Endelea tu kuwagawa Watanzania misingi ya Vyama, mfumo wa vyama vingi ulianzishwa kwa malengo mazuri tu kama kioo cha Serikali iliyopo madarakani kujipima kama inafanya vizuri. Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alikuwa na uwezo wa kukatalia mbali mfumo wa vyama vingi, lakini kwa busara zake akashauri mfumo huo uwepo ili wale wenye mawazo tofauti na Chama Tawala, wapata sehemu ya kusemea. Lakini kwa akili ndogo ya watu kama wewe, wanafikiri kuna makosa yalifanyika kuanzisha mfumo huo. Nina hakika watu kawa wewe mkimaliza kuwagawa kwa msingi huo, mtaanza kujigawa ndani ya vyama vyenu kwa kuangalia undugu.
Ni kweli mkuu, hawa watu mashabiki wa vyama vya siasa, hususani CCM, na CHADEMA, ni kero.
Jambo lisilo la kisiasa, wenyewe huingiza siasa.
Hata pale mada ambayo ingewapa watu Elimu, huaribiwa na UCCM, na CHADEMA.
Watu wanawaza vyama, kuliko watoto wao, na wazazi wao.
Hii forums, ina majukwaa mengi, na kila jukwaa lina mambo yake, sasa tupo jukwa la Sayansi, tunajadili labda, aina za simu, na ubora wake, mtu unaingiza siasa.
Siasa ipo, lakini maisha lazima yaendelee, Na unaepinga nae kwenye siasa kwenye mada ya Dini, mnakuwa upande mmoja.
Ama unaepingana nae kwenye Dini, mnakuwa upande mmoja kwenye michozo, hivyo ndivyo inavyotakiwa.