Nikiri kuwa huyu Mtanzania alikuwa ni hazina ndani ya CHADEMA lakini kinachoshangaza ni kuona Viongozi wakuu wa CHADEMA wakishindwa kutimiza malengo yake.
Wakati mwingine ni vizuri kutoa pongezi pale unapoona adui yako anafanya vizuri. Nawapa pongezi CHADEMA kwa kuwapa CCM kijana ambaye ni hazina ya kisiasa.
Huyu kijana anafaa sana kuwa Katibu Mwenezi wa CCM kutokana na uwezo wake katika majukwaa ya kisiasa.
Ni kweli CHADEMA wana baadhi ya vijana ambao ni wazuri sana kisiasa lakini kwa sasa wanajiunga CCM kutokana na yanayotokea ndani ya chama.
Angalia hii video inayoonyesha uwezo wa huyu kijana katika jukwaa la kisiasa.
[MEDIA]
Bora hao wanasema ndiooo!Masikitiko yangu kwa wale wanaosikika kwenye background wakisema ndiooo, semaaaa nk.
Wao wanaburuzwa tu huyo mjinga akishuka hapo account ishasoma manoti.
Bora hao wanasema ndiooo!
Kuna wengine huzungusha mpaka mikono na viuno huku wakideki barabara!
Kwahiyo lengo lenu la kuwavunjia miradi yao lilikuwa ni njia ya kuwafanya warudi kwenye chama chetu cha mauaji ccm.!?Tuachane na ushabiki wa kisiasa mimi binafsi sina chama chochote
Lakini lazima tutafakari huyu jamaa alichokisema kwakweli ni maneno mazito saana,na yapo wazi.Yaani wanapeana hadi Ubunge wa viti maalum,!!!
Kumbe chama kilikuwa cha babamkwe,!!duuhh!!!
Hio hoja ya barabara alisema kama mfano tu,hata hoja ya kujenga choo yote ni mifano tu,ila hio ya wabunge kutoa milion na nusu kila mwezi na ruzuku ya chama,aseee ni kali saana,
Kumbe tokea 2015 hadi leo 2018 chama kimeshaingiza bilioni 15
Duuhh,!!ndio maana hata wakivunjiwa majumba yao(billicanas)wakipokonywa mashamba yao wenyewe wapo tu,hawakiachii chama.
Mmhh kumbe kuna ulaji kinoowmaa[emoji1321]
We acha kufananisha Simba SC na vitu vya kijinga kama ChademaChadema ni kama SIMBA SPORTS CLUB kuna vijana wengine wenye uwezo mkubwa wapo wengi........vipi kuhusu wewe hapo lumumba bado unauza kapelo na scuff mpaka leo??