Huyu mtangazaji wa EATV, hapana kwa kweli!

Huyu mtangazaji wa EATV, hapana kwa kweli!

Status
Not open for further replies.
Leo nilikuwa naperuzi hizi local channel na ghafla macho yangu yakatua kwenye EATV, nikakutana na mjadala ambao ulikuwa ukiongozwa na dogo mmoja, simfahamu jina lakini nadhani yupo mda mrefu sana hapo EATV maana kuna wakati flani hivi nilikuwa naangalia hiki kituo na kumuona huyu dogo akisoma habari!
Kilichonifanya niandike uzi huu, ni muonekano wa huyu mtangazaji, kwa kweli ukimtazama mara moja unatamani kubadili chanel fasta hata kama kinachojadiliwa ni kizuri!
Japo mimi siyo mtaalam sana wa masuala ya utanashati lakini nlivyomuona anahitaji msaada juu ya utanashati maana unapokuwa mtangazaji tena unaongoza kipindi cha zaidi ya nusu saa, inabidi muonekano wako uvutie kuanzia nywele(kichwani), uso pamoja na mavazi!
Sasa huyu dogo, mh nywele zipo rough, hajachana (au angezinyoa kama na kuziweka kwenye muonekano mzuri, hazichaniki vizuri), shati na tai naona kama haviendani kabisa na hata suruali!
4271a7f7c2cd2bb42789a4f07edb959b.jpg

3ca55aabde83f6dfa77cd9e394d50c59.jpg

99773ed813e09989d05d6c8e386c9d81.jpg

My take; Asije akanyoa kiduku...
Ajitahidi kuwa mtanashati!
Tai na jinzi wapi Na wapi?
 
Tuwaoneeni huruma tu hawa wadogo zetu/ wakubwa zetu na ndg zetu. Mazingira nlya hii kazi ni magumu sana kwa baadhi ya vituo, hasa ukiwa huna kitu kingine kinachoweza kukusogeza mbele.
 
Kila mtu ana vile anapenda kuonekana,,, So lyf style ya mtu n ngumu kuijaji,,,, Mf. Me naweza kuwa napenda sana kufuga Nywele bt nachana za pemben juu sichan, navaa jeans na tai juu,,, That's lyf style of somebody,,,

Yeye anaenjoy anavyoapia so worry out abt someone appearance,,,
Kwa hayo uliyosema inategea dress code ya sehemu husika...huwezi kuvaa ulivyosema then ukaenda kufanya kazi ofisi za umma!
 
Yupo poa tu mbona, ulitaka apake Vaseline kwenye lips?
 
Acha wivu we jamaa..yeye kachagua na wewe unataka mchagulia ili iweje?
 
Mwanaume halafu unajali utanashati w mwanaume mwenzio ili akufanyeje sasa

Mambo mengine bhana
Hujui dress code au unajitoa ufahamu? Kavae pensi uende kufanya kazi ofisi za umma, ndio utaelewa nini maana ya utanashati!
 
MZEE MENGI ANA WALIPA HELA NDOGO SANA NDIO MAANA WANAMKIBIA KILA LEO.....
LEO NIMESHANGAA KUMSIKIA MWANAIDI SULEIMAN E-FM...
Hela ya kunyoa hawana
 
Mwanaume kumuangalia mwanaume mwenzako na kujadili uvaaji wake ni ushoga
Sidhani kama content umeielewa...
Ila nafahamu unaelewa nini maana ya dress code na hata muhtasari wa dress code unaufahamu!
 
Hujui dress code au unajitoa ufahamu? Kavae pensi uende kufanya kazi ofisi za umma, ndio utaelewa nini maana ya utanashati!
Huwa napata shida sana kumuelewa mwanaume anayeaigia au kuongelea utanashati wa mwanaume mwenzake
 
Mwanaume kuwa simple inapendeza pia. Akiwa mtanashati saaana pia wengine wangeponda na kusema mshahara wenyewe kiduchu alafu anafukuzana na fashion utadhani demu. Mambo mengine pia hufanyika kwa sababu maalum. Hivi unadhani bosi wake hamwoni?
Siyo kuwa mtanashati kupita kiasi...
Sasa mtu unakaa rafu rafu, hata kama ni umaskini inabidi ufiche umaskini wako wakati mwingine...
 
Analipwa shilingi ngapi,tuanzie hapo.
Wakati huu wa ugumu wa ajira,
kama anajitolea,na muda wote
anapambana na kupata nauli
na pesa ya kula wakati anasubiri ajira tutajuaje?
Nashawishika kusema,jambo hili tumuachie yeye na mwajiri wake.
au msemo rahisi ni huu "ya ngoswe mwachie ngoswe"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom