Furaha yako iko kwako

Love Doctor

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
726
786
Wewe ni wewe 🫵

Hisia ni nini?
Hisia ni kiungo cha ndani cha mwanadamu, hisia huonekana katika kila jambo la mwanadamu, furaha ni moja katika hisia chanya.

Hisia ya furaha ni hisia muhimu sana kwa mwanadamu. Furaha huongeza nishati mbadala katika mwili wa mwanadamu, kama ulivyo upweke una madhara basi furaha ni faida. Unaachaje kuipa furaha nafsi yako?

Dini zote zinahimiza uwe na furaha kwa sababu furaha inajenga afya yako ya akili na kiroho na kupunguza msongo wa mawazo.

• Furaha yako inakutegemea wewe mwenyewe ni jukumu lako.
• Furaha utaipata katika maamuzi yako.
• Furaha itakupa amani.
• Furaha inatoa ufunguo wa maisha yako ya sasa na baadae.
• Furaha inahitaji juhudi ili kuhakikisha unabaki nayo siku zote.
• Tafuta msaada unapoona furaha yako imetoweka.
• Tafuta kufurahi popote ulipo kwenye mazingira yoyote, watu wako vitani na wanafurahi wewe unakosaje furaha?
• Kama furaha yako ni kupata pesa tafuta pesa.
• Furaha ndio maisha yenyewe, hutapata furaha kwa kuingilia furaha za watu wengine. Kila mtu na tabia yake na furaha yake jua namna ya kudhibiti hisia zako za furaha.
• Furaha zetu hazifanani usimlazimishe mtu utatafuta kuondoka kwa furaha yako.

Ukikosa Furaha;
• Unapunguza uwezo wa akili kufanya kazi.
• Hutokuwa na uhusiano mzuri na watu.
• Kudhoofu kimwili.
• Kutokujiamini.
• Kupungua kwa guvu za kiume.
• Kuwa mkavu na kukosa msisimko
• Kua na maamuzi mabaya.
• Kujihisi uchomvu muda wote.
• Utalaumu na kuhisi kuonewa.
• Kutamani kujidhuru au kujiua.

Ongea na watu ujenge furaha, zungumza na wataalam urudishe furaha yako. Kucheka sio alama pekee ya kufurahi kama ilivyo kulia si alama pekee ya huzuni.

Furaha iko ndani yako huna haja sisi tuione, ukiwa na furaha utanawiri tu mpaka wakuonee wivu, furaha haiuzwi ila vitu vinavyoweza kusababisha furaha vinauzwa.

Hakikisha unafurahi maisha yaende. Pesa haiwezi kununua furaha ni kweli lakini pesa kuikosa kutakunyima furaha amua mwenyewe uwe nayo au uikose.

Furaha yako ni maisha yako na vyoote vipo katika mikono yako.

Abuuabdillah
0744883353
Jumaomari5@gmail.com
 
Back
Top Bottom