Ni ipi mbegu ya furaha isiyonyauka wala kutikisika?

Nov 2, 2023
60
50
Kwenye maisha yetu kuna muda tunakuwa na furaha na kuyapenda maisha, ila kuna muda hatutamani hata tuwepo duniani mahali tulipo kwakuwa ni huzuni inayo tuzidi na kutupa giza kushindwa kuishi vyema kwenye maisha yetu. Nakupelekea kuchukia maisha kabisa.

Na upotevu wa furaha halisi katika maisha yetu unatufanya tuboreke kwenye maisha na kuzama kwenye mtego wa kutafuta raha ya muda kwenye vitu, au kuwa tegemezi kwa mtu akupe raha japo kwa muda tu ili na wewe ujihisi umepata ladha ya furaha ya maisha.

Hatari ya kutoweza kuelewa mbegu ya furaha halisi itakufanya utumie nguvu zako nyingi sana katika kuishi kwako kutafuta kitu chenye matokea ya raha ili upate ahueni ya kufurahia maisha tena. Iwe chakula, iwe mahusiano au burudani yoyote itayo kurudisha kwenye uzima wako wa kufurahia maisha tena, na huu ni utumwa si uhuru kwenye maisha kutegemea tu kupewa raha.

Ni rahisi sana siku hizi kuwa watumwa katika mapenzi kwa kuwa tunahisi kama ndio tegemeo letu la kutupa furaha na kutupa maana ya maisha. Tumeweka nguvu kutafuta vitu vya kurefusha matendo ya mapenzi kwa kufikiri tutaipata furaha lakini tunaishia kujiumiza kwakwenda kinyume na miili yetu uwezo wake wenye afya. Kama umepanda mbegu ya furaha akilini mwako hutokuwa wa kukimbizana na raha ndogo ndogo kwakuwa umeshaotesha mbegu ya furaha na mzizi kushika.

Mbegu ya furaha ina maana gani?

Tuweke hili sawa kwanza, furaha haihusiani na mipango yako yoyote kwenda sawa. Wala haipatikani kama hatua ya mwisho ya kufanikisha jambo fulani, wala haipo unapokuwa na matumaini mema. Kwa ufupi huwezi kuitafuta wala kuisubiri furaha ikufikie katika maisha yako.

Mbegu ya furaha inanza kuota pale unapoelewa ukweli halisi "to understand facts" kuhusu jinsi unavyoishi kwenye maisha yako ndani ya ulimwengu, bila kuficha chochote na kuwa wazi kabisa katika akili yako mwenyewe binafsi kuweza kuona, kufahamu na kutambua jinsi gani akili yako inavyojiakisi katika mazingira yako na kuelewa kabisa hilo.

Ni unaingia ndani yako kuelewa mawazo yako, hisia zako na mwenendo wako wote wa kifikra na kupata uhuru kwenye kuelewa jinsi mazingira yako yanavyo kutengeneza kwa kukushawishi kuwa na wewe jinsi ulivyo. Ukiweza kuondoa ujinga na giza lote linalokuletea mkanganyiko na kuchanganyikiwa na kuleta amani na utulivu na umoja wa akili yako kwa kujua thamani yako halisi si kutokana na kitu chochote bali kuweza kuwa na ufahamu wote wa akili yako jinsi inavyoshiriki katika mazingira yako na kuacha kukinzana nayo na hiyo ndio mbegu ya furaha isiyokwisha maishani mwako.

Tatizo letu kubwa ni kutojifahamu tu, na ujinga wetu ukituendesha basi kila kitu kina haribika na tunapoteza ubora wetu na kujithamini kwetu. Na inakuwa ni rahisi kwa watu kutuendesha wanavyotaka kwakuwa wanajua tumekuwa tegemezi kwao kuweza kupata faraja kwenye maisha.

Nb: Ni wewe pekee unayeweza kujikomboa mwenyewe kwenye hili, hakuna mwenye wajibu huo wala atayeweza kufikia kupanda mbegu ya furaha ndani yako zaidi ya wewe mwenyewe kujielewa wote bila kuficha na kuelewa kwanini uko hivyo.
 
Upo sahihi ,nambie haya MAARIFA umeyapata baada ya kusoma Kitabu gani?
 
Hakuna kitabu kikubwa kama kuwa makini na maisha unayoishi
YEs kwa sababu wao walioandika vitabu walikuwa makini na maisha waliyoishi then wakajifunza kupitia maisha hayo ndio zile ideas wakazitia kwenye vitabu na leo tunasoma

Hivyo mtu akiwa na kawaida ya kuwa mdadisi wa kuyasoma maisha anayoishi na maisha ya wengine wanavyoishi basi mtu huyo atakuwa na maarifa ambayo yanafanana na yale ya vitsbuni.
 
Back
Top Bottom