Huyu mdudu anaitwaje?

Huyu mdudu anaitwaje?

Huyo mdudu akikuuma kadri anavyo tembea ndivyo sumu inasambaa mwilini
Huo ni uongo stories za wahenga. Nimeshanga'twa zaidi ya Mara 3 na huyo mdudu. Mara moja alifanikiwa kukimbia baada ya kuning'ata.
 
huyo ni mende pori...no, ni tandu, mpuuzi tu kwetu akikuuma unajikata ulipoumwa, unamchoma jivu lake unajipa kesi imeisha
 
Siku moja nilikuwa nimekaa barazani huyu mdudu alikuja kuingia ndani ya suruali sikujua kabisa, mara hafla nikahisi kitu kinantembea, nikajua visusumizi tu, nikabofya kwa nguvu ili kujikuna kidogo. mara [red]hafala nahisi mtembeo kwenye paja yuwaja juu, sikujali tena nlivua suruali nijui nini kumbe tandu...
Sheikh Zanziberi kwema?

 
Siku moja nilikuwa nimekaa barazani huyu mdudu alikuja kuingia ndani ya suruali sikujua kabisa, mara hafla nikahisi kitu kinantembea, nikajua visusumizi tu, nikabofya kwa nguvu ili kujikuna kidogo. mara hafala nahisi mtembeo kwenye paja yuwaja juu, sikujali tena nlivua suruali nijui nini kumbe tandu...
Hata jamaa yangu aliingiliwa na huyu mdudu kwenye suruali lakini bila ya kujua kama ni Tandu alivua suruali na kumtoa bila ya kuumwa,nadhani inapofikia kukuuma ni lazima utakuwa umembana au umemkanyaga,tofauti na Nge..
 
Huyo Ni tandu anauma na ana sumu Kali tu japo haiui. Akikuuma kama leo sa10 utabaki na maumivu makali mpaka kesho mda kama huo ndio unapata nafuu
 
Mtoto wangu ali umwa na huyo mdudu kisha kambeba kaja nae hahaha ilikua shughuli maana alikua bado hajaanza kuongea vzr baada ya mda kidogo joto lake la mwili lilipanda sana kiasi tuliingiwa uoga sana, shida ikawa hosp za kiTz hawajui dharula kabisa ya mtu anae umwa magonjwa ya kawaida na alie umwa na mdudu ama kupata ajali wakataka tukae foleni tuliyo ikuta na foleni kwenye hosp za watoto zilivyo mh! Mtoto hali ili change kabsaaa sikuamini kama mdudu huyo akiamua kufanya yake anaweza kubadili hali ya hewa, mwisho alipata matibabu na hata ivyo tuliambiwa anabahati alie mng'ata alikua mdogo hivyo sumu si kubwa sana mana alikua kama ana rangi ya kijani kidogo, kwa madai ya dr anasema wale wekundu na wengine wanakua kama wana mbawa mbili mwishoni mwa mikia yao ndio noma zaidi
Kwa kifupi sio mdudu rafiki sana huyo kama nnge
Pole sana
 
Hata jamaa yangu aliingiliwa na huyu mdudu kwenye suruali lakini bila ya kujua kama ni Tandu alivua suruali na kumtoa bila ya kuumwa,nadhani inapofikia kukuuma ni lazima utakuwa umembana au umemkanyaga,tofauti na Nge..
Yah nahisi ni kweli, kama umekaa umetulia ivi hakuumi ata kama anatembea kwenye mwili hata kama utamuondosha kwa mkono na akawa bado yupo katika mwili haumi, huyu nahisi anauma pale unapombonyeza kwa nguvu kiasi cha kuhatarisha uhai wake ndio ana respond. Nilishukuru mana nlikuwa na waza sijui kama ningekufa siku hio 😀 😀 😀
 
Habari wakuu,

Hapa nnapo ishi nimekutana na hawa wadudu mmoja ni mkubwa balaa na mwingine ni mdogo kama huyu, sasa nauliza hawa wadudu wanaitwaje je wanauma na akikuuma dawa yake ni nini na njia ya kuwazuia ni ipi.Nimewakuta wawili wapo karibu na shimo la maji machafu wanakula mende.

View attachment 696000
Tandu Huyo, Kuna species nyingi sana, baadhi ya specie wana sumu Kali sana kiasi akikung'ata ukachelewa kupata matibabu Unaweza ku-paralyse mwili
 
Back
Top Bottom