Huyu dada huyu jamani lol!!

Sidhani labda ni mtazamo wangu tu wa kizamani....lakini vijana wanaojiunga JF hivi karibuni wanataka kubadilisha muonekano wa JF...kutoka kuwa Home of great thinker.....mpaka kuwa mtandao unaohamasisha ngono.....,

Kumekuwa na mlipuko mkubwa wa picha zisizo na maadili kwenye mtandao huu.....kana kwamba watu wanaperuzi mitandao ya ngono........

Hii si dalili nzuri kama hili jambo halitakemewa mapema.....inaweza ikafikia kipindi mtu anaweza akajirekodi yeye na mpenzi wake wakifanya ngono na kutupia huku.....

Maadili yanaporomoka kwa kasi sana hapa JF.....na bado mods wamelala usingizi wa pono......sijui kuwa na wao wanafurahi picha hizo au la......

Ombi langu ni kuwa kama mods wameshabadilisha maudhui ya mtandao huu watuambie....ili sisi wengine tujipime kuwa tunastahili kuendelea kuwepo hapa na kuutazama uchafu huu......

Au la basi mods wafanye kazi yao ipasavyo....maana naamini kabisa wanaweza wakalizuia hilo......

Hizi picha ni za kidhalilishaji na kufedhehesha hasa kwa dada zetu...mabinti zetu....na majirani zetu......

Hatua zichukuliwe ipassavyo....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…