- Thread starter
- #181
niwe mkweli mimi nilikuwa kama chris wako, nilikuwa muasherati na hata baada ya ndoa nikawa mzinzi sana. hapo ulipo jua kuwa unazini na adhabu yake ni moto wa milele, ukifa sasaivi unaenda motoni moja kwa moja, shida ni kwamba haujui utakufa lini, leo, usiku huu, kesho au lini, umejiandaaje? unabahatisha maisha uishi kwa bahati nasibu kwamba nikiishi basi nisipoishi basi wakati Mungu amekupa uzima ambao ni opportunity ya kupanga na kuchagua?
kuna siku Mungu alinifunulia hicho nilichokiandika hapo juu, nikaogopa sana, nikapiga magoti nikatubu dhambi zangu, nikajiunga na wokovu na kuwa mwokovu hadi kesho na kuendelea, sitaacha wokovu. ndio maana nakuandikieni hata ninyi, sio kwamba nahukumu bali nawashauri muache michezo hiyo. pamoja na dhambi hizo za uasherani, Mungu anakuona, ila ameandaa njia ya wokovu kwa Yesu Kristo, alimwaga Damu ili ukitubu akusamehe uzinzi wake wote, ila kama hautatubu utabaki na dhambi zako na ukifa ni motoni moja kwa moja. mwogope Mungu, Yusufu alisema nimtendeje Mungu dhambi kubwa namna hii? dhambi ya sirini uzinzi ambao hata angefanya asingejulikana ila akajua Mungu anamwona amtendeje Mungu anayemuona kila kitu dhambi ya uzinzi ile? kwanini umsaliti Mungu anayekuona tangu unavua ngua hadi uchafu wote, dharau gani hizo kwa Mungu aliyekukataza usifanye hayo na wewe bado unafanya tena kwa makusudi? tumaini lako ni nini hapo ulipo?
TITO 2:11 inatuaburu kuukataa ubaya natamaa za dunia,na tuach euovu, INASEMA: Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
Amua leo, okoka, ama la hukumu ipo juu yako. UFUNUO 14:13 INASEMA: Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
usidanganywe na mapadre na wachungaji wanaosema ukifa wataiombea maiti yako nayo itasamehewa dhambi. Mungu amekupa nafasi ya kutengeneza mambo yako ungali hai, ukifa ndio deadline yako ya kutubu, hapo juu Biblia inasema ukifa utaenda na matendo yako. sehemu zingine anasema baada ya kufa ni hukumu. baada ya kufa sio kutubu, unatubu vipi sasa wakati maisha yako ya hapa duniani yameisha? na kama nafasi hiyo ingekuwepo Mungu asingesema tusifanye dhambi kwasababu angejua hata tungefanya siku tunakufa ndugu zetu huwa wanahuzunika sana lazima tu wangetutubia dhambi badala yetu. lakini sio hivyo, hata waombe na kufukiza uvumba namna gani huwezi kusamehewa baada ya kifo, nafasi yako ya kutengeneza na Mungu imekoma, matendo yako utaenda nayo, utahukumiwa nayo. hapa ndipo penye hekima na busara ya watakatifu, wewe unayetaka kuwa mtakatifu pambana kuyakimbia makanisa ya aina hiyo yanayofundisha watu kuwa watawazika vizuri kwa kuwaombea, hayo ya katoliki na mengine, ni uongo wa shetani, ndio maana mmeshikwa masikio mnaogopa mapadre na wachungaji kama nini kwasababu mnaogopa nani atawazika, kwani mkiliwa na mamba au simba nani atawazika? mkiungua moto au kupotea na ndege hewani nani atawazika? akili zenu zimeenda wapi ndugu zangu. Mwogopeni Mungu, tubuni mkaiamini Injili ya kweli, nanyi mtapata kipawa cha Roho Mtakatifu awaongoze muishi maisha matakatifu ili mkaurithi uzima wa milele, ama la hukumu ya Mungu ipo juu yenu. Heshima na utukufu kwa Mwanakondoo wa Mungu, Kwa Jina la Yesu!
Nilikuwa huko mkuu walokole wakanitenda sasa sitaki mwanaume wa kujifanya mlokolee nataka mwanaume mcha Mungu

