Afisa Mteule Drj 2
JF-Expert Member
- Mar 21, 2017
- 3,961
- 4,663
Angekuwa mwanaume mwenzako amekuomba msosi huo angekuwa ana miplasta usoni mda huu
Haya maisha ya maigizo bana kwel yame waathiri watu sanaSiku ya leo siwezi kuisahau.Nilikua maeneo flani hivi nikapitia restaurant moja hivi kupata chakula cha mchana na njaa ilikuwa imenikamata kwelikweli.
Nimeagiza chakula mhudumu kanihudumia pale vema kabisa ile naanza tu kula akaja Dada mmoja huku kaachia tabasam,akaketi na kunisalimia "kaka samahani naomba hiki chakula chako dk moja tu"nilishtuka kidogo maana jinsi alivyo hadi muonekano wakealivyo vyaa si type yangu kabisa vile ni vyombo vya watu wenye pesa zao.
Basi nilihisi ana njaa nikamsogezea nikaagiza chakula kingine.Mara nikaona mtu yuko busy kafungua mkoba katoa sim Heeee!!!eti badala ale anaaza kupiga maphoto chakula Mara kanipa sim kaka Nipige picha huku kasogeza zile sahan karibu yake,muhudum alivyofika na chakula kingine yule Dada kasepa kajifanya anaenda kunawa jumla.
Nikabaki na mshangao na mashwali mengi nikajikuta nimeshiba gafla bila kula nililipa nikaondoka.
Vipi nyie jaman mlishawai kukutana na vimbwanga kama hivi?