Huyu Dada aliniacha na mshangao!!!

Huyu Dada aliniacha na mshangao!!!

Jaribu kupita insta unaweza ukamkuta na chakula chako[emoji4]
nakupa kazi unisaidie ukikuta kasamaki ka kukaanga,chipsi kavu na juice ya chungwa ni pm uniambie anatumia jina gani
 
Mwenzio alikuwa ana OSHA jina Instagram.......jinga kabisa badala ya kula linakimbilia ma picha picha.
 
Usiemwe na wasi mkuu alikuwa amemdanganya baby wake kuwa nakula mgahawani jamaa akaomba amtumie pics
 
hapo sasa kama ilikuwa wali maharage kaenda kupost kwenye social network ..natafakali huenda status yake aliweka ''mara moja sio mbaya''
 
Kuna ule mwimbo wa samahani naomba nisaidie kushea , binafsi naona ndo anaufanyia kazi huyo binti
 
Ningemtafuta nimtie konde akome kuletea watu ungese ... Nawe hukua na njaa yaani msosi unauachia hivihivi na hela umelipa? Nakula sahani moja .. Moja naomba mfuko natilia ntakula jioni kwanije!
 
Hapo usikute njemba wake amemuuliza upo wapi na yeye kajibu yupo restaurant ndo njemba likamwambia ebu piga picha unitumie ili niamini ndo akaona aje kwako fasta
 
Siku ya leo siwezi kuisahau.Nilikua maeneo flani hivi nikapitia restaurant moja hivi kupata chakula cha mchana na njaa ilikuwa imenikamata kwelikweli.

Nimeagiza chakula mhudumu kanihudumia pale vema kabisa ile naanza tu kula akaja Dada mmoja huku kaachia tabasam,akaketi na kunisalimia "kaka samahani naomba hiki chakula chako dk moja tu"nilishtuka kidogo maana jinsi alivyo hadi muonekano wakealivyo vyaa si type yangu kabisa vile ni vyombo vya watu wenye pesa zao.

Basi nilihisi ana njaa nikamsogezea nikaagiza chakula kingine.Mara nikaona mtu yuko busy kafungua mkoba katoa sim Heeee!!!eti badala ale anaaza kupiga maphoto chakula Mara kanipa sim kaka Nipige picha huku kasogeza zile sahan karibu yake,muhudum alivyofika na chakula kingine yule Dada kasepa kajifanya anaenda kunawa jumla.

Nikabaki na mshangao na mashwali mengi nikajikuta nimeshiba gafla bila kula nililipa nikaondoka.

Vipi nyie jaman mlishawai kukutana na vimbwanga kama hivi?
Haya maisha ya maigizo bana kwel yame waathiri watu sana
 
Back
Top Bottom