Huyu HR/Receptionist kimeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu HR/Receptionist kimeo

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Maundumula, Aug 18, 2012.

 1. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hii imenikuta jana, natoka zangu job jioni nikasema nipitie dukani nikanunue mahitaji mawili matatu. Nimeshanunua nakaribia mlangoni simu inaita , naangalia naona namba land line siijui.Nikapokea na mazungumzo yangu na Caller yakawa hivi.

  Caller: Hallooo (Sauti ya mwanamke wa makamu kiasi atleast 40 years of age)
  Maundumula: Halloo habari

  Caller: Wewe ndio unaitwa Maundumula (sauti ya ukali)
  Maundumula: (Anasita kidogo kwakuwa anayepiga simu hajajitambulisha na tone yake inaonesha yupo impatient)

  Caller: Au sio wewe mimi nikate simu
  Maundumula: Ndio mimi , nazungumza na nani?

  Caller: Mbona unanijibu kwa ukali, nitakata simu mimi, nakupigia kwa faida yako mwenywe
  Maundumula: (Confused, anabaki kimya)

  Caller: Uliomba kazi ya ...... au hukuomba nikate simu?
  Maundumula: Unapiga simu kutoka wapi?

  Caller: Nina watu wengine wa kuwapigia na wewe unanipotezea muda, au nikate simu??
  Maundumula. Mama, mbona unakuwa mkali hivyo , au ndio unanipigia ushahidi tu wakati mna watu wenu mmeshawaahidi kazi?

  Caller: Huoo usemi ndio ufute kabisa yaani uufute kabisaaa huo wa kusema tuna watu wetu tungekuwa na watu wetu tusingekupigia blah blah blah (Amehamaki temper is at max, breathing heavily) , au unataka nikate simu eeeeh
  Maundumula: Bora ukate tu mama maana naona hatutaelewana
  Caller: Tiii tiii (Hang up)

  Ushauri wangu: Hizi kazi za mawasiliano ni vyema wawe wanapewa watu ambao wamesomea na communication skills japo kidogo. Huwezi kupiga simu hujajitambulisha wewe nani na unapiga kutoka wapi halafu on top unajifanya una haraka wakati hiyo mojawapo ya kazi yako.

  Ni aibu kwa taasisi kubwa kama hii kutokuwa na mtu competent wa kuweza kupiga simu akaongea kwa kueleweka tena kwenye lugha ya nyumbani. Nadhani next time watu kama hawa wakikupigia wao wakiongea Kiswahili dawa yao kuwajibu kwa kizungu . Kizungu huwafanya watanzania waende kwenye point moja kwa moja :happy:.
   
 2. NAFIKA

  NAFIKA Senior Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wengi wao huhisiwanamiliki hizo ofisi, customer care ni problem kwa Watz wengi.
   
 3. C

  CLEMENCY JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Pole sana kaka. Cstomer service Tanzania mbona ilishakufa zamani sana? Halafu wakenya wakiajiriwa tunakuwa wakali
   
 4. ummu kulthum

  ummu kulthum JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 2,791
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  yaani sijui nani ametuloga...........
   
 5. mito

  mito JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,613
  Likes Received: 1,992
  Trophy Points: 280
  pole mkuu, ila nimecheka sana hayo majibu ya huyo mama, loh!
   
 6. Bandabichi

  Bandabichi JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ilinitokea mwaka 2009 ndo namaliza chuo. Alikuwa ni Zone manager NMB-Southern Zone wa wakati huo sijui kama kabadilishwa na ilikuwa Jumapili. kuuliza naongea nani akawa mkali.

  Nikamwambia kupigiwa na landline inamaana kuwa naongea na taasisi na sio mtu binafsi. Alinijibu hovyo na kukata simu.
   
 7. Baba Watoto

  Baba Watoto JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 218
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Kaka pole sana, customer care TZ iko nyuma, lakini matatizo yapo kwa mfumo wa ufundishwaji wenyewe kabisa. Anyways lakini ss hv tunataka fanya integration ya NLP wakati wa kuwafundisha hawa watu, ila wawe fresh maana kumfundisha mtu anayekwambia 'sisi tumezoeaga hivi..' ni hatari zaidi
   
 8. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ha ha ha....pole mkuu....huo mkwara wa "au nikate simu" umenifurahisha. alilazimishwa kukupigia labda huenda ulionekana wewe ndio mwenye sifa na uzoefu. yeye alishaweka mtu wake pending......:eek2:
   
 9. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,834
  Likes Received: 2,771
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red Mkuu! Kwani lini ilikuwapo? Wa-TZ sisi ni mzigo kwenye Jumuiya ya A/M. Ni bora kazi zote wachukue tu hawa wa-Kenya. Mpaka hata Serikalini waajiri tu wa-Kenya sisi hatuna maana tumb..f zetu!

  Hivi kuna vyuo vinavyofundisha masuala ya huduma kwa wateja hapa kwetu? Kenya kwenye vyuo vya aina hiyo kama utitiri ndo maana yanajua sana maswala ya Huduma kwa wateja. Yaani ukienda kwenye hata kwenye hitel palipo na M-Kenya tegemea huduma ya kufa mtu, kabla hujakaa umeshaulizwa huduma unayohitaji.
   
 10. b

  bdo JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  mmh, tupatie hio namba ya landline ili tuwape ukweli, maana kama kazi ushakosa..
   
 11. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Why don' we think it in a positive way?! Wht if lengo lake ni kuona "how you can handle difficult customers?" Niaje kama nilitaka kuona "how u can work under pressure?" Wht if i meant to knw how you can manage ur calls?!
   
 12. Catherine

  Catherine JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  i was thinking the same, hapo kuwork under pressure panahusu sana. kama ndio ilikuwa interview yenyewe hapo kashafeli.
   
 13. Chambo81

  Chambo81 JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 19, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu nashindwa kuamini kama hii imetokea seriously....nimecheka kinoma nahisi kama komed flani hivi natamano nomwone huyo bi. mkubwa...pole sanaaa!!!!
   
 14. bombu

  bombu JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,134
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  was that supposed to be part of an interview au ndo kusema kampuni zenu zachuja watu kwa njia hiyo? Even if it was part of an interview an interviewer had a call of introducing her/himself . After all working under pressure haimaanishi hiyo condition but kufanya kazi under limited time Coz PRESSURE= WORK/TIME.

  I think hawa customer care epmloyees, huwa wana wivu pia na vyeo vya wenzao teh, so kuwapigia watu ili wapate kazi zenye mazlahi kuliko ya kwao huwaumiza vijiroho vyao.

  Ndo maana mie huwa nawaambia watu, why take a job you don't Love and feel in heart? You have to love the job before you accept it.
   
 15. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Naweee, unaleta mambo ya fizikia za sekondari ndani ya jukwaa la GTs?! .....hapo si mahala pake!! Anyway, tuache hilo, but nilichosema ni why don' we think it in a positive way...na ndio maana nikatanguliza "handling difficult customers!" Hivi we unawafahamu difficult customers au unasema tu?! Let's say u're service provider; umesham boa sana mteja wako with ur unsatisfactory service to him/her....then, unatarajia huyo m2 akupigie simu na kuanza kuji-introduce kwamba am mr. so and so ?!?!?! u can not be serious chuck!! Alichofanya huyo mdada ndiyo haswaaa kinachofanywa na hao difficult customers....nd in fact, wanaenda mbali zaidi ya hapo!!!

  Likewise, hata kama sisemi kwamba hiyo ilikuwa ndiyo interview yenyewe(remember wht i said, i.e. let's think it in +ve way), lakini kwa wengine (orgs zingine) interview is just a process....ni mchakato!! organisations za aina hiyo interview ni b4 hujafika hata hapo kwenye interview panel...u got it chuck?! they can even watch u wht du do after leaving the wash room.....do you clean ur hands?! ur tendency after leaving the wash room explain a lot abt u!!!! One may ask, suala la kusafisha mikono after leaving the wash room lina uhusiano gani kwenye interview!!! Do you think a person who can not even clean his/her hands after leaving the wash room anaweza kuwa perfect match 2 work with business executives?! The answer is absolutely NOT! Others even watch u the way u open and close the door in the interview room!

  Now let's go back to hiyo theory ya ku-work under pressure......don' tell me kama unachofahamu suala la ku-work under pressure linaishia hapo hapo ulipoelezea ww kwa ku-work under limited time hadi ukafikia kutoa hiyo P=W/T!!!! YES, u've limited time and u need to complete the task at ur desk within the given time no matter wht!!! Bad enough, wakati upo completely constrained na time; people above you they don wanna hear anything but the job 2b done efficiently....na katika situation kama hiyo unaposhindwa ku-handle the situation unaweza hata kugombana na wakubwa zako kwani si ajabu kila dakika ukawa unapigiwa kama si kuingiliwa ofisini "as 2 why the job is not yet done!" Hawa watu lazima wakushinikize coz' na wao huko wanakumbana na similar situation! May be the board of directors wanamshinikiza CEO wako apeleke report as soon as possible......si ajabu board yenyewe nayo inaghasiwa na owners of the company.....u need to calm down to work under these situation! So, though theoretically ku-work under pressure ni ku-work under limited time, but practically is how u can handle external forces while working under tht limited time nd make sure ur job is done effectively nd efficiently within tht time! if u can not handle such situation, ur work may be poorly completed!
   
 16. i

  i wish Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  NasDaz wat if i applied for more than one company with the same service?does asking who r u o whr r calling from a suicide?
   
 17. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hilo neno "nikate simu"limefanya nicheke sana,pole sana
   
 18. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  pole sana...kweli wanaiharibu professional yao. mtu anaongea kama anakusuta!
   
 19. KANCHI

  KANCHI JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 3, 2011
  Messages: 1,547
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hili suala halihitaji kusomea wala, ni busara inahitajika hapo!
   
 20. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Hayo maongezi yamenikumbusha siku nimepigiwa na watu wa sijui mnaiita Taesa(sina uhakika na jina)...
  Yule dada sijui alikua ametoka kukatwa mshahara sasa alikua anatafuta mahali pa kupunguzia stress....
  Eti ile kumuuliza tu "nani mwenzangu", basi likawa kosa, jibu lililotoka hapo naliweka kapuni...
  Nilivyoona simuelewi elewi nikakata zangu simu...
   
Loading...