Huyu mwanamke ni mzuri kama malaika, halafu mlokole

Huyo hajaokoka mkuu....alookoka deeply angejitenga na wewe kukutafta tafta ..anakulia timing..huenda na yeye kavutiwa na wewe ndo maana lazima akucheki...kila la heri kwenye urafiki wenu

Waliookoka huwa hawavutiwi na watu kimapenzi?
 
Wakati wa kufunga shule nilienda kumchukua kijana wangu shule moja ipo Kahama. Katika kusubiri maelekezo nikaona dada mmoja akiwa amekaa peke yake huku akichezea simu. Moyo ulilipuka sana baada ya macho yetu kugongana.

Nikawa kama nimepigwa shoti ya umeme. Niliona ni kama nimekutana na malaika aliyeshuka toka mbinguni. Nikatamani kumsogelea yule mrembo lakini nikawa na shaka kama niko presentable kwake?

Nikajivuta na kusogea karibu yake. Nikakoki sauti yenye mvuto na kumsalimia kikakamavu. Tukapiga stori mbili tatu za kuisifia shule yetu na hatimaye akanitaka nivute kiti tukae pale kubadilishana mawazo. Akajitambulisha anaitwa M (ufupisho) na anaishi kanda ya ziwa.

M ni mwanamke mzuri wakuu, fikiria naamka muda huu kuandika kuhusu uzuri wake. Licha ya kuvaa mavazi yenye stara, hiyo haikuwa sababu ya kuficha uzuri wa asili mwanadada huyu. Kwa umri wangu mpaka sasa huyu ni mwanamke mzuri zaidi ukilinganisha na wanawake wote duniani. Licha ya usemi unaosema uzuri upo machoni kwa mtu, lakini ukweli utabaki palepale M ni mzuri kiasi cha kusisimua.

Wengi tumekuwa na fikra kuwa pengine Angelina Jolie na Aishwarya Rai, ndiyo wanawake wazuri duniani lakini hapa hawaingii hata nusu. Hiyo
imesababishwa na umaarufu tu walionao walimbwende hao.

Ni mwanamke mrefu kiasi, maji ya kunde wa kung'aa kama kamwagiwa chocolate, ana mguu, ana kifua, ana macho ya kurembua, nyuma kafungasha,kiuno kimekatika. Mbaya zaidi anajiremba, nilimnusa kajipulizia utuli wa kuvutia sana. Nilijiridhisha huyu mwanamke hana kasoro kwa asilimia 90. 10 naziacha kwa viungo vya ndani.

Mara nyingi nilimtazama kwa macho ya kushangaa hata yeye akagundua. Nikataka kumjua zaidi, ananiambia yeye ana mtoto mmoja aliyemfuata pale, ni mwajiriwa lakini pia ameokoka anampenda Yesu. Baadae stori zake zikawa ni shuhuda mbalimbali za mambo ambayo Yesu amemtendea. Hakika nilivutiwa sana na M kiasi cha kuona nimewahi sana kuoa.

M amekuwa rafiki yangu,hakuna siku anaacha kunijulia hali. Nikimpotezea hulazimika kunipigia simu akilalamika kuwa kimya.

Kwa hiyo najiona kama mtu mwenye cheo. Cheo cha rafiki wa mwanamke mzuri kuliko wote duniani. Mzuri wa sura na yupo karibu na Mungu.
Huku kwetu sa mbili na dk 36
 
Back
Top Bottom