WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 946
Pichani spika wa jamhuri ya Burundi kwa jina anaitwa Paschal Nyabenda. Kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya Burundi huyu ndie atakuwa raisi wa muda mpaka mwisho wa mwezi wa name mpaka atapoapishwa raisi aliyeshinda uchaguzi wa mwaka bwana generali Evariste Ndayishimiye.
Nyabenda atashika nyadhifa hi kwa muda tokana na matakwa ya katiba ya jamhuri ya Burundi. Katiba inafanunua endapo raisi atafariki au kushindwa kuongoza tokana na maradhi basi spika wa jamhuri ya Burundi ndie atakuwa raisi wa muda mpaka raisi mwingine atapopatikana kupitia uchaguzi mkuu.
Kwa bahati nzuri uchaguzi ulikuwa umeshafanyika na kumpata mshindi bwana generali Evariste Ndayishimiye ambae atapishwa mwishoni mwa mwezi wa nane. Bunge la jamhuri ya Burundi litakuwa chini ya naibu spika bwana Agathon Rwasa pichani.
Paschal Nyabenda kazaliwa 12/4/1966, mnamo mwezi 6/2020 alifanywa kuwa acting president of Burundi.
Amewahi kuwa gavana wa Jimbo la Bubanza kupitia chama tawala Cha CNDD–FDD na pia amewahi kushika hatamu mbali mbali Kama unaibu spika wa jamhuri ya Burundi.