Mkuu
nendiwekilasa,
Pole..lakini usitumie lugha kali na mbaya sana kwa mmeo(presumably) mf. ("Lipo" tuu, "lipo" busy, "lipo" macho)..nadhani ungejiuliza ni wapi kuna shida...yaani kwako binafsi, kwa mwanaume au kati yenu wote.
Kwa kuanza(Kwako binafsi), hakuna jambo ulilomkwaza na hivyo akaamua "kukuadhibu" kwa njia hiyo?kama hakuna jaribu kuongea naye/kudadisi pengine kuna jambo linalomsumbua hata huko kazini(work under pressure) linalomfanya awe jinsi alivyo sasa.
-Kama hakuna kati ya hayo then labda kuna shida kati yenu wote.
Personally, nadhani unamwamini maana kipindi hicho chote kama usinge mwamini "usingempa hiyo nafasi ya kusema leo basi" hivyo Kumbuka yale mazuri mliyokuwa mnafanyiana mwanzoni mwa uhusiano, unaweza kujaribu pia..
Waweza muandaa toka akiwa kazini(kumfanya atake kuwahi nyumbani..kwa mambo mazuri ofcourse)...kwa namna yeyote ile, pili mapokezi na jinsi atakavyojaliwa atapofika nyumbani, mazingira(kumbuka ndiyo weekend hii)..vinaweza kumfanya kubadilisha mawazo hata kama alikuwa hataki hapo mwanzo.
Tafadhali usitoke nje, wiki moja ni ndogo sana(sina kipimo cha kusema muda flani unafaa) lakini jiulize kama ulishawahi kuwa mjamzito, au pata uzoefu wa marafiki waliokuwa wajawazito tayari..waume wao hawakutoka nje, waliendelea kuvumilia hivyo hivyo! Na je, ukitoka nje ukagundua kuwa alikuwa anatatizo kweli utafanya nini? Na yeye akifanya kulipiza kisasi, au wakati wa ujauzito when you need most(mfano tu)!?
Punguza hasira, dadisi shida iko wapi, muandae(atamani kurudi kukuona), mtegemed Mungu yatakwisha.
Goodluck.