Huyu dada ameelemewa, anaomba ushauri

eti alimwacha sababu anakunywa sana? mshauri huyo dada ampatie jina kama baba wa mtoto anavyotaka
 
Hivyo vitisho alivyo vitoa huyo mlevi ni hatari sana.Kwanza nashangaa inakuaje mpaka hivi sasa hamjaenda kuripoti hivyo vitisho aisee.Katishia maisha na ushahidi mnao,nendeni polisi mtoe taarifa haraka sana
 
Vitisho vya mlevi dhidi ya A.t.m machine ilomeza kadi baada ya kukosea password baada ya kuiomba japo imhurumie apate japo pesa,dada akomae na msimamo kama wa A.t.m kutotoa hela hata kama mtoto damu ya jamaa asikwazike kabisa hata agange agangue kwa sangoma wote mtoto atalindwa na nguvu za mungu as long as alimkataa mwanzo,kaomba msamaha sasa anataka kuja na jipya
 
Maneno ya mkosaji hayo......malaika huyo amemkosea nini wakati alipewa nafasi akaikataa.....Mungu ni mwema atamlinda huyo malaika kama alivyomlina mwanzo.....
 
Jamani asanteni kwa ushaur mungu ni mkuu atamlinda tu yule mtoto badala ya kufa mtt atakufa yeye
 
Habari zenu jamani, kuna dada yangu mmoja alikuwa na mpenzi wake miaka miwil iliyopita. Mapenzi yao yalidumu lakini ilifikia sehemu wakaanza kukosana kosana kwasababu dada alishindwa kumvumilia yule mwanaume kwa tabia yake ya kunywa sana hadi kupitiliza dada akaamua aachane nae.

Lakini walipoachana ndani ya wiki mbili dada akahisi ana ujauzito kaenda kupima kweli akakuta anaujauzito, akaomba ushauri kwa ndugu na marafiki wengi wao wakamshauir amwambie baba wa mtoto japo hawapo kwenye mahusiano tena.

Dada kaamua kumtafuta na akamueleza kwamba nina mimba yako yule mwanaume alikataa kama hamjui alikataa mimba na akamwambia usinitafute tena kwa huo upuuzi wako.

Dada huyu alivumilia kwa vile alikuwa na kazi yake alilea mimba yake vizuri akisaidiana na ndugu zake mpaka akajifungua salama mtoto mzuri wa kike.

Sasa tatizo ni kwamba mtoto amekuwa hadi sa hivi ana miaka miwili, ndiyo yule mwanaume katafuta namba na kaanza kumtafuta tena huyu dada yangu na wakati kipindi cha nyuma hajawahi kupiga simu hata mara moja.

Amebembeleza dada hataki kumuonyesha mtoto hadi alimtafuta baba wa huyu dada na kuomba msamaha sana watu wakamshahuri aje kumuona angalau mtoto yule bwana karuhusiwa kumuona mtoto baada ya kuomba msamaha sana.

Sasa siku moja akampigia simu akamwambia dada yangu nakuja kesho. Kesho ilipofika hasubui na mapema kampigia dada simu na kuanza kumtukana eti huyo mtoto nimewapa kama zawadi kwanza huyo mtoto hamkumpa jina la mama yangu sidhani kama ni mwanangu ilikuwa pigo jingine tena kwa dada yangu.

Sasa ninavoandika hivi huyo bwana alipiga tena simu kwa baba yake huyu dada akamwambia huyo mtoto ni mal yangu sasa nyie mmeamua kunizurumu hata jina la mtt nilitaka aitwe jina la mama yangu nyie hamja mpa nitaakikisha tunamkosa wote huyo mtoto hata nikimaliza waganga wote tz lkn had nitaakikisha kitoto hicho kinaondoka duniani.

Sasa anaitaji ushauri afanyeje kwa mwanaume huyu nyie wanawake mliozaa mtajisikiaje kama ungekuwa ww nawasilisha jaman....

katika wanaume wapumbavu na wasio jielewa huyu jamaa yumo
familia ya mwanamke imekuwa wastarabu sana kumsamehe na kumruhusu kumwona mtoto
sasa hapo si anatishia kuua?
mkabidhini mtoto kwa Mungu ni mikono salama hiyo

jamaa akiendlea kuleta vitosho na kuwanyima aman lifungulieni kesi tu
 
mipombe inamsumbua huyo mwanaume! kwa kuwa mtoto hajapewa jina la mama yake ndo aamue kumuua mtoto?wakati wa kuzaliwa mtoto si alikata mguu hakujihusisha?so alitegemea mtoto asipewe jina hadi cku akiyokuja yeye? yawezekana alidhani angezaa wengine kirahisirahisi tu na wasichana wengine kumbe uzazi siku hizi kasheshe so akagundua huyo ndo mwanawe.mi ningempa tu jina la bibi yake kwani kuna shida gani?kuna watoto wana majina mawilomawili baba katoa na mama katoa jina na maisha yanasonga.unadhani kweli atamuua?hawezi .
 
Hizo imani za kipuuzi akiziogopa na kumsikiliza huyo mlevi, mdada atajikuta amani hana na anaishia kwa waganga. Mshauri aachane na kumsikiliza mpuuzi, huyo bwana anaweza kuua mtoto wake kweli? Tena ambaye anasaidiwa kulelewa bila gharama? Siamini kama linawezekana, labda amechanganyikiwa na zimeruka.
 
asiwe na wasiwasi hataweza kutatisha maisha ya huyo mtoto hata iweje,dada amuombe Mungu ulinzi na aendelee na shughuli zake huyo mwanaume hajielewi ufahamu wake ni mdogo sana na kwa jinsi hio hatafanikiwa mpango wake kamwe.na ampotezee tu asiwe na mawasiliano nae tena.
 
Kuliko kumpatia mtu aliye na mawazo ya kudhuru au kuua mtoto, ni bora huyo mtoto afe nikimuangalia. Hana lengo la kumtunza huyo mtoto anataka kumkomoa tu huyo dada.
 
Nendeni mkatoe taarifa kituo cha polisi kilicho karibu,kutishia kuua kwa maneno ni kosa la jinai

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Habari zenu jamani, kuna dada yangu mmoja alikuwa na mpenzi wake miaka miwil iliyopita. Mapenzi yao yalidumu lakini ilifikia sehemu wakaanza kukosana kosana kwasababu dada alishindwa kumvumilia yule mwanaume kwa tabia yake ya kunywa sana hadi kupitiliza dada akaamua aachane nae.

Lakini walipoachana ndani ya wiki mbili dada akahisi ana ujauzito kaenda kupima kweli akakuta anaujauzito, akaomba ushauri kwa ndugu na marafiki wengi wao wakamshauir amwambie baba wa mtoto japo hawapo kwenye mahusiano tena.

Dada kaamua kumtafuta na akamueleza kwamba nina mimba yako yule mwanaume alikataa kama hamjui alikataa mimba na akamwambia usinitafute tena kwa huo upuuzi wako.

Dada huyu alivumilia kwa vile alikuwa na kazi yake alilea mimba yake vizuri akisaidiana na ndugu zake mpaka akajifungua salama mtoto mzuri wa kike.

Sasa tatizo ni kwamba mtoto amekuwa hadi sa hivi ana miaka miwili, ndiyo yule mwanaume katafuta namba na kaanza kumtafuta tena huyu dada yangu na wakati kipindi cha nyuma hajawahi kupiga simu hata mara moja.

Amebembeleza dada hataki kumuonyesha mtoto hadi alimtafuta baba wa huyu dada na kuomba msamaha sana watu wakamshahuri aje kumuona angalau mtoto yule bwana karuhusiwa kumuona mtoto baada ya kuomba msamaha sana.

Sasa siku moja akampigia simu akamwambia dada yangu nakuja kesho. Kesho ilipofika hasubui na mapema kampigia dada simu na kuanza kumtukana eti huyo mtoto nimewapa kama zawadi kwanza huyo mtoto hamkumpa jina la mama yangu sidhani kama ni mwanangu ilikuwa pigo jingine tena kwa dada yangu.

Sasa ninavoandika hivi huyo bwana alipiga tena simu kwa baba yake huyu dada akamwambia huyo mtoto ni mal yangu sasa nyie mmeamua kunizurumu hata jina la mtt nilitaka aitwe jina la mama yangu nyie hamja mpa nitaakikisha tunamkosa wote huyo mtoto hata nikimaliza waganga wote tz lkn had nitaakikisha kitoto hicho kinaondoka duniani.

Sasa anaitaji ushauri afanyeje kwa mwanaume huyu nyie wanawake mliozaa mtajisikiaje kama ungekuwa ww nawasilisha jaman....

Mkuu hapo ktk green, ndio ulivoomanisha? Mimi mwanaume, ngoja niwaachie hao waliowataja wacomment!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom