Habari gani wakuu? Natumai wote mu wazima. I ain't yo mama ndio kichwa cha uzi huu hapa.
Ni hivi nimekua na mahisiano ya kimapenzi na mdada mmoja hivi kwa zaidi ya mwaka na mambo yamekua yakienda fresh hamna mbaya lakini hivi majuzi niliamua kukatisha mapenzi hayo kwa sababu ya wimbo wa i ain't yo mama, kisa ni hivi
Week tatu zilizopita tuliamua kutoka out na huyo aliyekua mupenzi wanguu tulienda disco ama club. Watu walicheza sana koz dj alikua vizuri sana kila nyimbo aliyotupia watu kelele weweeeeeeeeeee, ila sisi hatukua tunacheza bali tulikua tunakunywa mvinyo tuu na kuangalia watu wanavoamsha kwenye dansi floo koz sisi sio wachezaji wazuri wa muziki ila tunapenda muziki. Cha kushangaza ni pale dj alipocheza wimbo wa i ain't yo mama huu wimbo nauona unachezwa mara kwa mara kwenye chanel ya Trace urban ila sijui aliyeimba ni nani. Wimbo huu ulipoanza tuu mpenzi wangu aliruka kwenye kiti moja kwa moja akicheza kuelekea kwenye dansi floo huku akiuimba wote sijui ni lini ameukariri. Niliwaza kidogo kwanini kaenda kucheza huu wimbo na sio mwingine? Nikasema isiwe kesi may be ni mvinyo imeingia kichwani, alicheza akifurahia sana huku akinyoosha vidole na wimbo ukawa unafika ukingoja akarejea kwenye kiti huku akiendelea kuimba wimbo huo huo.
Tuliondoka na kurejea nyumba ila nikiwa na kitu kichwani kama nawaza ila sijui nawaza nini. Kesho yake tuliagana akarudi kwake na mimi nikaendela na mambo yangu.
Sasa weekend hii alikuja hom akapika tukala mambo yakawa yanaenda fresh. Nikakumbuka natakiwa kumtumia ndugu yangu flani hivi document alikua anaziihitaji tangu asubuhi. Chaa ajabu nilivomwambia mpenzi wangu huyo akaniletee vocha ya halotei aliguna then akawa anaondokaa kwenda dukani huku akiimba I AIN'T YO MAMA. Hasira zilinijaa sana nikaamua kumtolea kila kilicho chake na kumwekea mlangoni nikafunga mlango nikatokea uwani kwa ufipi penzi lilishia hapo japo nilipata taarifa alilia sana. Ataenda kuhadithia wenzake.