Huyu alikuwa ni hazina ya CHADEMA

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Nikiri kuwa huyu Mtanzania alikuwa ni hazina ndani ya CHADEMA lakini kinachoshangaza ni kuona Viongozi wakuu wa CHADEMA wakishindwa kutimiza malengo yake.

Wakati mwingine ni vizuri kutoa pongezi pale unapoona adui yako anafanya vizuri. Nawapa pongezi CHADEMA kwa kuwapa CCM kijana ambaye ni hazina ya kisiasa.

Huyu kijana anafaa sana kuwa Katibu Mwenezi wa CCM kutokana na uwezo wake katika majukwaa ya kisiasa.

Ni kweli CHADEMA wana baadhi ya vijana ambao ni wazuri sana kisiasa lakini kwa sasa wanajiunga CCM kutokana na yanayotokea ndani ya chama.

Angalia hii video inayoonyesha uwezo wa huyu kijana katika jukwaa la kisiasa.

[MEDIA]
 
Hivi kweli Bilioni zaidi ya tatu kwa mwaka akina Mbowe walishindwa kumpa ulinzi Tundu Lissu pamoja na kuwa alishatoa taarifa?
Hapa hatuna sababu kabisa ya kuwalaumu wasiojulikana.
Chama chenyewe hakikujali kabisa tishio la mwanansheria wake, na sasa hata kumlipia matibabu wanachangisha watu kweli?
 
Huyu asiyejua kazi za vyama vya upinzani, anawauliza wananchi CHADEMA wanaweza kujenga barabara? ....... Njaa tu huyu aliishi kwa pesa za Ndesambulo. Ajira shida, uchumi umeshuka chari biashara haziendi. Uchaguzi ukiisha sijui hata nauli ya kurudi Moshi atapata. Anaweza taja chama cha upinzani dunia kilichojenga barabara bila kuwa madarakani, bila kukusanya mapato ya nchi. Wakati mwingine unajuta kuzaliwa Tanzania.
 
Kwa nini unajuta kuzaliwa Tanzania wakati siku hizi kubadili uraia ni sawa na kubadili nguo.

Residence permit ya Burundi ya miaka 99 unaipata ukitoa dora 1000
 
Hivi kweli Bilioni zaidi ya tatu kwa mwaka akina Mbowe walishindwa kumpa ulinzi Tundu Lissu pamoja na kuwa alishatoa taarifa?
Hapa hatuna sababu kabisa ya kuwalaumu wasiojulikana.
Chama chenyewe hakikujali kabisa tishio la mwanansheria wake, na sasa hata kumlipia matibabu wanachangisha watu kweli?

Mkuu,wewe unawaza kwanini hakuwekewa ulinzi,!!!Wenzio walikuwa wakikereka saaana TL alivokuwa akiwika kwenye bunge,medias,kwa wananchi na kila kona nchini TZ utaskia jina la Lisu
Mkuu,wewe unawaza atibiwe kwa pesa ya chama,? Hujiulizi kwann walimktalia Mh Wazir wa Afya baada ya kuwaambia tumpeleke muhimbili na tufate taratibu za kiserikali akimaanisha lolote litakalotokea.itakuwa ni jukumu la serikali kumsimamia mgonjwa.Lkn viongozi wa CDM waligoma tena na kuonesha jeuri kabisa kukodi ndege na kumwahisha kenya.Je hujiulizi hapo??alipokuwa hoi mahututi hana fahamu alipelekwa kenya
Mungu kasaidia kampa afya njema kaanza kuongea na kuchangamka kaweza na kusimama,kula chakula kuongea na waandishi wa habari ati ndio wamempeleka ubelgiji
Hapo ndio ujue kufa ni kufaana
Jamaa wameshamfanya ATM mwenzao
 
Huyu asiyejua kazi za vyama vya upinzani, anawauliza wananchi CHADEMA wanaweza kujenga barabara? ....... Njaa tu huyu aliishi kwa pesa za Ndesambulo. Ajira shida, uchumi umeshuka chari biashara haziendi. Uchaguzi ukiisha sijui hata nauli ya kurudi Moshi atapata. Anaweza taja chama cha upinzani dunia kilichojenga barabara bila kuwa madarakani, bila kukusanya mapato ya nchi. Wakati mwingine unajuta kuzaliwa Tanzania.

Tuachane na ushabiki wa kisiasa mimi binafsi sina chama chochote
Lakini lazima tutafakari huyu jamaa alichokisema kwakweli ni maneno mazito saana,na yapo wazi.Yaani wanapeana hadi Ubunge wa viti maalum,!!!
Kumbe chama kilikuwa cha babamkwe,!!duuhh!!!
Hio hoja ya barabara alisema kama mfano tu,hata hoja ya kujenga choo yote ni mifano tu,ila hio ya wabunge kutoa milion na nusu kila mwezi na ruzuku ya chama,aseee ni kali saana,
Kumbe tokea 2015 hadi leo 2018 chama kimeshaingiza bilioni 15
Duuhh,!!ndio maana hata wakivunjiwa majumba yao(billicanas)wakipokonywa mashamba yao wenyewe wapo tu,hawakiachii chama.
Mmhh kumbe kuna ulaji kinoowmaa
 
Niliwahi kuandika hapa, hamahama ya madiwani na wabunge Upinzani ni kulazimishwa michango inayotokana na posho zao. Wakilalamika wanaambiwa usingezipata kama sio chama kukupa nafasi uliyonayo. Milioni moja na nusu kwa mwezi unalazimishwa kutoa kama vile viongozi hao hawana matatizo yao binafsi ya uhitaji. Mbaya zaidi wameanzisha nafasi za uongozi ambazo haziwakilishi wanachama. Mfano, Viongozi wa kanda ni mzigo kwa wenyeviti was mikoa na wilaya, hawana wanachama lakini wana nguvu na mamlaka kuliko viongozi wa kuchaguliwa wenye watu. Na kwa kua wao ni foresight ya Makao Makuu matokeo yake ni kunawatisha wenzao watoe pesa la sivyo watawaondoa ktk nafasi zao. Huo ndio udikiteta unaokimaliza chama Iringa Mjini na kwingineko sio kununuliwa. Wanaona afadhari kuziacha hizo posho zao kuliko kendelea kuwafanyia kazi na malipo ya jasho lao linaliwa na watu wengine kwa kisingizio cha kuimarisha chama.
 
Chadema maslahi hamna ndo mana watu wanahama...hata ningekuwa mimi kama silipwi lazima nikuimbie cha kwanza kula mengine yanafuata

Kinachoendelea chadema kiukweli kinahizunisha sawa now..lkn ndo uhalisia huo
 
Hivi kweli Bilioni zaidi ya tatu kwa mwaka akina Mbowe walishindwa kumpa ulinzi Tundu Lissu pamoja na kuwa alishatoa taarifa?
Hapa hatuna sababu kabisa ya kuwalaumu wasiojulikana.
Chama chenyewe hakikujali kabisa tishio la mwanansheria wake, na sasa hata kumlipia matibabu wanachangisha watu kweli?
Wameshindwa hata kununua thamani za Ofisi. Wanalipa madeni kwanza na kumkusanyia bwana Mkubwa fedha za kugombea urais 2020
 
Hivi kweli Bilioni zaidi ya tatu kwa mwaka akina Mbowe walishindwa kumpa ulinzi Tundu Lissu pamoja na kuwa alishatoa taarifa?
Hapa hatuna sababu kabisa ya kuwalaumu wasiojulikana.
Chama chenyewe hakikujali kabisa tishio la mwanansheria wake, na sasa hata kumlipia matibabu wanachangisha watu kweli?
Mkuu;

Hujui kama Mbowe ni mfanyabiashara?

Fikiria hata kutibiwa imebidi Mbowe achangishe badala ya kuchukua kwenye pesa ya ruzuku!
 
Hivi kweli Bilioni zaidi ya tatu kwa mwaka akina Mbowe walishindwa kumpa ulinzi Tundu Lissu pamoja na kuwa alishatoa taarifa?
Hapa hatuna sababu kabisa ya kuwalaumu wasiojulikana.
Chama chenyewe hakikujali kabisa tishio la mwanansheria wake, na sasa hata kumlipia matibabu wanachangisha watu kweli?
Hivi nikuulize...mwenye jukumu la kulinda usalama wa raia ni nani?
Kama polisi yenye jukumu hilo haikufanya hivyo..unataka vyama vya siasa vifanye? Vyama vya siasa vina train majeshi ya ulinzi?
Be serious kiasi kidogo basi...
 
Tatizo sio yanayotokea ndani ya chama ndio inafanya waame NO, wengi waliopo wanatafuta ugali unategemea mtu aendelee kupigika wakati upande wa pili kuna neema...
Pesa sabuni ya roho

Sasa kama viongozi wakuu wa CHADEMA hawatoi hiyo pesa kuwalipa wafanyakazi wake wakati wanapokea bilioni 15 huoni kuwa ni tatizo ndani ya CHADEMA
 
Back
Top Bottom