Sasa ni dhahiri kwamba Godbless Lema ni mwamba wa Kaskazini na mtu hatari zaidi kwa uhai wa CCM Arusha.
Kampeni za uchaguzi wa Kata nne jijini Arusha zimechukua sura ya kitaifa kutokana na umuhimu wake.Kwamba ushindi wa Chadema katika kata zote maana yake Meya wa CCM Gaudence Lyimo afungashe virago na akabidhi utawala wa jiji hilo kwa Chadema.
Godbless Lema ameongoza kampeni za Chadema tangu kampeni zianze na amekuwa akikusanya umati mkubwa wa watu katika mikutano yake.Kutokana na mamia ya watu wanaomfuata kila anakokwenda Lema anaonekana kama shujaa halisi wa siasa za Arusha.
Nguvu ya Lema Arusha imesababisha CCM kutoka mafichoni na kuleta karibu viongozi wote wa kitaifa hapa Arusha kukabiliana na nguvu ya mpiganaji huyu.Mawaziri kadhaa waandamizi wamekuwa wakipishana kila kata kujaribu kukabiliana na Lema bila mafanikio.
Kwa upande wake Chadema imemuamini Lema pekee akisaidiwa tu na vijana wadogo maarufu kama Makamanda wa Arusha Town.Hakuna kiongozi yeyote wa kitaifa wala Kamati kuu aliyekuja Arusha zaidi ya Freeman Mbowe aliyealikwa kufunga kampeni leo.
CCM wametumia mamilioni ya pesa kukabiliana na Lema lakini walichoambulia ni Zomeazomea kila wanakopita.Wakati mikutano ya Lema inahudhuriwa na watu karibu elfu moja kila inapoitishwa,CCM kwa upande wake wanahudhuria watu wasiozidi mia moja tena wengi wao wakiwa watoto na watu wanaohama nao kutoka kata moja hadi nyingine.
Hata hivyo CCM wamejifunza kitu kimoja kwamba Lema si mtu rahisi kama wanavyodhani bali mwanasiasa huyo kijana ni tishio kuu kwa uhai wa CCM Arusha.Pia wamefahamu kwamba Lema anapendwa hapa Arusha mfano wa mama mzazi anavyompenda mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.
Kwa hali ilivyo hapa Arusha ushindi wa Chadema kwa kata zote nne hauna shaka yoyote.Tena utakuwa ushindi mkubwa kuwahi kutokea siku za karibuni.Rafiki yangu mmoja aliyeko kwenye kamati ya kampeni ya CCM alinieleza lengo la CCM kwa sasa si kushinda bali walau kupunguza idadi ya kura za Chadema ili CCM isishindwe kwa kura za aibu.