Huyu Dada aliniacha na mshangao!!!

Huyu Dada aliniacha na mshangao!!!

Mr mgeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2014
Posts
1,222
Reaction score
812
Siku ya leo siwezi kuisahau.Nilikua maeneo flani hivi nikapitia restaurant moja hivi kupata chakula cha mchana na njaa ilikuwa imenikamata kwelikweli.

Nimeagiza chakula mhudumu kanihudumia pale vema kabisa ile naanza tu kula akaja Dada mmoja huku kaachia tabasam,akaketi na kunisalimia "kaka samahani naomba hiki chakula chako dk moja tu"nilishtuka kidogo maana jinsi alivyo hadi muonekano wakealivyo vyaa si type yangu kabisa vile ni vyombo vya watu wenye pesa zao.

Basi nilihisi ana njaa nikamsogezea nikaagiza chakula kingine.Mara nikaona mtu yuko busy kafungua mkoba katoa sim Heeee!!!eti badala ale anaaza kupiga maphoto chakula Mara kanipa sim kaka Nipige picha huku kasogeza zile sahan karibu yake,muhudum alivyofika na chakula kingine yule Dada kasepa kajifanya anaenda kunawa jumla.

Nikabaki na mshangao na mashwali mengi nikajikuta nimeshiba gafla bila kula nililipa nikaondoka.

Vipi nyie jaman mlishawai kukutana na vimbwanga kama hivi?
 
Attention ni kitu kibaya sana. She's doing all that ili baadae akapate attention mitandaoni.
 
Atakua shetani uyo!
Mwanamke hata awe mshenzi vipi hawezi kufanya jambo hilo kwa mtu asiemjua
 
Back
Top Bottom