Huyu ni mnyama gani?

Nungu nungu hilo ulilotaja nila kilugha
Huyu ni hedgehog kwa kijaluo siyo pocupine!

Hedgehog ni karunguyeye hilo jina kidungumaria nahisi ni la Kichgga coz tulitumia Moshi. Kenyewe ni kadogo hafiki kilo mbili. Kapo kama panya ila manyoya yake ikawa miiba!! Kanaishi kwenye makazi kanakula mabaki ya vyakula.

Pocupine ndiyo nungunungu, yeye ni mkubwa na anaishi porini
 
Kama wadau walivyomtaja hapo juu acha niongezee kitu.

Baadhi ya kabila Wanaamini pia hichi kijitu kinabahati mfano ukikutana nae basi wanadai kuna mambo mazuri yatakuwa nayaendelea juu yako.

Pia zamani tulikuwa tunaweka ngozi yake katikati ya mbegu za mahindi ambazo tunaenda kuotesha kwa imani hiyo kuwa ana bahati.

Pia hafugiki na ukitaka mfuga kuna muda atakupotea bila kujua.
Huyu haliwi kwa utamaduni wetu.(🤣🤣 ila nadhani twajua china hawapitwi na kitu).
Na hiyo miba yake haichomi japo ukitaka mshika anajitunisha inakuwa kama yakwarua
 
Wakati ni mtoto mwiba wake nilikuwa nachomewa na kuwekewa moshi puani pindi damu ikianza kutoka na ilikuwa inakata
 
Back
Top Bottom