Huyu dada ameelemewa, anaomba ushauri

Huyu dada ameelemewa, anaomba ushauri

Mtoto mwenyewe hana hatia lkn yule mwanaume kwa akil zake anaweza kuua kwel kwa njia ya kiganga maana hana huruma kabisa
 
Sasa ninavoandika hivi huyo bwana alipiga tena simu kwa baba yake huyu dada akamwambia huyo mtoto ni mal yangu sasa nyie mmeamua kunizurumu hata jina la mtt nilitaka aitwe jina la mama yangu nyie hamja mpa nitaakikisha tunamkosa wote huyo mtoto hata nikimaliza waganga wote tz lkn had nitaakikisha kitoto hicho kinaondoka duniani.

Sasa anaitaji ushauri afanyeje kwa mwanaume huyu nyie wanawake mliozaa mtajisikiaje kama ungekuwa ww nawasilisha jaman....

Tafuta wanasheria na mtengeneze mazingira ya kupata ushahidi upya wa vitisho kama hapo juu...

Kutoa vitisho vya kuua au kumaliza uhai wa mtu ni kosa la jinai na mtu atoaye vitisho vya namna hii huhukumiwa na jamhuri...

Kwa upande mwingine hakikisha kuwa huyo dadayo haachi kusali maana pasipo ulinzi wa Mungu ni bure tu...
 
Habari zenu jamani, kuna dada yangu mmoja alikuwa na mpenzi wake miaka miwil iliyopita. Mapenzi yao yalidumu lakini ilifikia sehemu wakaanza kukosana kosana kwasababu dada alishindwa kumvumilia yule mwanaume kwa tabia yake ya kunywa sana hadi kupitiliza dada akaamua aachane nae.

Lakini walipoachana ndani ya wiki mbili dada akahisi ana ujauzito kaenda kupima kweli akakuta anaujauzito, akaomba ushauri kwa ndugu na marafiki wengi wao wakamshauir amwambie baba wa mtoto japo hawapo kwenye mahusiano tena.

Dada kaamua kumtafuta na akamueleza kwamba nina mimba yako yule mwanaume alikataa kama hamjui alikataa mimba na akamwambia usinitafute tena kwa huo upuuzi wako.

Dada huyu alivumilia kwa vile alikuwa na kazi yake alilea mimba yake vizuri akisaidiana na ndugu zake mpaka akajifungua salama mtoto mzuri wa kike.

Sasa tatizo ni kwamba mtoto amekuwa hadi sa hivi ana miaka miwili, ndiyo yule mwanaume katafuta namba na kaanza kumtafuta tena huyu dada yangu na wakati kipindi cha nyuma hajawahi kupiga simu hata mara moja.

Amebembeleza dada hataki kumuonyesha mtoto hadi alimtafuta baba wa huyu dada na kuomba msamaha sana watu wakamshahuri aje kumuona angalau mtoto yule bwana karuhusiwa kumuona mtoto baada ya kuomba msamaha sana.

Sasa siku moja akampigia simu akamwambia dada yangu nakuja kesho. Kesho ilipofika hasubui na mapema kampigia dada simu na kuanza kumtukana eti huyo mtoto nimewapa kama zawadi kwanza huyo mtoto hamkumpa jina la mama yangu sidhani kama ni mwanangu ilikuwa pigo jingine tena kwa dada yangu.

Sasa ninavoandika hivi huyo bwana alipiga tena simu kwa baba yake huyu dada akamwambia huyo mtoto ni mal yangu sasa nyie mmeamua kunizurumu hata jina la mtt nilitaka aitwe jina la mama yangu nyie hamja mpa nitaakikisha tunamkosa wote huyo mtoto hata nikimaliza waganga wote tz lkn had nitaakikisha kitoto hicho kinaondoka duniani.


Sasa anaitaji ushauri afanyeje kwa mwanaume huyu nyie wanawake mliozaa mtajisikiaje kama ungekuwa ww nawasilisha jaman....

jina kitu gan bana,tabia ya kurithisha watoto majna siipendi,ndo ile mtoto anafata tabia za ajabu za huyo mtu.kama alitaka mtoto apewe jna la mama yake alishndwaje kulea mimba,aache ujinga,watu kama hawa adhabu yao kukatwa vidudu vyao wanakera sana,pumbaaaaaavu.
 
Asome hesabu 23:23 alafu ayakabidhi maisha yake kwa mungu. Hakuna uchawi wala uganga kwao wanao mtegemea Mungu
 
yani mpaka leo anjampeleka ustawi wa jamii anasubiri nini? kuna wanawake wapole aisee .......sasa huyo dada asimjibu chochote ila tu akimpigia simu au kutuma sms ya vitisho mpeleke mashtaka sehemu husika acheni kulea lea wanaume wapuuzi wasiojitambua..... mwanaume ni kujielewa kama alikuwa mlevi kupindukia ni tatizo pia.... jamaaa anawasiwasi wa kuzaa kwa sababu lilevi sasa hapo kabahatisha anataka kulalia nyambafu kabisa
 
Ingekua mm ningetulia tulii akipiga cmu napokea nasikiliza porojo zake wala cmjibu hata atukane wala cmjibu Kwa matusi namwambia tu nimesikia.naendelea kumtunza mwanangu tu Basi.Huyo kweli ni mlevi dada alikua right kuachana nae.mwambie alee mwanae aachane na Hiyo mikwara ya huyo mlevi.
 
Mbona jambo dogo mno?? MUNGU ndo aliyempatia na MUNGU huyo huyo ndo atamlinda, mwambie amtumainie yeye tu.
 
Kwanza mtoto ni mali ya wazazi wawili hivyo mnapaswa kumuonesha mtoto pia kwani hata yeye ni mzazi japo tatizo lake hajitambui lkn sio kigezo cha kumnyima haki yake kama baba wa mtoto eti kisa ni mlevi kwani hata msipo fanya hivyo badae huyo mtoto akikua atawalazimisha mumtafute au atamtafuta yeye mwenyewe japo baba yake nimlevi na kuhusu vitisho ni hasira tu lkn mkae mkijua dam ya mtu haipotei hata siku moja baba ni baba hata kama ni kichaa mpeni haki yake msitumie ubabe hiyo ni dam yake bwana pia mumsamehe kwa kuto jitambua
 
Kwel jaman jambo la msing nitamshahuri dada yangu aende ustawi wa jamii lakin pia bado hatujawa na ushahid wa kutosha kwa maana anapiga simu tu bila kutuma sms na anatumia namba tofaut tofaut jambo lingne ni kuomba sana na kumuachia mungu kila kitu nawapenda sana ndugu zangu kwa ushaur wenu mzur
 
huyo mwanamme kichaa

Mwanamke ndiyo kichaa,unamuacha mwanamme sababu anakunywa sana?Basi wengine tungekuwa tumeisha achwa na wake zetu!!

Kama nakunywa sana nipepele kwa wataalam nipunguze sio kuniacha
 
mi nasema hv atakaecheza na vipenzi vyangu(wanangu)
aisee ntakomaa nae hata kwa kumaliza pesa zangu zote
anavyouma mtotoooo...!!!!jamani
siujui uchawi ila ndo ntautafta
 
Back
Top Bottom