Huzuni/furaha tunazitengeneza sisi katika haya maisha, kila unachodhani kitakupa furaha kipo neutral + SULUHISHO LAKE

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
11,169
15,851
Kama kweli furaha inatokana na kitu fulani ambacho unakihitaji jee kwa nini baada ya kupata kitu hiko bado kuna vitu vingine vitakukosesha furaha na kukutia stress ?

Yaani utajikuta umepata mtoto tayari,lakini kodi ya nyumba inakunyima raha

,je ni ipi faida ya furaha ya mtoto kama furaha hiyo haiwezi kuondoa hata huzuni ya kudaiwa kodi ya nyumba ?

Ni ipi faida ya furaha ya kuwa na gari kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kazi nyingi ofisini ?

Ni ipi faida ya kuwa na furaha ya kupata nyumba kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kipato kidogo ?

katika haya maisha hicho unachodhani ukikipata kitakupa furaha sio kweli.

FURAHA YA KWELI NI ILE AMBAYO INAKUONDOLEA HUZUNI UNAYOIPATA KATIKA VITU VINGINE.

furaha unayo mwenyewe na wala haipo kwenye vitu unavyovihitaji Kama vile watoto,pesa,nyumba n.k.

Unaweza kutamani gari,ukalinunua na siku za mwanzo ukawa na furaha sana na upya wake.

lakini masiku yakikatika unaliona gari la kawaida hivyo halikupi tena furaha kama ile ya mwanzo,imeenda wapi furaha ile ?

vitu ambavyo tunategemea vitatupa furaha tukishavimiliki tu baada ya masiku kadhaa tunaviona vya kawaida na havitupi tena furaha.

Nilitamani sana kuoa na siku ya kuoa nilikuwa na furaha sana,lakini leo hii sijui furaha ile imeenda wapi na ndoa bado ninayo.

Nilitamani kuwa na mtoto,nilipopata mtoto nilikuwa na furaha sana.

leo mtoto ninaye lakini sijui ile furaha ya mwanzo ya kuwa na mtoto siioni tena na mtoto bado yupo.

Hakuna kitu chochote ambacho ni chanzo cha furaha kwenye maisha yetu isipokuwa sisi wenyewe.

SULUHISHO.

FURAHA TUNATAKIWA KUZITENGENEZA KAMA AMBAVYO TUNATENGENEZA CHAKULA,MAGARI AU NYUMBA.

KUITENGENEZA FURAHA.

furaha tunaitengeneza kwa KUSHUKURU na kutafakari faida ya kitu hicho.

Utakapotafakari faida unazopata kwa kitu fulani na kushukuru basi hapo ndipo furaha utaiona.

Ukiamka asubuhi unaenda kazini kwa daladala sawa hauna gari jee umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa daladala kwako na ukasema asante Mungu..?

Umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa macho yako kwa namna unavyotumia na ukasema asante ?

Je miguu,masikio,pua,mdomo umeshawahi kutakarai kwa ucahche umuhimu wa hivyo vitu kwako kwa namna unavyovitumia ?

Bila kuwa na utaratibu huo utajikuta unaamka kila siku uko bored,hauna mood,hauoni kitu kipya katika dunia na utaanza kudhani kwamba furaha yako kuna sehemu imejificha.

Ukweli mchungu ni kwamba hapa duniani kila kitu sisi ndio tuntengeneza,hata furaha tunatakiwa tuitengeneze wenyewe.
 
Umeandika vizuri sana mkuu , tabia ya binadamu ni kutoridhika hiyo ni asili yetu yaan ukipata A unawaza kwanini nisiende B hivyo kadri unavyopata unazidi kuchase kinachofuata ndo maana kutengeneza furaha ya kudumu huwa haiwezekani ! Cha kushangaza huzuni ya kudumu inawezekana kuitengeneza 😂😂😂
 
Ni sahihi.

Tunatengeneza huzuni ya kudumu kwa sababu kuna mambo tunadumu nayo ambayo hayo ndio yanaleta huzuni ya kudumu.

Mfano mtu anadumu na suala la kuamka asubuhi bila kuwa na shukurani na kutafakari umuhimu wa vitu alivyokuwa nayo,kudumu katika hali hiyo ndio kunadumisha huzuni.
 
Hivi kwa mfano mtu alikuwa hataki ndoa akidhani kwamba akiwa single atakuwa na furaha, matokeo yake akaikosa hiyo furaha akaamua kuingia kwenye ndoa sababu anaamini labda huko ndiko ataipata furaha, ila cha ajabu huko nako anakosa furaha huyu mtu anatakiwa afanyaje

Au mtu alikuwa masikini na akawa hana furaha, hivyo akawa anahangaika kutafuta utajiri akidhani kwamba akiwa tajiri ndio atakuwa na furaha, matokeo yake akawa tajiri ila akaikosa hiyo furaha aliyokuwa anaitafuta huyu mtu anatakiwa afanyaje

Mifano ni mingi ila hoja yangu ni, ikiwa kila kitu pamoja na kinyume chake vyote havina furaha, mtu atatakiwa achague kipi
 
🤔🤔🤔🤔
 
Kama kweli furaha inatokana na kitu fulani ambacho unakihitaji jee kwa nini baada ya kupata kitu hiko bado kuna vitu vingine vitakukosesha furaha na kukutia stress ?

Yaani utajikuta umepata mtoto tayari,lakini kodi ya nyumba inakunyima raha

,je ni ipi faida ya furaha ya mtoto kama furaha hiyo haiwezi kuondoa hata huzuni ya kudaiwa kodi ya nyumba ?

Ni ipi faida ya furaha ya kuwa na gari kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kazi nyingi ofisini ?

Ni ipi faida ya kuwa na furaha ya kupata nyumba kama furaha hiyo haiwezi kuondoa huzuni ya kipato kidogo ?

katika haya maisha hicho unachodhani ukikipata kitakupa furaha sio kweli.

FURAHA YA KWELI NI ILE AMBAYO INAKUONDOLEA HUZUNI UNAYOIPATA KATIKA VITU VINGINE.

furaha unayo mwenyewe na wala haipo kwenye vitu unavyovihitaji Kama vile watoto,pesa,nyumba n.k.

Unaweza kutamani gari,ukalinunua na siku za mwanzo ukawa na furaha sana na upya wake.

lakini masiku yakikatika unaliona gari la kawaida hivyo halikupi tena furaha kama ile ya mwanzo,imeenda wapi furaha ile ?

vitu ambavyo tunategemea vitatupa furaha tukishavimiliki tu baada ya masiku kadhaa tunaviona vya kawaida na havitupi tena furaha.

Nilitamani sana kuoa na siku ya kuoa nilikuwa na furaha sana,lakini leo hii sijui furaha ile imeenda wapi na ndoa bado ninayo.

Nilitamani kuwa na mtoto,nilipopata mtoto nilikuwa na furaha sana.

leo mtoto ninaye lakini sijui ile furaha ya mwanzo ya kuwa na mtoto siioni tena na mtoto bado yupo.

Hakuna kitu chochote ambacho ni chanzo cha furaha kwenye maisha yetu isipokuwa sisi wenyewe.

SULUHISHO.

FURAHA TUNATAKIWA KUZITENGENEZA KAMA AMBAVYO TUNATENGENEZA CHAKULA,MAGARI AU NYUMBA.

KUITENGENEZA FURAHA.

furaha tunaitengeneza kwa KUSHUKURU na kutafakari faida ya kitu hicho.

Utakapotafakari faida unazopata kwa kitu fulani na kushukuru basi hapo ndipo furaha utaiona.

Ukiamka asubuhi unaenda kazini kwa daladala sawa hauna gari jee umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa daladala kwako na ukasema asante Mungu..?

Umeshawahi kutafakari kwa uchache umuhimu wa macho yako kwa namna unavyotumia na ukasema asante ?

Je miguu,masikio,pua,mdomo umeshawahi kutakarai kwa ucahche umuhimu wa hivyo vitu kwako kwa namna unavyovitumia ?

Bila kuwa na utaratibu huo utajikuta unaamka kila siku uko bored,hauna mood,hauoni kitu kipya katika dunia na utaanza kudhani kwamba furaha yako kuna sehemu imejificha.

Ukweli mchungu ni kwamba hapa duniani kila kitu sisi ndio tuntengeneza,hata furaha tunatakiwa tuitengeneze wenyewe.
Kwa maneno rahisi furaha ni subjective sio destination!!!
 
Kuna wakati nnatengeneza wazo-nadharia kwamba kuna mambo matatu kama sio manne na leo nitaeleza mawili makubwa yao. Baba lao;
1 Furaha
2. Huzuni
3. Raha
4. Shida
5. Shida na Raha

Furaha inapatikana kwa anayeweza kuelewa tu asiyeelewa yake ni huzuni.

Asiyeelewa pia anaweza kupata shida, au raha

Lakini mwenye kuelewa anaweza kuwa na furaha hata akiwa yupo katika hizo shida na raha.

Tafuta kuelewa, ndipo furaha ilipo ✌
 
Umeandika vizuri sana mkuu , tabia ya binadamu ni kutoridhika hiyo ni asili yetu yaan ukipata A unawaza kwanini nisiende B hivyo kadri unavyopata unazidi kuchase kinachofuata ndo maana kutengeneza furaha ya kudumu huwa haiwezekani ! Cha kushangaza huzuni ya kudumu inawezekana kuitengeneza 😂😂😂
Basi tumeumbwa tofauti sana yani, mimi kuna mambo nayataka maishani nikifanikiwa hayo wala sitohangaika tena. Ni kula bata hadi uzee tu na kubwa kuliko ni "Mpunga" au "Pesa" ya uhakika hilo ndio la muhimu.

Hayo mengineyo yatakuja yenyewe tu as long as grassess are greener.
 
Hivi kwa mfano mtu alikuwa hataki ndoa akidhani kwamba akiwa single atakuwa na furaha, matokeo yake akaikosa hiyo furaha akaamua kuingia kwenye ndoa sababu anaamini labda huko ndiko ataipata furaha, ila cha ajabu huko nako anakosa furaha huyu mtu anatakiwa afanyaje

Au mtu alikuwa masikini na akawa hana furaha, hivyo akawa anahangaika kutafuta utajiri akidhani kwamba akiwa tajiri ndio atakuwa na furaha, matokeo yake akawa tajiri ila akaikosa hiyo furaha aliyokuwa anaitafuta huyu mtu anatakiwa afanyaje

Mifano ni mingi ila hoja yangu ni, ikiwa kila kitu pamoja na kinyume chake vyote havina furaha, mtu atatakiwa achague kipi
Huyo mtu atakuwa na shida basi, yani niamke kwenye account kuna yangu salio linasoma billion 13. Hivi naanzaje kuwa na makasiriko na huzuni?

Internet ipo ya kutosha, naishi comfortable. Siwazi ada za watoto wala kodi ya nyumba. Siumwi chochote mwili wangu uko sawa.
 
Matajiri ugonjwa wao mkubwa ni power mkuu na maswala ya eternal life sababu ya kuhofia kupoteza vingi.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Hivi kwa mfano mtu alikuwa hataki ndoa akidhani kwamba akiwa single atakuwa na furaha, matokeo yake akaikosa hiyo furaha akaamua kuingia kwenye ndoa sababu anaamini labda huko ndiko ataipata furaha, ila cha ajabu huko nako anakosa furaha huyu mtu anatakiwa afanyaje

Au mtu alikuwa masikini na akawa hana furaha, hivyo akawa anahangaika kutafuta utajiri akidhani kwamba akiwa tajiri ndio atakuwa na furaha, matokeo yake akawa tajiri ila akaikosa hiyo furaha aliyokuwa anaitafuta huyu mtu anatakiwa afanyaje

Mifano ni mingi ila hoja yangu ni, ikiwa kila kitu pamoja na kinyume chake vyote havina furaha, mtu atatakiwa achague kipi
Huyu mi ntamshauri afanye kujifunza hali kutoka kwa watu wanaoipenda hiyo hali na kuiishi kwa shukrani kabisa- kama mleta mada alivyosisitiza

Ukiwa single, nenda kwasikilize masingle wengine wanaoufurahia huo usingle katika hali chanya kabisa. Kina 'KATAA NDOA'. Usijifunze kuhusu usingle kwa jicho la wenye ndoa.

Na ukiingia kwenye ndoa, pia kawasikilize watu walio ndoani na wanaoifurahia ndoa kama madam Nifah

Ukiwa tajiri wasikilize matajiri wanaofurahia kuuishi utajiri kwa shukrani na ukitaka kuwa maskini nenda kajifunze uzuri na utamu wa umaskini kwa mabudha wenye kushukuru kabisa kwa kufanikisha kuwa masikini katika dunia ilojaa vitu.

La msingi tu ni kajifunze kuiishi hali husika toka kwa wahusika husika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom