Huyu msichana nataka tu hela zake yeye simpendi

Huyu msichana nataka tu hela zake yeye simpendi

jean phillipe beyun

Senior Member
Joined
May 18, 2015
Posts
142
Reaction score
167
Kuna huyu mwanamke aliyeniomba tuishi wote baadae tukatofautiana kwenye kuchangia hela ya pango hivyo nikahama kurudi kwangu kwenye gharama ndogo

Baada ya kuondoka kwake nikampotezea nikawa simjibu sms wala kupokea simu zake, akawa anahaha kunitafuta, nikastukia ameibukia kazini kwangu, akadai tukaongee pembeni, nikasema nakusikiliza

Akasema amepata hela kiasi flani twende tukanunue vifaa na material tumalizie nyumba yangu ambayo nimeifikisha kwenye linta, na hela zingine anategemea mkopo wake utatoka anytime, then nyumba ikiisha tuamie tuishi wote , kwamba ameshindwa kukaa mwenyewe

Wadau huyu mwanamke kiukweli simpendi isipokua ana vijisenti na amekua akiniwezesha sana napokwama, tangu nimekuwepo nae kidogo mshahara wangu unapumua

Ingawa sina demu mwingine permanent ila huyu sijamkubali kutokana na sababu zifuatazo:-

(1) huduma yake kitandani haijakidhi viwango nilivyozoea

(2) kitendo cha kuwa na watoto wawili kinanikatisha tamaa
Hasa kutokana na shuhuda mbalimbali kutoka kwa waliooa wenye watoto humu jf

(3 ) ana mzigo mkubwa wa dependants, watoto, wadogo zake, nilivyomsoma hataki kuwa mbali nao

(4 ) sina mapenzi ya dhati kwake, infact wakati fulani dhamira huwa inanishitaki na hivyo nafikia uamuzi wa kujitoa, lakini yeye husikitika sana na kutumia njia zote ili tuendelee, wakati mwingine akiona nafanya hivyo anaweza kunirushia hela kwa sim basi najikuta naona aibu najirudi

Madai yake ni kuwa anahitaji tu settle down, tufunge ndoa, tuishi pamoja for better for worse

Guys is this a right woman for me?

Can I risk and settle down with her?

Or should I give it more time for this relationship to work?

Or should I find another chick and dump this one for good?

Your help pls
 
hahahahajajahaaaa yaaan ww huwaga unanichekesha sana.

ngoja aje miss chagga.
 
Hayo ni mambo ambayo unapaswa kuamua wewe mwenyewe,na kama hakufai bora uachane nae na usiendelee kula hela yake,kumbuka what goes around comes around,iko siku utapata mjanja wako kwani naona unatafuta laana.
 
jean kwan yey huwa haingii humu jf??unajiharbia dili mwanangu akiona hutaramba hata mia
 
Hayupo JF? Au ndo unamfikishia ujumbe this way
 
Wadau huyu mwanamke kiukweli simpendi isipokua ana vijisenti na amekua akiniwezesha sana napokwama, tangu nimekuwepo nae kidogo mshahara wangu unapumua
i-21.jpg
 
Jifanye unajua kula vya watu, sisi ni waafrika na tuna mila desturi bila kusahau "technolojia" yetu. Yakikuta usije sema hatukukuonya.

Nyie ndio baadae hujifanya kukimbilia kuokoka mkitoa shuhuda.
 
Jifanye unajua kula vya watu, sisi ni waafrika na tuna mila desturi bila kusahau "technolojia" yetu. Yakikuta usije sema hatukukuonya.

Nyie ndio baadae hujifanya kukimbilia kuokoka mkitoa shuhuda.

ha ha ha ha duuh
 
Mmh hayo maswali yote n ya kujibu sisi kwel mbna unatuonea! Haya maswal nafsi yako ndio inatakiwa ifanye maamuzi sahihi ucje ukatafuta wa kumtupia lawama baadae
 
Wewe mwanaume una matatizo sana mmh umenichosha

Tafuta kwa jasho lake na umwache dada wa watu kama humpendi loooh
 
Ujinga kama huu najuta kuufungua unalala nae anakusaidia unataka wa kumsaidia ww sawa niwekee no yake pm ili nimsaidie akuache
 
Inasikitisha Sana.. Kaka Kwanini Unamfanyia hvyo huyo Dada? Kwanini Ule Hela zake na yeye ana Mahitaji Mengi kiuhalisia kuliko wewe? Ni Dhambi kubwa. hapo Unapanda Laana juu ya Maisha yako kama ulkua hujui kama hutaiona Leo ujue inakusubiri kesho. Tubu kwanza kwa dhambi hii.. Then Kama Umegundua Humpendi why don't U seat down with Her Utumie lugha ya Hekima na Busara Umueleze Ukweli kutoka Moyoni Mwako kuwa Hamuwez kuwa pamoja? Anaweza akawa ni Mwanamke sahihi sawa lakini wewe umekuanae Muda wote huo umeshindwa kumpenda unategemea ujipe Muda tena ukitegemea muujiza gani utokee afu Ujikute unampenda kama mwanzo ulishindwa? Si vyema Kumpotezea Muda na Pesa. Muweke wazi kama ni fedha zake Mshauri Azihifadhi kwaajili ya kesho ya watoto wake. (Always truth set Us free) ni Bora Ukamuumiza kwa Ukweli kwa faida yake yeye kuliko kum'bembeleza kwa Uongo hii haitamsaidia. Be A Gentleman
 
Back
Top Bottom