Huyu ni mtu pekee anayefahamu vyema yanayotokea Kibiti na Ikwiriri na huenda akawa na majibu yake

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,015
Mwaka 2012, Huko Ikwiriri wakati wa mapigano ya wakulima na wafugaji, aliyekuwa kamanda wa operesheni maalumu wa jeshi la polisi SACP Simon Sirro alitumwa kwenda kuweka mambo sawa.

Sirro akazungumza na wakulima, wafugaji, viongozi na polisi wa ikwiriri, lakini cha ajabu kidogo(kwa viongozi wa Tanzania), Simon Sirro alifanya jambo nadra kulifanya kwa viongozi wa kiafrika.

Akitoa majumuisho ktk mkutano wa hadhara akawatuhumu jeshi la polisi wa Ikwiriri Kuwa ndo chanzo cha mgogoro huo, kwani wamekuwa wakichukua "maziwa" kwa wafugaji na kusababisha kutotenda haki.

Akaendelea kuwalaumu polisi kuwa wanapaswa kutenda haki na "hali hiyo ikiendelea italeta shida na shaka siku za mbele".

Leo ni miaka mitano tumeona utabiri wa Simon Sirro, Mauaji ya polisi, viongozi wa chama dola na serikali wakiwa ni walengwa zaidi.

Hata ukweli upingwe vipi ila kwa sura ya nje Kibiti na Ikwiriri Kuna tatizo kubwa, huenda kuna kundi linalipa kisasi kwa uonevu walioupata mahala.

Kwa sasa ni mtu mmoja tu anaweza kutumia akili, uwezo na busara zake kuweka mambo sawa Kibiti, ni kamanda wa polisi wa mkoa wa DAR ES SALAAM wa sasa ndugu yangu Simon Sirro.

Nina hakika hata jeshi la polisi likiamua kufanya reform na likafanya mapinduzi ya kimuundo na kiutawala ili kujiweka ktk hali ya kukwepa lawama na chuki dhidhi yake kama raia kubambikiwa kesi, kujiingiza ktk siasa, matumizi makubwa ya nguvu, changamoto za ndani ya jeshi nk. huenda huyu bwana akaweza kuwa ni kiongozi wa mabadiliko hayo.
 
KINACHOKATISHA TAMAA MAENEO YA KIBITI NA RUFIJI: WALE WANAOENDA KUTOA TAARIFA ZA SIRI POLISI NDIO HUTOKEWA NA MAJAMBAZI NA KUUWAWA! SWALI, MAJAMBAZI WANATOA WAPI HABARI KUA FULANI KAPELEKA TAARIFA POLISI? JE POLISI YA HUKO KUNA WAHALIFU WNAOSHIRIKIANA NA WAHALIFU?
 
Wanachokifanya wafugaji ambao ni wahamiaji huko kusini ni unyanyasaji na uonevu kwa wenyeji. Hili litaleta shida Leo , kesho na kesho kutwa.

Ni jambo la hatari sana kama mtu anaweza kutembea na mifugo kutoka Mwanza au Arusha na kuhamia nayo ikwiriri au rufiji au morogoro na kuiswagia kwenye shamba la mtu anayemkuta huko. Huu ni zaidi ya uonevu.
 
Solution ni kujenga kambi kubwa ya kijeshi huko ikwiriri/kibiti otherwise tutegemee matukio ya mauaji kuwa mengi zaidi....

Hivi umesoma na ukaelewa mada kweli?

Chanzo kulingana na mleta mada ni "Polisi kutotenda haki....ni Polisi kuwa waonevu...". Hivyo basi wingi wa wanajeshi/polisi sio tiba kwa sababu chanzo sio uchache wa askari Rufiji/Ikwiriri. Majibu lazima yawe yanajibu tatizo sio kulazimisha mambo.
 
kwaiyo tatizo ni nini uko?
1, ugaidi
2.majambazi
3wakulima na wafugaji(visasi
 
Mwaka 2012, Huko Ikwiriri wakati wa mapigano ya wakulima na wafugaji, aliyekuwa kamanda wa operesheni maalumu wa jeshi la polisi SACP Simon Sirro alitumwa kwenda kuweka mambo sawa.

Sirro akazungumza na wakulima, wafugaji, viongozi na polisi wa ikwiriri, lakini cha ajabu kidogo(kwa viongozi wa Tanzania), Simon Sirro alifanya jambo nadra kulifanya kwa viongozi wa kiafrika.

Akitoa majumuisho ktk mkutano wa hadhara akawatuhumu jeshi la polisi wa Ikwiriri Kuwa ndo chanzo cha mgogoro huo, kwani wamekuwa wakichukua "maziwa" kwa wafugaji na kusababisha kutotenda haki.

Akaendelea kuwalaumu polisi kuwa wanapaswa kutenda haki na "hali hiyo ikiendelea italeta shida na shaka siku za mbele".

Leo ni miaka mitano tumeona utabiri wa Simon Sirro, Mauaji ya polisi, viongozi wa chama dola na serikali wakiwa ni walengwa zaidi.

Hata ukweli upingwe vipi ila kwa sura ya nje Kibiti na Ikwiriri Kuna tatizo kubwa, huenda kuna kundi linalipa kisasi kwa uonevu walioupata mahala.

Kwa sasa ni mtu mmoja tu anaweza kutumia akili, uwezo na busara zake kuweka mambo sawa Kibiti, ni kamanda wa polisi wa mkoa wa DAR ES SALAAM wa sasa ndugu yangu Simon Sirro.

Nina hakika hata jeshi la polisi likiamua kufanya reform na likafanya mapinduzi ya kimuundo na kiutawala ili kujiweka ktk hali ya kukwepa lawama na chuki dhidhi yake kama raia kubambikiwa kesi, kujiingiza ktk siasa, matumizi makubwa ya nguvu, changamoto za ndani ya jeshi nk. huenda huyu bwana akaweza kuwa ni kiongozi wa mabadiliko hayo.
Mh Mwigulu upo humu? Hoja hiyo imerudiwa zaidi ya mara tano. Uzi huu upate mtizamo positive.
 
Kwa mtazamo wangu, mambo yafuatayo yanaweza kuwa chanzo kikubwa cha yanayoendelea Rufiji na mkoa wa Pwani kwa ujumla.

1) Kuvunjika kwa uhusiano na ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Wakaazi wa maeneo husika (yametajwa mengi mfano rushwa, uonevu, kubambikiza kesi, biashara haramu, uhalifu usioshughulikiwa nk)

2) Migogoro sugu kati ya Wafugaji na Wakulima (kila mtu analifahamu vema)

3) Ukosefu wa Ajira (An idle mind is a devil's workshop)

4) Misuguano na mitazamo ya kisiasa na kijamii vs dini.

5) Udhaifu wa Serikali na Uongozi wa nchi, wizara na taasisi zake kushughulikia matatizo kabla hayajakomaa.

6) Nafasi ya Elimu na Siasa katika kuchughulikia matatizo ya wakaazi wa Rufiji/Kibiti/Bagamoyo nk mpaka sasa ni mdogo sana.
 
Kuna viongozi vishoka.

Ni bahati mbaya na hasara kwa Taifa kwamba awamu hii wako wengi tu.
 
Hivi umesoma na ukaelewa mada kweli?

Chanzo kulingana na mleta mada ni "Polisi kutotenda haki....ni Polisi kuwa waonevu...". Hivyo basi wingi wa wanajeshi/polisi sio tiba kwa sababu chanzo sio uchache wa askari Rufiji/Ikwiriri. Majibu lazima yawe yanajibu tatizo sio kulazimisha mambo.
Tumia akili wewe,hao wenyeviti wa ccm nao ni polisi?
 
Solution ni kujenga kambi kubwa ya kijeshi huko ikwiriri/kibiti otherwise tutegemee matukio ya mauaji kuwa mengi zaidi....

Kambi ya kijeshi ndio itafanya nini?, hao wauaji hawana uniform wako kiraia sasa hao wanajeshi watawatambuaje?
Swala la Kibiti au tuseme Rifiji kwa ujumla wake linahitaji busara na interejensia ya nguvu kuweza kujua shina la yote liko wapi, hao jamaa wanaoneka wako very skilled na wanajua nini wanachokifanya so sidhani kama nguvu ni suluhisho kwa sasa unles umeshajua wako wapi na wamejizatiti vipi ndio nguvu itahitajika,
 
Back
Top Bottom