Huyu Traffic hajipendi, aache Sifa!!

Huyu Traffic hajipendi, aache Sifa!!

Hii mitindo ya kukupiga picha na kuwatumia wenzake mbele huwa mara nyingi inakosa uthibitisho kabisa, mimi huwa nauliza una uthibitisho gani zaidi ya picha kuwa nimepita kwenye speed limit wakati picha haionyeshi alama yeyote, naomba ambaye ameshapelekwa mahakamani atoe ushuhuda hakimu aliamua vipi kwa ushahidi wa picha peke yake
 
Sasa mkoba na viatu vya kike vipi? Au huwa wanakuwa zamu wawili wawili?
 
Inabidi watumie hii njia ya kujificha ili waweze kupata chochote kitu kwani madereva nao wamekuwa wajanja wanapeana ishara kiasi kwamba imekuwa vigumu kunaswa katika hali ya kawaida.
 
wa daraja la kigamboni wanjificha nyuma ya nguzo
 
Hii mitindo ya kukupiga picha na kuwatumia wenzake mbele huwa mara nyingi inakosa uthibitisho kabisa, mimi huwa nauliza una uthibitisho gani zaidi ya picha kuwa nimepita kwenye speed limit wakati picha haionyeshi alama yeyote, naomba ambaye ameshapelekwa mahakamani atoe ushuhuda hakimu aliamua vipi kwa ushahidi wa picha peke yake
Inaonyesha gari na speed unayotembea nayo muda huo, mwenye picha ya lile basi liliopata ajali miezi michache iliyopita anaweza kuiweka hapa. lilikua liko 120km/hr na muda mchache baadae ndio waligongana uso kwa uso na mwenzie
 
Huyo lazma atakua Singida, maaskari wa Singida wana njaa, anajificha kichakani na camera yake afu picha anaituma whatsapp unakamatwa mbele....
 
Inabidi mjifunze kutii sheria bila shuruti, na mimi nasema MPIGWE TU maana hamna namna. Huwa mnajifanya kutii sheria mkiwaona na nguo nyeupe wameanika vitambi barabarani sasa huyu wacha awanyooshe pambaff. Unadhani usalama barabarani ni kwa faida ya mkewe?
 
Sasa mkoba na viatu vya kike vipi? Au huwa wanakuwa zamu wawili wawili?
MANI zumbemkuu lusungo BAK
Asubuhi wakati anaondoka nyumbani kachukua "kikoi" cha mke wake kabisa kwa ajili ya kukalia hahahaha kamwambia "ukinipa hicho kikoi nikienda nacho leo, nakuhakikikishia jioni unakula kitimoto na bia na Kesho Jumamosi lazima uende saluni ukasuke ule msuko uupendao, wee nipe tu hicho kikoi utafurahi"
 
Hii mitindo ya kukupiga picha na kuwatumia wenzake mbele huwa mara nyingi inakosa uthibitisho kabisa, mimi huwa nauliza una uthibitisho gani zaidi ya picha kuwa nimepita kwenye speed limit wakati picha haionyeshi alama yeyote, naomba ambaye ameshapelekwa mahakamani atoe ushuhuda hakimu aliamua vipi kwa ushahidi wa picha peke yake

Wanakupigia kwenye kibao cha speed limit na kinaonekana kabisa kwenye hiyo picha na gari lako na spidi uliyopo
 
Ha ha ha ha nimecheka sana, dawa yao ni kusafiri usiku
Usiku hakai hapo hata kwa dawa... hivi akikalia siafu hapo itakuaje? Maana siafu bhana hakuumi huku ambako utamuona, atapanda kimya kimya hadi afike zile sehemu laini, zenye joto kidogo. Pale unapokua umetulia kabisa ndio anakushtua.
 
Back
Top Bottom