Leo nimekereka sana.
Nina familia ya mke na watoto wawili. Kwa sasa, kikazi niko Mbeya, ila familia iko mkoa wa Kilimanjaro. Huyu mke wangu nilimfahamu kwa mara ya kwanza akiwa kwa shemeji yake. Mwaka 2007 tukafunga pingu za maisha. Ila yeye alikuwa form four leaver na hakufanikiwa kuendelea na masomo. Baada ya kufunga ndoa nikamwendeleza kielimu na hata sasa yuko masomoni. Huwa namtembelea walau mara moja kila mwezi na hivi majuzi nimetoka huko.
Nikiwa huko nilipiga picha kadhaa za familia yangu niliporudi nikaiweka facebook. Marafiki zangu wakatoa comments zao kunipongeza kwa familia nzuri, watoto wazuri na mamsap naye kapendeza kweli kweli. Sio kwamba najisifu sana, lakini pamoja na maisha kubana huwa nawapatia kila aina ya mahitaji muhimu, pale anaponiambia kuna shida au kuishiwa hela huwa nafanya juu chini kwa vyovyote vile lazima niwatumie hela. kwa ufupi hajui kuishiwa maana niko radhi nikope hela kuliko mke wangu kuishi maisha ya kubangaiza.
Sasa, kuna binti fulani kwa sasa yuko Kigoma, alikuwa house girl enzi hizo yeye akiwa kwa shemeji yake. Yule binti naye amejiendeleza kimasomo na sasa ni secretary. Naye yuko fb hivyo ni miongoni mwa rafiki zangu fb.
Huyo binti akatoa comment fb kumsifia mke wangu na watoto. Hakuishia hapo, akampigia simu na kumpa hongera zake, si unajua tena mbwembwe, oooh, hongera ma mdogo, naona ba mdogo anakutunza na bla bla nyinginezo. Sasa kasheshe, mrs kanipigia simu anasema eti xxxx amenipigia simu na kunieleza.............. Nikamjibu ndiyo hiyo picha niliweka fb kwa hiyo atakuwa kaiona huko, hata friends wengine nao wamenipongeza mbona?
Akaniambia is there anything between you and her? stay away from that lady, na siyo huyo tuu, be careful na marafiki zako wa kike mtandaoni. Sasa nimejikuta nashangaa kwani kosa langu ni lipi? kuweka picha ya familia fb? akanijibu hapana. Haya, basi niambie mbona huyo binti anakuita mama mdogo, na mimi ananiita ba mdogo, alafu sina mawasiliano naye, kwanza yuko Kigoma, na mimi niko Mbeya, wapi na wapi? Hao marafiki wa kike ni wapi na wamefanya nini? hana majibu.
Kwa ufupi mwenzangu ana wivu wa kupindukia, akiona jina la kike kwenye simu anaanza kuniuliza huyo mtu ni nani, anafanya nini, na yuko wapi. Nikipigiwa simu ikiwa ni sauti ya kike hata mchana wa saa nane ataniuliza huyo ni nani, yuko wapi anafanya kazi gani. Ikiingia message ndo usiseme, maswali kibao, hata kama ni message ya kiofisi. Jamani kwa mwendo huu naona maisha yatanishinda. Nimemwambia ingia fb hataki. Nikamnunulia simu kali yenye internet na madoido mengine, wakati mimi nina nokia tochi na tecno, kuonyesha jinsi ninavyomjali lakini wapi.
Sasa nifanyeje wadau? nimepatwa na hasira.