Huyu alikuwa ni hazina ya CHADEMA

Huyu alikuwa ni hazina ya CHADEMA

Chadema Ni taasisi ya umma inaendeshwa kwa kutumia kodi za wananchi hivyo tunahaki ya kujua mapato na matumizi ya Chama.

Kama chama cha upinzani chenye nia ya kushika dola kilitakiwa kuwa mfano kwa vyama vyote hasa chama tawala.

Lakini mpaka kwa leo bado inaonekana Chadema wanarudi kujifunza siasa kwa ccm hatua ambayo walishatoka kabla ya ujio wa Lowasa.
Bado point yako haieleweki ...
Toa na ushahidi kwamba hao chadema wanajifunza kwa CCM
Na Lowasa ameingiaje hapa.
Hilo la matumizi nimekueleza ufike ofisini kwao hao jamaa.
 
Nyani haoni kundule
Hussein mwingi
Mrs malesela
January makamba
Adam malima
Rtz kikwete
Mrs kikwete
...
....
......
Makarai mlio kimbia mpoo!!!!!!
 
Chadema maslahi hamna ndo mana watu wanahama...hata ningekuwa mimi kama silipwi lazima nikuimbie cha kwanza kula mengine yanafuata

Kinachoendelea chadema kiukweli kinahizunisha sawa now..lkn ndo uhalisia huo
Ni bora kama wafanyakazi wote wasingekuwa wanalipwa lakini kwa sasa kuna baadhi yao wanafaidika sana na pesa za ruzuku huku wengine wakiishia kubeba madeni binafsi katika kukihudumia chama.

15 bilioni ni pesa nyingi sana!
 
Chadema ni kama SIMBA SPORTS CLUB kuna vijana wengine wenye uwezo mkubwa wapo wengi........vipi kuhusu wewe hapo lumumba bado unauza kapelo na scuff mpaka leo??
Unalinganisha siasa na vilabu vya mpira?

Siasa zinagusa maisha ya kila mmoja wetu wakati michezi ni burudani yenye dhana ya kama itapendeza!

Sioni mantiki ya Simba Sports Club na vyama vya siasa
 
Wameshindwa hata kununua thamani za Ofisi. Wanalipa madeni kwanza na kumkusanyia bwana Mkubwa fedha za kugombea urais 2020

Wewe Benson Mramba ni mtu mpumbavu ambaye nimekujua tangu muda mrefu, wewe uliachishwa kazi makao makuu ya CHADEMA kwa ufisadi, ulitumia pesa za kampeni ya Kalenga kulala na wake za watu, mmoja ni yule aliyeolewa na tumbili. Ulifanya utapeli wa milioni tano kwa ajili ya matengenezo ya gari la ofisi ya Kanda ya Kaskazini, ulifanya wizi wa fedha za kusafirisha pikipiki za chama kwenda kwenye wilaya na majimbo mwaka 2013, ulifanya wizi wa fedha kwenda TRA kwa ajili ya usajili wa pikipiki za chama. Nitakulipua zaidi kabla ya mwezi wa nne....mpumbavu wewe ulieachishwa kazi TANROAD kwa ajili ya wizi...
 
Mimi binafsi ni mpigakura wa chadema toka nkiwa na miaka 17, hayo mengine aliyoongea jamaa ni siasa za siasa tu... Na ufinyu wake wa akili... Lkn swala la chadema kutokuwa na ofisi ya milioni mia saba, ni fedheha kubwa.... Hii mana yake ruzuku ikipungua basi chama lzm kife, mana hata kodi ya kulipa Pango haitakuwepo, ila wangejenga ofisi hata kila mkoa tu tena zile za kawaida tu..... Ingekuja kusaidia ken mazingira yyt ya kisiasa huko mbeleni lkn kwa hali hii itasumbua...... Bilioni 3 per year ni nyingi sana lzm zipatiwe maelezo ya kutosha.......
 
Niliwahi kuandika hapa, hamahama ya madiwani na wabunge Upinzani ni kulazimishwa michango inayotokana na posho zao. Wakilalamika wanaambiwa usingezipata kama sio chama kukupa nafasi uliyonayo. Milioni moja na nusu kwa mwezi unalazimishwa kutoa kama vile viongozi hao hawana matatizo yao binafsi ya uhitaji. Mbaya zaidi wameanzisha nafasi za uongozi ambazo haziwakilishi wanachama. Mfano, Viongozi wa kanda ni mzigo kwa wenyeviti was mikoa na wilaya, hawana wanachama lakini wana nguvu na mamlaka kuliko viongozi wa kuchaguliwa wenye watu. Na kwa kua wao ni foresight ya Makao Makuu matokeo yake ni kunawatisha wenzao watoe pesa la sivyo watawaondoa ktk nafasi zao. Huo ndio udikiteta unaokimaliza chama Iringa Mjini na kwingineko sio kununuliwa. Wanaona afadhari kuziacha hizo posho zao kuliko kendelea kuwafanyia kazi na malipo ya jasho lao linaliwa na watu wengine kwa kisingizio cha kuimarisha chama.
Kwa hiyo vitu maalum wanasaini rushwa mbili, 1.5m na ngono?
 
Alafu alivyokuwa na upeo mdogo eti anasema ruzuku CHADEMA wanapewa na serikali ya CCM wakati ni takwa la sheria ambalo hata kma ingekuwa serikali haupendi upinzani kiasi gani lazima wasign pesa zitoke ila huyu anadanganya watu kana kwamba ni fadhila ya CCM

Badala awaambie nini mtulia atafanya anaishia kuwaambia "ubaya" wa chama alichotoka.... Inashangaza sana mkuu
Huyu jamaa ana njaa nyekundu, hovyo kabisa. Kila mmoja akianza kusakanya madhaifu ya kila upande kuna chama kitabaki salama? Hivi ni nani anajua ruzuku ya ccm pamoja na michango ya wabunge wake ni kiasi gani na matumizi yake ni yapi? Vijana wafanye kazi waache kusubiria kubebwa bebwa na kulamba nyayo za wakubwa.
 
Hivi kweli Bilioni zaidi ya tatu kwa mwaka akina Mbowe walishindwa kumpa ulinzi Tundu Lissu pamoja na kuwa alishatoa taarifa?
Hapa hatuna sababu kabisa ya kuwalaumu wasiojulikana.
Chama chenyewe hakikujali kabisa tishio la mwanansheria wake, na sasa hata kumlipia matibabu wanachangisha watu kweli?
Mabilioni mengi ya serikali yalishindwa kumpa ulinzi Waziri Mkuu wa zamani Moringe Sokoine na mabilioni ya kutosha yalishindwa kumpa ulinzi rais wa kwanza wa Zanzibar Karume.
 
Tuwekee vielelezo pia kama uthibitisho.
Unataka vielelezo gani zaidi ya kilichosemwa na aliyekuwa Katibu wa Kilimanjaro!

Au unadhani huwa kuna document kuonyesha kuwa pesa hazipelekwi kwenye mikoa na wilaya!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Wakati naanza kusoma mkuu nikajua jambo la maana sana au nikajua huyo kijana unayemsemea sijui ni nani......
Mkuu;

Ndiye huyo ambaye kwa jicho la pili unaweza kugundua kuwa ni hazina ya kisiasa nchini.
 
Nikiri kuwa huyu Mtanzania alikuwa ni hazina ndani ya CHADEMA lakini kinachoshangaza ni kuona Viongozi wakuu wa CHADEMA wakishindwa kutimiza malengo yake.

Wakati mwingine ni vizuri kutoa pongezi pale unapoona adui yako anafanya vizuri. Nawapa pongezi CHADEMA kwa kuwapa CCM kijana ambaye ni hazina ya kisiasa.

Huyu kijana anafaa sana kuwa Katibu Mwenezi wa CCM kutokana na uwezo wake katika majukwaa ya kisiasa.

Ni kweli CHADEMA wana baadhi ya vijana ambao ni wazuri sana kisiasa lakini kwa sasa wanajiunga CCM kutokana na yanayotokea ndani ya chama.

Angalia hii video inayoonyesha uwezo wa huyu kijana katika jukwaa la kisiasa.

[MEDIA]

Huyu ni victim wa ujinga. Alikuwa hajui alipo na kwa nini yupo. Kwa sasa hajui la kufanya na baadaye atakuja kujua kuwa kumbe ni mjinga.
Mleta mada unapamba wajinga kwa vile unawahusu na wanakuhusu.
Soma mada ya Paskali ya Ccm kuendelea kuchaguliwa
 
Mabilioni mengi ya serikali yalishindwa kumpa ulinzi Waziri Mkuu wa zamani Moringe Sokoine na mabilioni ya kutosha yalishindwa kumpa ulinzi rais wa kwanza wa Zanzibar Karume.
Mkuu una maana hata sisi hatuna tofauti na maCCM?
Tunapiga madili tu kama wao?
 
Mtu kutoka chadema kurudi ccm ni sawa sawa kurudi nyuma hatua 10 na kwenda Mbele hatua mbili na kujipongeza.
Fikra ni zako na una haki ya kufikiri lakini huna uwezo wa kubadilisha ukweli.

Inawezekana umeandika bila kujua maana ya zero-sum politics
 
Back
Top Bottom