhusiwi kumiliki. Si wangehifadhi warehauzi kama ni kwa matumizi ya taasisi maalumu??????
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Taanzania Tanzaniaaa nilukupenda nchi yangu!!!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Feb 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280

  kinachonishangaza Nyambala ni kuwa wanakasirishwa sana na kukutwa pingu ndani ya gari kuliko bunduki!! NIlikuwa najiuliza mara ya mwisho kusikia majambazi yamevamia mitaa na pingu au wamepora benki kwa kutumia pingu ilikuwa lini?
   
 9. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ...Hii ni kali......Imebidi nicheke sana...You have made my morning!
   
 10. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi hawa viongozi wetu wanashindwa nini kabla ya kuongea kuhakikisha kuwa wemepima wanachoongea? Ngumu kweli kwa sasa kujua kuwa mtu amekosea kwa makusudi au hajui aongeacho
   
 11. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #11
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  hili swala naamini likifikishwa mahakamani kuna mengi yaliofichika yatakua wazi, upo upande utaumbuka na utatafuta pakufichia sura zao. nasema haya kwa maana kuna mtafaruku katika kila hatua, hali ambayo inamuacha mtanzania wakawaida asiwe na maoni binafsi yaliyo huru....bado natamani kumuona Jerry Muro akiulizwa swali la matumizi ya pingu yake mahakamani .... maana Kova ameshindwa kumuhoji hilo swali kama Jerry mwenyewe alivyonukuliwa.
  sasa baaada ya sakata hili na UMMA kueleweshwa juu ya matumizi ya PINGU bila shaka duka linalouza pingu lijiandae kupokea maombi mengi ya kuhitaji bidhaa hiyo.
   
 12. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #12
  Feb 5, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
  HUYU KOVA KASEMA PINGU NI ILLEGAL,swali la msingi MTU AKIKUTWA NA GONGO(which is deemed illegal) huwa anaulizwa risiti ya kununulia gongo hiyo?au huwa anakamatwa kwa kumiliki,kunywa gongo?
   
 13. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2010
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,095
  Trophy Points: 280
  Unless it is ILLEGAL,matumizi ya Pingu ni Private matter ya mhusika.Walichotakiwa kufanya Polisi ni kumkamata akiitumia red-handed katika matumizi ambayo ni kinyme cha sheria.
   
 14. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #14
  Feb 5, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani hawa jamaa wala hawapingi wala kukataza watu kumiliki Pingu ila tu kwasababu wana agenda zao kwa Muro ndo maana wanajifanya leo wanashangaa kuona raia wa kawaida akimiliki Pingu wakati huo huo ni wao wenyewe wameruhusu uuzwaji wake na mimi sidhani kama Muro ni mtu wa kwanza kukutwa na pingu mpaka kwake iwe skendo....naamini kabisa Kova na wenzake katika harakati zao za kukuamata wahalifu wameshawahi kukuta Pingu lakini hawakuwahi kuripoti,tumekuwa tukisikia tu,tumekamata risasi na bunduki kadhaa walikuwa haripoti pingu kwasababu it was not a big deal kwanini leo iwe kwa Muro?
   
 15. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,251
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 160
  Duuuuuuuuuuhhhhhhhhh! mkuu hii ni kali kuliko!1 haaaaa heeeeeeeee kwekwekweeeeeeeeeeeeee.
  Ntafukuzwa kazi kwa kicheko.
   
 16. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Unajua huyo kamanda wa polisi alichofanya ni kujaribu kucheza na minds za watanzania. Ajenda ikiwa ni rushwa, well attempted rushwa.......... Ikaingizwa bunduki na pingu to justfy maelezo ya mtu aliyedai kuombwa rushwa. Sasa Imekuja kuonekana ishu haina mashiko baada ya kutenganisha hizo items:

  1. Rushwa - Tunaambiwa CCTV imekamata. Lakini kwa mtu wa stahiki ya Kova angekuwa amesharusha hiyo clip hewani. And he would be one of the most genious cop kusubstantiate ushahidi kisheria kutoka kwenye the alleged CCTV videos.

  2. Bunduki - Inamilikiwa kihalali

  3. Pingu - Hapa naona Kova ndio aliamua kukandamizia huku akisahau ubatili au uhalali ulitakiwa uthibitishwe kisheria. Sasa kwa sababu, nadhani ni audience aliyoizoea akakurupuka kutamka kwamba hakuna raia anaruhusiwa kuwa na pingu. Na kama eti ni halali aje na risiti...........

  Sasa na hawa wengine inaonekana hawajaelewa kwamba polisi wameshafanya fu..up ya namna walivyohandle the whole ishu. Nao wanaanza kwa mtindo ule ule wa kushangaa.......... I would have thought kwa watu smart kama JWTZ wangefanya uchunguzi kwanza kabla ya kuanza kushangaa.

  Well nadhani ni staili ya serikali siku hizi kushangazwa, kushtushwa etc.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  nguvumali (old or new?), kwani kazi ya pingu ni nini hadi mtu aulizie mahakamani? Kweli tunahitaji mahakama kuuliza kazi ya pingu ni nini?
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Yuko jamaa yangu mmoja anafanya kazi kwenye nyumba ya mapadre. Alikuta kondomu kwenye moja ya mifuko ya suruale ya Padre. Akashtuka. Akaja kunisimulia. Nikamuuliza kondomu hiyo ilikuwa imeonyesha kutumika? Akaniambia hapana. ilikuwa imefungwa vizuri tu ndani ya kifuko chake. Nikwamwambia Padre wetu Mkatoliki hana kosa. Huenda alikuwa anaitumia kuonya wanaozitumia wakidhani ni kinga ya ukimwi!
  Huenda na Muro alikuwa akizitumia pingu kuwaonya wala rushwa.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Feb 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  bingo!!!!!!!!!!! I like you Kimweri.. ndio maana nimesema kwenye ule ukurasa mwingine hakuna jaji wala mahakama inayoweza kumfunga Muro kwa "kosa" la kukutwa na pingu ambazo zilikuwa ndani ya gari (wapi???)! Vinginevyo, itafungua mlango wa watu kufungwa wakikutwa na kamba, mnyororo n.k!
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tena afadhali piongu maana kamba hutumika kunyongea!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...