Huyu binti ananifanya nikonde

Huyu binti ananifanya nikonde

Huyo mpige chini FASTA. Eti unampenda! Unampenda nini? Wako wengjne maelfu wazuri tu. Kama anakudengulia leo hata hujasema unataka kuanza mchakato wa ndoa ukimwoa akikudengulia utafanyaje? Tena fahamu: Hawezi kukudengulia kama hana mtu mwingine.
 
Ulimkuta na nyuzi?? Una mpendaje mtu mpka uchanganyikiwe na hujamkuta na nyuzi zake? Pole sana ndio moyo husukuma damu tu sio kingine ila huyo kashakuawashia taa nyekundu sasa wewe washa ya kijan usepe na dawa yake tafuta mashine nyingine kali zaid
 
Ukirudi kubembeleza unekwisha. Huyo hakuhitaji. Ukichana naye kwa muda anakuwa na nani? Ukimuoa atakusumbua.
 
uyo piga chini ameshaona hujaona dem mwingine ni yy tu ukiendelea atakusumbua
 
Kuna binti mmoja nilimpata, dah ana bonge la shepu, lkn nae akawa anatabia kama hizo mara tuachane, mara turudiane, utoto mwingi na akabadili namba mara tatu. Nikafikiria hivi hilo shepu lake na amani ya moyo wangu kipi bora, nikaona acha niachane nae baada ya mwezi ananifuata turudiane, yaani mpaka hivi sasa ananibembeleza simu haziishi na mimi nimeshamchomolea mazima, najua huko mbele atanisumbua. Kwa hiyo ndugu thamini furaha na amani ya moyo wako, usizuzuke na uzuri wake, wanawake wapo wengi achana nae.
 
Be
Ndugu zangu,

Awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa kuniweka salama siku ya leo japo hapa nilipo pressure ipo juu kweli kwasababu ya binti ambaye kwa dhati ya moyo wangu niweke wazi napenda sana awe mama watoto wangu kwa muda ambao yeye atakuwa tayari mimi nipo tayari muda wowote.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni hali ngumu na mawazo anayonipa huyu binti sio uwongo ananidengulia sana, ni mwanamke niliye dumu naye kwenye uhusiano kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu lakini nimetokea kumpenda mpaka nimefikia hatua ya kutaka kuoana naye na akanikubalia.

Lakini kwa siku za karibuni zisizozidi wiki mbili amekuwa mtu asiyeeleweka kwa maana ya kwamba anatuma SMS ananiambia tuachane kwa mda kwanza alafu tuendelea baadaye hivyo hivyo nalialia mpaka anabadilisha mawazo. Lakini hiyo tabia ilijirudia kwa mara tatu na mara ya nne nikapiga moyo konde japo naumia moyo nijamjibu kuwa asiwe na tatizo nimekubali kuachana nae kama anavyohitaji.

Lakini leo asubuhi akatuna SMS kwamba hakumaanisha bali ni utani tu na mimi nikamwambia HAPANA acha iwe kama ulivyohitaji mwanzo, akajibu POA.

Lakini ndugu zangu niwe muwazi ili mnishauri vyema huyu binti nampenda sana sana ila niliamua tu kutikisa kiberiti na mimi.

Je, kuna uwezekano ananipenda au ashaniona kilaza na kunifanya mdoli?

Tafadhali nahitaji ushauri wenu.

Mmekuwa pamoja miezi 3 halaf unasema nn ??
 
Tehe tehe tehe pole sana bwana! Kumuacha mtu unayempenda siyo kidogo kama ambavyo wengine wanakushauri 'piga chini', ni sawa mtu kama huyo hupaswi kabisa kulazimisha kuendelea kuwa naye atakusumbua sana sababu ameshajua madhaifu yako. Lakini utamuacha vipi ili usimkumbuke na kupata msongo wa mawazo... Hapa nd'o kuna muziki, kinacholeta shida kwenye mapenzi ni yale mazoea japo unaweza kumpotezea na taratibu utajikuta umemsahau ila kwa kitambo kirefu utakonda kwa mawazo.
 
Jamii kuna ma great thinker's sanaaa.....

Mrejesho baada ya ku apply baadhi ya ushauri kuntu, ushauri jiwe au ushauri ambao kama ni mtu wa kulia lia lazima machozi yakutoke maana hamna kubembelezana ni za uso alafu unapita hivi.

Kila mmoja wenu kwa wakati wake alinishauri kwa namna alivyoona ni bora zaidi ili kunitoa kwenye msongo wachache pia kama ilivyo ada kwenye msafara wa mamba kenge na mijusi huwa hawakosi walishusha mitusi yao japo sikuathirika zaidi nilipuuza tu.

Eeeeeeeh bwanaaaa nili nyuti kama wengi wenu mlivyo nishauri na nimeamini ni njia bora kabisa ya Ku handle situations kama zangu yaani binti wa watu sasahivi ni anapiga simu na anatuma sms za ku apologize za kutosha lakini jitu sina habari nazo japo ka moyo kana dunda dunda kwa mbali lakini nimeona hamna kulegeza maana itani cost. Nimeweka nguvu kwenye kusaka noti sio mambo ya kijinga kama walivyoelekeza baadhi ya wachangiaji humu, ukiwa na pesa watakuja tu au hawatasumbua.

Niwaambie tu huduma zote nazikata hawezi nifanye babake at the same time aniletee ungese ngese nimeamua kufanya kama TANESCO walivyofanya ARUSHA hamna kuangalia usoni na naamini kwa jinsi alivyonifanya guardian lazima namba ataisoma sawasawa.

Hapa navyoandika huu mrejesho ni sms tu zinafululiza mi sina habari narudisha feedback barabara.
 
Sasa mapenzi ya kuachana na kurudiana ya kazi gani. Hata hujajiuliza kama mkiachana kipindi unachosubiri kurudiana atakuwa na nani?

Hebu jiongeze nawewe.
..mapenzi washa zuma kama umeme wa Tanesco..
 
inauma kufanyiwa ivo.
baasi tu macho ya rohoni ndo uhaba tulionao.

nakushauri usilazimishe kitu hujui Mungu anakuepusha na nini?
 
Achan ukooo mwaya maan kinachofata apo ni sukari na presha ufe kabla ya siku
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom