Huyu jamaa ana roho mbaya Iseee!

Huyu jamaa ana roho mbaya Iseee!

Et Leejay49 ukienda eneo kama hili kupata mlo halafu atokee mtu wa aina hii, hivi kesho utakuwa na hamu ya kurudi hapo kula?
Nilivyo nakinyaa kwanza mtu tu akiwa ananiangalia angalia usoni nasusa kula sembuse huyo kunisogelea namna hiyo,.

Kuna siku cafe sikuwalipa hela kisa mmama mmoja chizi ameingia wahudumu wanamwangalia tu akaja na mikono yake bila kunawa akachukua nyama kwenye sahani yangu wanamchekea chekea tu nilinyanyuka nikaondoka zangu bila kusema kitu nao nadhani walijua kwanini wala hawakuniulizia bili
 
Nakumbuka siku moja nipo kinondoni manyanya kuna mgahawa nakula akaja teja anataka buku nikamwambia sina akaanza maneno ya shombo.. kwa hiyo unakula biriani na juice hutaki kunipa buku

Nikamwita mhudumu (mdada) hebu niondolee huyu mtu sitaki usumbufu tofauti na hapo nitaondoka na silipi maana mnalea ujinga kwenye mgahawa wenu

yule mdada alienda kumwita mpishi (jamaa) akaja akamtoa lkn jamaa anatolewa huku aninitamkia maneno ya hovyo.

Kiufupi huu ni usumbufu wakati nakula sitaki vurugu, kwa nini ukose ustaharabu nimalize kula ndio uniambie.
Haipendezi hata kidogo . Sio tu mgahawani hata kuna pub moja jirani hapa ni maarufu kidogo,sasa humo ndani kuna muda mateja na vichaa wanaingia kuombaomba hela na kuleta kero kwa wateja wamekaa kiustaarabu wanapata vinywaji vyao ofcourse inanikera japo sio mimi ila inaboa sana najaribu kuvaa viatu vyao nashindwa.. na hii sometimes inaweza hatarisha maisha ya wateja.. maana watu wa sampuli hii wanakuwa na mambo mengi muda mwingine anatafuta mtu wa kufa nae
 
Hahahaha uyo maza jau sana
Ni omba omba hao au?

Mtoa mada asihukumu watu kwa snap za picha bhana!

Alitakiwa aje na stori unganifu inayoeleza kisa kamili kumhusu jamaa.

Je huyo ni mkewe na huyo ni mwanaye?

Haelewi madhara ya kugawa kwa mtu chakula unachokula?

Yaani kama ni omba omba wamemvamia kwenye mgahawa, kosa si la kwake huyo mteja bali ni la utawala wa Canteen.

Ndiyo maana biashara nyingi hujifia vifo vya kawaida kutokana na ukosefu pamoja na management mbovu.
 
Back
Top Bottom