Huyu ndie Padre aliyeuawa Zanzibar

Huyu ndie Padre aliyeuawa Zanzibar

...............Kumbe Tanzania inaelekea huku.......? RIP Fr. Mushi. Roho za watakatifu zinaendelea kumlilia Mungu kwamba ni lini atawaadhibu hawa watu wanaoua wenzao ambao hawana hatia?
 
2013-02-17+10.58.55-1649158318.jpg


Nenda kwa amani Father, MUNGU ameruhusu hili litokee. RIP

Wauaji wamepata faida gani? wasubiri hukumu yao.
 
dah kwa kweli kuna watu wamezaliwa katili forever
eeh mungu ipokee roho ya marehemu
 
Sijakuelewa unachomaanisha, uchunguzi hauwezi kufanyika kwa namna unayopendekeza wewe, what is the basis for your hypothesis formation.!??
Nina maana huyu padri alikuwa na maisha binafsi pia kama mwanadamu mwingine yeyote, tunaweza kufanya makosa makubwa ikiwa tutakuwa tunahusisha tu nafasi yake ya kazi kwa kuona ni chuki tu dhidi ya ukristu au uislamu.
Tumeshuhudia kashfa kubwa kubwa zilizoligubika kanisa katoliki duniani hadi kupelekea Papa mwenyewe kujiuzulu kwa uzito wa kashfa dhidi ya kanisa hilo.
 
Serikali ya Kikwete ni dhaifu tangia udini umeanza kuchoma makanisa na kuwa watumishi wa Bwana Mungu,hamna alie tiwa nguvuni na wakitiwa nguvuni wanatoka kwa midhamana.Haya mambo hayataisha kama hamna hatua kali kuchukuliwa.

Toka kwa MrArsenal
 
Nina maana huyu padri alikuwa na maisha binafsi pia kama mwanadamu mwingine yeyote, tunaweza kufanya makosa makubwa ikiwa tutakuwa tunahusisha tu nafasi yake ya kazi kwa kuona ni chuki tu dhidi ya ukristu au uislamu.
Tumeshuhudia kashfa kubwa kubwa zilizoligubika kanisa katoliki duniani hadi kupelekea Papa mwenyewe kujiuzulu kwa uzito wa kashfa dhidi ya kanisa hilo.

Sipingani na mtazamo wako,ila ni vema wachunguzi wakatoka na majibu kutoakana na uchunguzi na sio waingie kwenye uchunguzi na pre conceived answers
 
JK anahusika na haya mauaji, haiwezekani akawa anataarifiwa kuhusu chokochoko hizi tangu awali alafu yeye anakaa kimya.
 
you shut up hakuna aliyesema waislamu wameua ila mnajishtukia wenyewe u Better quit tunamsikitikia FATHER wetu,,, nan asiowajua nyinyi. RIP FATHER

napenda nikuunge mkono! Kuna taharuki kubwa kwa wenzetu, hakuna aliyewaambia wanahusika lakini wamejitokeza kulaani, kufananisha mauaji ya Padri na kumwagiwa tindikali kwa Shekhe huko Zanzibar, kuelezea hakuna udini ni ujambazi, wengine hata kutoa madai ya uhusiano wa kijamii! Inadhihirisha uongozi wote wa Uislamu wanafahamu kilichotokea na ukisikiliza yale mahubiri ya kada wao kule Mwanza kuhusiana na kuuawa kwa Sheik yule wa Mombasa, unajua nini kinachoendelea.

Mungu atalipiza kisasi sio sisi! RIP Evarist
 
tusichukulie matatizo makubwa kama mepesi...mjumbe natumaini masaburi hayakutumika ktk kufikiria ulichokiandika hapo juu..maana,ts aagghh!
Uchunguzi wa kina ufanyike ukizingatia maeneo yafuatayo:

1. Kumewahi kutokea malumbano specific katika kanisa lake baina ya waumini na mapadri?
2. Padre alikuwa analalamikiwa katika jamii anayoishi? kwa lipi?
3. Je! Padre alikuwa na mahusiano yoyote na watoto wadogo hasa wakiume? wakati wowote ule?
4. Je! Padre kama mchagga alikuwa nafanya biashara yoyote akiwa Padre? kuzulumiana kukoje?
Nk NK
 
Pumzika kwa Amani Padri. Pole kwetu sote tulioguswa na mauaji haya!
 
Apumzike kwa amani, Mungu wetu si Kiziwi na wala Yeye si kipofu!
 
Back
Top Bottom