hadhari ya kamera kwa wenye SMARTPHONEs
nenda Google play store: pakua SPEED CAMERA, install kisha fanya settings kwa ku-connect na google map.
ukianza safari; hakikisha una bundle na uweke DATA ON; weka simu yako karibu na upeo wa macho yako mf. dashboard au gear lever/gear stick. we ruhusu mguu ucheze na accelerator pedal upendavyo huku jicho likitua 'kimakengeza' kwa smartphone yako.
*ukiweza kufanya settings vizuri waweza kuwa una-oversee uwepo wa kamera njia unayotarajia kupita
*ukiikaribia kamera, smartphone yako itatoa alarm/alert kuashiria upunguze endapo utakuwa una-cruse over 50km/h
*jenga mazoea ya kukimbia <48km/h kabla hujafikia kibao cha 50km maana hawa watani wa madreva wana tabia ya kujificha na kupiga picha hata kabla hujakanyaga eneo la tukio.
*changamoto kubwa ni charge ya simu yako. kama ukiwa na chaja ya kiberiti (madereva mnajua) au power bank itakusaidia
[HASHTAG]#Samahani[/HASHTAG] kwa 'Kiswanglish' aghalabu sipendi itokee ila leo nimejikita kuinakishi rejesta mujarabu kwa madereva wa rika la 15-30
asante