Huyu mzungu ametuchanachana aisee!!

Huyu mzungu ametuchanachana aisee!!

Hapo vip!!

Nimejaribu kusoma maelezo ya mzungu mmoja, kwenye hyo attachment hapo chini, nikamkumbuka Trump alisema, waafrika tumejee kwenye industries ya dini tukiamini umaskini inaletwa na pepo!!
Maneno ya mpangani ayawezi kuwa sawa na muamini,hizo hizo dini walizotuletea zimetufanya kuwa wastarabu na kuelimika pia kuwafukuza wakoloni maana wapigania Uhuru wengi walipata mwanga kupitia shule za wamissionary.
 
Hapana mkuu, historia Inaonesha kwenye imani za dini hizi ndiko kwenye maovu sana. Chukulia tu hata kwetu Afrika, maisha kabla ya hizi dini na baada ya dini. Mfn. Ushoga kwetu unahusishwa zaidi na jamii za Pwani na visiwani ambako dini zina zaidi ya karne kadhaa.

Halafu sheria za Mungu haziko tu kwenye vitabu, Mungu sio Magufuli hata ategemee makaratasi kukupatia sheria zake, zipo tu kwa kila kiumbe, ziko wazi hata panya, nyoka na miti inazijua na kuzitii ama kuzivunja.

Mbwa au paka wanajua kabisa kuiba ni kosa, hili ni bila kufundishwa.
Umesema kweli, kila kiumbe anazo sheria za Muumba wake ndani ya nafsi. Huu ujuzi wa watu wengine kujifanya wana mungu mzuri zaidi ndiyo shida.
 
Huyo alichokiandika ni non sense Kabisa hata kama Mimi Sijui kiingereza na tena atuache na Imani zetu nzuri na za Baraka,hao watu ni anti Christ so hawawezi kusema chochote juuu ya
UKristo
 
A few factual errors: "China ni miongonij mwa nchi zenye waumini wachache"-Dini za Confusius na Buddhism zona waumini wengi kuliko Wakristo na waislamu combined!
 
Nchi pekee iliyoendelea kwa dini ni Roma, sadaka za dhahabu fedha na vito, ukwepaji mkubwa wa kodi ndiyo mtaji wao"-Roma haikuwepi kodi. Makubaliano ya Rome kunilipa kid I yalifikiwa kati ya Vatican na serikali ya Dikteta Musolini. Vatican iliomba kusamehewa kid I na enyewe, kupitia ushawishi wake, iwasababishe waumini wake kumtii Dikteta Musolini!
 
Hajasema kwamba tusiamini kuwepo kwa Mungu, after all, tulishanza kuamini hivyo hata kabla ya ujio wao, anachosema ni ujinga wa kuendelea kuwaamini miungu ya kigeni ktk Ugeni uleule tuloletewa nao, namuunga mkono... Ni ujinga uliotukuka.
Ukristo ndiyo uliondoa utumwa katika pwanj ya Africa Mashariki na Magharibi karne ya 19.
 
Hapo vip!!

Nimejaribu kusoma maelezo ya mzungu mmoja, kwenye hyo attachment hapo chini, nikamkumbuka Trump alisema, waafrika tumejee kwenye industries ya dini tukiamini umaskini inaletwa na pepo!!
What about islamic
 
Ukristo ndiyo uliondoa utumwa katika pwanj ya Africa Mashariki na Magharibi karne ya 19.
Hapana, sio Ukristo uliondoa utumwa, bali ni mageuzi ya viwanda na ukoloni. Biblia inaruhusu utumwa. Kwahiyo kummiliki mtu kiutumwa si dhambi ktk Ukristo.
 
Msingi mkuu wa dini zote ni kudhibiti watu uwatawale na umiliki mali. Dhana ya Mungu imewekwa kuufunika ukweli huo. Wenye akili ya kuhoji hujipambanua na huonekana wapinga imani. Wasio na uwezo wa kuhoji hukesha wakilia na kurukaruka makanisani mpaka wigi zinadondoka.
 
Despite his words, kuamini huko kunatufanya tuwe na amani. Nawaza tu kwamba wanadamu wasingekuwa wanaamini uwepo wa Mungu nini kingeendelea duniani.. Hata huyo aliyeandika yawezekana asingekuwepo. Hofu ya Mungu ndio inayofanya watu wasifarakane zaidi au kuuana au kutendeana mabaya
 
Ukweli unauma ila alichokiandika ukikitafakari kwa kina ni sawa yupo sahihi kabisa, dini za kigeni zililetwa afrika ili kupumbaza na kurahisisha utawala wa kikoloni
 
Dini/ Imani ndio ugonjwa mbaya kabisa wa akili kuwahi kutokea hapa duniani
 
Back
Top Bottom