Huyu binti ananifanya nikonde

Huyu binti ananifanya nikonde

Mkuu, kwani ulishawahi kula mzigo? Inawezekana basi kiwango chako hakikumkuna. Jaribu kuimprove pia kwenye hiyo sekta...
 
anayekupenda hawezi kukutania miutani ya hivyo iliyovuka mipaka mwache aende mwanzoni utaumia sbbu umemzoe badae utamsahau pole sana mkuu huna mpenzi hapo ila ni jaka moyo kupeana presha tu
Huyo bila shaka atakuwa ana umri kati ya miaka 18-20
 
anayekupenda hawezi kukutania miutani ya hivyo iliyovuka mipaka mwache aende mwanzoni utaumia sbbu umemzoe badae utamsahau pole sana mkuu huna mpenzi hapo ila ni jaka moyo kupeana presha tu
Afanye nini ili aweze ku cope hali ya atakayokuwa nayo baada ya ku break up. Hapo ndiyo shida yake kubwa ilipo.
 
Ana umri gani?
Mana kuna mmoja alishaniletea kama hizo
Nilichomwambia ni kuwa we nenda utakapo komaa akili na kujiona uko tayari njoo uniambie kuwa umeshakuwa sasa niko tayari.
me namwangalia tu sasa hivi
Anaendeleaje kwa sasa
 
Ndugu zangu awali ya yote napenda kumshukuru Mungu kwa kuniweka salama siku ya leo japo hapa nilipo pressure ipo juu kweli kwasababu ya binti ambaye kwa dhati ya moyo wangu niweke wazi napenda sana awe mama watoto wangu kwa muda ambao yeye atakuwa tayari mimi nipo tayari muda wowote.

Kilicho nisukuma kuandika uzi huu ni hali ngumu na mawazo anayonipa huyu binti sio uwongo ananidengulia sana, ni mwanamke niliye dumu naye kwenye uhusiano kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu lakini nimetokea kumpenda mpaka nimefikia hatua ya kutaka kuoana naye na akanikubalia. Lakini kwa siku za karibuni zisizozidi wiki mbili amekuwa mtu asiyeeleweka kwa maana ya kwamba anatuma sms ananiambia tuachane kwa mda kwanza alafu tuendelea baadaye hivyo hivyo nalia lia mpaka anabadilisha mawazo. Lakini hiyo tabia ilijirudia kwa mara tatu na mara ya nne nikapiga moyo konde japo naumia moyo nijamjibu kuwa asiwe na tatizo nimekubali kuachana nae kama anavyohitaji.

Lakini leo asubuhi akatuna sms kwamba hakumaanisha bali ni utani tu na mimi nikamwambia HAPANA acha iwe kama ulivyohitaji mwanzo, akajibu POA.

Lakini ndugu zangu niwe muwazi ili mnishauri vyema huyu binti nampenda sana sana ila niliamua tu kutikisa kiberiti na mimi. Je kuna uwezekano ananipenda au ashaniona kilaza na kunifanya mdoli?

Tafadhali nahitaji ushauri wenu.
Mkuu hakuna kitu kizuri kama unaempenda naye anakupenda,, lakini huyo nakushauri jitahidi umsahau,
Huyo hajaingia kwenye yupo hivo vipi akishakuwa. Ktk ndoa,, by the way huyo tayari kuna mtu ana GEGEDA bila hata huruma,,so temana naye,
Halaf inaonekana unamhonga sana!! Ndo maana naye yupo kama anasitasita kukuacha
 
Kiundani kabisa inaonekana wewe bado akili yako haijakomaa vizuri kwenye suala zima la mahusiano, na pia hujawaelewa vizuri wanawake. Ukikua utaacha
 
Tambua pia Mungu aliwaumba wagonjwa wa akili,
na wengine tunaishi nao bila kujijua. Think twice
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom