I am too Rich to get married

anaweza akawa na point upande mwingine..

ingekuwa kuna mtu alikuwa anakupenda toka enz ya msoto yupo free. huyo unaweza oa... ila hawa wa kukutana nao umeshatoboa.. hawa ni wa kwenda nao kwa umakini...

babu sambeke hakuoa hadi anafariki, ruge mutahaba mpaka kesho hajaoa... na wengine wengi tu
 
Hakuna haja ya kuoa unapokuwa unamiliki mkwanja wa kutosha, ya nini kujisogezea stress ambazo kimsingi unaweza ziepuka? Naungana na huyo bilionea asiyejulikana.
Buhahaha bilionea asie julikana
 
Floyd Mayweather ana akili kuliko Barack Obama??
Mbona unatolea mfano wa watu wasio kuhusu..mi nimesema ukiona MTU anapesa nyingi kuliko wewe maana yake ni kwamba ana akili nyingi kuliko wewe..Jitafakari wewe na maisha yako .na uchukulie kama challenge katika maisha yako.Dont bring Obama and May weather here..We are not talking about them
 
yupo sahihi kwa upande wake na fikra zake.
 
Hizo ni kauli za kichochezi na huo ni uchochezi wa kijinsia. Sikubaliani na huyo tajiri uchwara kwa namna yoyote ile. Utajiri au umaskini siyo excuse ya kutooa, wapo matajiri ambao wameingia kwenye listi ya matajiri kumi bora duniani ya FORBES na wote wameona. Huyo mvulana wa mkoani atakua ana matatizo ya kijinsia na anaogopa siri zake zisije zikawekwa hadharani. Kuoa ni ibada, kuoa ni kutengeneza mazingira ambayo watoto watalelewa vizuri kwa uangalizi wa watu wawili na hilo ndilo kusudio la Mungu kwa kuanzisha familia. Mali tunazokusanya hapa duniani mwisho wake ni kaburini, huyo tajiri uchwara akifa hawezi kuzikwa na mali zake ataenda kaburini kama alivyozaliwa. Kwangu mimi naona amekua mchoyo wa kutumia mali zake na mwanamke. Akiuzoea huo utajiri atabadilika.
 
Ha ha naona umekubali ulichokisema hakina mantiki. Siishi kwenye box naishi maisha yako wazi naangalia zaidi ya upeo wa macho yangu kwahio siwezi kuacha kuangalia watu kama Floyd,Obama,Carson etc.
 
Anasema mawazo yenye hekima na busara kama haya hutoka kwa watu masikini wasio na kitu.Lakini kwa yeye tajiri hawezi kuwa na mawazo kama yako..Anasema mawazo ya tajiri hayawezi kukaa kwenye kichwa cha masikini and vice versa.. Akatuambia hata " mkipataga pesa huwa mnaspend like u don't mean nothing ila zikiisha ndo akili zinakuja..I think he is right
 
Ha ha naona umekubali ulichokisema hakina mantiki. Siishi kwenye box naishi maisha yako wazi naangalia zaidi ya upeo wa macho yangu kwahio siwezi kuacha kuangalia watu kama Floyd,Obama,Carson etc.
Jiangalie wewe na watu wanao kuzunguka..Hatuwezi kuwazungumzia Obama na May weather kwa sababu hatujui wala hatuna uhakika Nani ana pesa nyingi kumshinda mwenzake
 
Na wewe ulimsupport kwasababu yeye ndio alikua mnunua vinywaji?
 
Mungu akusamehe kwa majaribu uliyowapa wanawake wapenda pesa. Si ungeweka namba yake bro

Akiweka namba za simu masikini watamsumbua Madam Mwajuma , Na yeye inaonesha hataki kufungamana na jamii ya watu masikini kama sisi.

Ahahhhahahahaaaa

Mimi nadhani hiyo sio sababu ya yeye kutokuoa, hiyo imekuwa kama sehemu ya kuficha mapungufu yake, hasa ukizingatia tumeambiwa watoto alionao aliwapata zamani kabla ya kuwa tajiri. Usikute ni utajiri wa masharti, labda haruhusiwi kuwa na familia nk.

Mtoa mada kwa niaba ya tajiri asiyejulikana LIKUD hujatuambia kuhusu watoto wa tajiri walipo kwa maana wanaishi wapi na wanalelewa na nani.
 
Kwanza nikuweke wazi huyo siyo tajiri ni mtu aliyepata nafuu tu kwenye maisha. Huyo ni mtu ambaye hana misingi ya utajiri na matajiri hawaongei na kufikiria kwa namna hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…