Huwa unafuata Sheria zipi au Utaratibu upi Mara uitwapo kwenye Mjumuiko (Jamii ya watu) ya watu au Date?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
May 10, 2012
8,606
17,783
Ni swali kwa wote ila Nitaanza na Sheria chache najua kuna wajuzi wengi wataziongezea..
  1. Ukiomba kuonana na mtu eleza shida yako usimletee aliyekuita/Waliokuita umbea.
  2. Fika eneo la kukutania Kabla yake na Kama utachelewa mjulishe mapema ukiwa na sababu za msingi.
  3. Ukiwakuta watu wamekaa mahali wawili au zaidi na wako kwenye mazingira official kana kwamba wanajadili jambo, wasalimie kisha waombe Kama unaweza kujumuika nao (kama unahitaji). Usijikalishe tu pengine watu hawakuhitaji wanateta jambo.
  4. Ukikaa mahali na watu hasa ambao sio watu wako wa karibu, soma mazingira jua wakati wa kuondoka.
  5. Usikae mpaka wakuombe uende ama wao waondoke. Ukishaona hakuna kitu cha maana tena mnachofanya au kuzungumza, waage waondoke hatakama unaenda kuzurura.
  6. Usiongee kama huna point ya maana.
  7. Usiongee Kama hujaombwa kuongea. Ikiwezekana kuwa wa mwisho kuzungumza na zungumza kwa ufupi.
  8. Usikae Kinyonge Kwenye Mkusanyiko wa watu.
  9. Usizungumze hovyo na usizungumze bila mipaka lakini pia usione pia kwamba huwezi kuongea jitu cha maana,Kwani point unayoogopa kuitoa ndiyo yenye msaada na huenda mtu mwingine akaizungumza
Wadau zingine tuongezee ili tuokoe Jahazi la Vijana wa leo
 
Back
Top Bottom