aliisaac1000
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 407
- 272
True, mie kwa bahati nilipata kutembelea huko nikashuhudia wingu la mifugo likirandaranda na hii ndio tatizo la wanasiasa wetu ambao wamefumbwa macho na wafugaji sijui kwa maslahi yanani! Tunaeza ishi bila kula nyama lakini sio chakula, kibaya zaidi tunashuhudia waziri mwenye dhamana Mh. Mchemba nae akitoa matamshi ya kukatisha tamaa, eti nguvu kwake ndio suluhisho! Toka nilivyomsikia nimegundua kumbe ana uwezo mdogo na hiyo wizara hakustahili. Kingine nilichokigundua askari wengi waliopekekwa kutumika huko na hisi wanatoka nje ya mkoa husika hivyo wameshindwa ku ' integrate' vizuri na wenyeji kwa hali hiyo wanakosa ushirikiano na inavyoonekana hawakubaliki sawa na askari wa bara kumpeleka Pemba unategemea nini! Mimi bado na question uwezo wa polisi wetu kwenye suala zima la taaluma ya 'upelelezi' watu wengi wameteseka bila ya kosa kwa kisingizio cha upelelezi, upelelezi gani unachukua zaidi ya mwaka kama si uonevu? Na kwanini umkamate mtu kama bado hujadhibitisha makosa yake?! Marekani polisi kamwe hamkamati mtu hadi awe na ushahidi kwa asilimia 90% ndio mtuhumiwa atakamatwa na mahakimu hawapati wakati mgumu wa kukaa na kesi kwakuwa polisi wamewarahisishia kazi ya kutoa hukumu kinyume na ilivyo kwa huku kwetu,Wanachokifanya wafugaji ambao ni wahamiaji huko kusini ni unyanyasaji na uonevu kwa wenyeji. Hili litaleta shida Leo , kesho na kesho kutwa.
Ni jambo la hatari sana kama mtu anaweza kutembea na mifugo kutoka Mwanza au Arusha na kuhamia nayo ikwiriri au rufiji au morogoro na kuiswagia kwenye shamba la mtu anayemkuta huko. Huu ni zaidi ya uonevu.